Hivi nyie wanadamu kwanini hampendi kuona watu wakifurahi eti?

Hivi nyie wanadamu kwanini hampendi kuona watu wakifurahi eti?

Ndio uko sahihi ila kwa ladies sio rahisi sana na inategemea na mahusiano ya watu hao, halafu issue ya ku-cutt off watu nilikuwa nayo aisee kuna muda unabaki mwenyew.. nilikuwa na kaujeuri hako! Inafika mahali u need people too sio makwazo kdg u leave, nikazoea saiz tunaishi nao tu! Utaachana na wangapi? Ulimwengu huu watu waaminifu wachache mno..! Ukisema uchunguze huwezi kumpata ni kama ndoa tu😅
Punguza na usimtegemee binadam kwa lolote
 
unaujua ule wimbo wa nyota ndogo? kuna watu na viatu

Lyrics of Watu Na Viatu by Nyota Ndogo​

Rafiki yangu mpendwa naja kwako siku nyingi
wanipokea kwa uzuri siku zote
wakati sina wanipa nitakacho husiti
nisemacho kwako sawa waniombea mungu
moyoni mwangu najua nina rafiki huyu wa kweli
hakuna yule ambaye atakuja kati yetu
wakati sina wanipa nitakacho husiti
nisemacho kwako sawa waniombea mungu
Ooh kuna watu na viatu duniani
ooh kuna watu wasiopenda maendeleo
ooh ukiwa nacho chawauma ndani kwa ndani
achana nao, waepuke haraka sana

Hivi majuzi nilipata kazi nzuri nikaja kukueleza
mtu wa kwanza nilifikiria ni wewe rafiki yangu
nilifurahi na kuruka na kutaja jina lake mungu
nikikuangalia mwako usoni usoni umejisononesha
Ukaanza kusonya ukirusha mikono
sura umeikunja kumbe hukufurahi
mafanikio yangu nilikuachi mimi kuja kukueleza
x2
Mtu wa kwanza mimi kumfikiria ni we rafiki yangu
Ooh kuna watu na viatu duniani
ooh kuna watu wasiopenda maendeleo
ooh ukiwa nacho chawauma ndani kwa ndani
achana nao, waepuke haraka sana
(repeat to end)
Writer(s): Nyota Ndogo
 

Lyrics of Watu Na Viatu by Nyota Ndogo​

Rafiki yangu mpendwa naja kwako siku nyingi
wanipokea kwa uzuri siku zote
wakati sina wanipa nitakacho husiti
nisemacho kwako sawa waniombea mungu
moyoni mwangu najua nina rafiki huyu wa kweli
hakuna yule ambaye atakuja kati yetu
wakati sina wanipa nitakacho husiti
nisemacho kwako sawa waniombea mungu
Ooh kuna watu na viatu duniani
ooh kuna watu wasiopenda maendeleo
ooh ukiwa nacho chawauma ndani kwa ndani
achana nao, waepuke haraka sana

Hivi majuzi nilipata kazi nzuri nikaja kukueleza
mtu wa kwanza nilifikiria ni wewe rafiki yangu
nilifurahi na kuruka na kutaja jina lake mungu
nikikuangalia mwako usoni usoni umejisononesha
Ukaanza kusonya ukirusha mikono
sura umeikunja kumbe hukufurahi
mafanikio yangu nilikuachi mimi kuja kukueleza
x2
Mtu wa kwanza mimi kumfikiria ni we rafiki yangu
Ooh kuna watu na viatu duniani
ooh kuna watu wasiopenda maendeleo
ooh ukiwa nacho chawauma ndani kwa ndani
achana nao, waepuke haraka sana
(repeat to end)
Writer(s): Nyota Ndogo
ewaaaa
 
mnafiki uyo alikua anazuga tu kuwa anahuzunika lakini nyuma ya pazia alikua anafurahia matatizo yako..
 
Ulimwengu Rakadha...Watu Jalili....Watu Kabiri...Ni Adhimu Mnoo Nyakati Hizi...Kaa Kitaalamu Haswa....​
 
Hahaha

Nimecheka sana unajua sisi binadamu bwana tuna kitu kimoja ila kabla sijakisema nataka niseme kitu kimoja, kuna siku nilikua naongea na Mzee wangu nikamtonya kwamba hapa street kuna baadhi ya watu nikikatisha maeneo yao hua wananisema nikipita au wengine nikiwasalimia hawaitikii kabisa, sio kwamba mimi ninajiona no ila napenda kuishi vizuri na watu, jibu la kwanza alilonipa Mzee ni kwamba "hao ni Wachawi", nikamuuliza sasa km ni wachawi kwanini nikipita wanachukia au wananisema au wengine wanajikoholeesha tu?

Akasema "ukiona hivyo wamejaribu kukuroga kwa kila mbinu na kila namna ila sasa wamekushindwa ndio maana wanakua hivyo" ikabidi nitulie akaongeza "wale ambao utapita na watakuzogoa nyuma ukishapita watu wana mambo yao wao wataongea maneno mawili matatu kukuhusu kisha watarudi kwenye shida zao kwa hio usiweke focus yako kwa watu wewe focus zaidi na maisha yako maana hata ukifa leo wapo watakao lia wapo watakao omboleza lakini hakuna hata mmoja ambae atakua tayari kufa kwa ajili ya wewe yaani wewe umekufa na yeye afe ili mzikwe pamoja huyo hayupo"

Mkuu Leejay49 usisikize watu wewe focus na maisha yako maana hata ukifa kesho utaakua umeshasahaulika ndani ya mwezi mmoja tu kila mtu ataendelea na habari zake zingine
 
Binadamu asilimia kubwa huwa wanapata burudani kwenye matatizo ya watu. Akifahamu tu fulani ana tatizo basi stress zake zote kwishaaa
Yaaan acha tuu...Kuna mtu aliwahi niambia Kwa kuwa hamjapata matatizo muda mrefuu ndio maana limetokea hili...Nikajiuliza amejuaje hatuna matatizo?..Ila walimwengu 🙌
 
Ni kwamba wewe ulichelewa kumgundua huyo mtu kuwa ni adui yako, kama hahusiki kukusababishia tatizo ulilokuwa nalo, bas anamfahamu mhusika au chanzo.

Katika watu usipende kuwaamini ni watu wanaojionyesha wema sana, watu wa dini.

Mungu mfuate wewe kama wewe, ukiwa peke yako, masuala ya kumfuata Mungu kwa kikosi uyaache.

Watu wanaojionesha kumpenda sana Mungu, wana mambo yakifunuliwa kwako, utazimia...
Exactly 💯
 
Back
Top Bottom