Hivi Padri mtuhumiwa wa ubakaji na yeye ana Wakili?

Ndio maana lazima upelelezi ufanyike na ikathibitishwe pasipo shaka mbele ya mahakama. Unaweza ukawa na bifu na watu wakakutegenezea zengwe usijue pa kutokea au ukategwa na wewe ukajaa.
Watu wamejawa na mihemko, kisa tu mtuhumiwa ni Padre! Yaani wanawachukulia hao Mapadre kama Malaika vile! Kumbe ni binadamu tu kama walivyo binadamu wengine. Kwa sisi tuliopitia huko seminarini, tunafahamu!
Isitoshe haya matukio yametapakaa kila sehemu! Yanafanywa na watu kutoka makundi yote katika jamii! Na hayafanywi na hao Mapdre pekee wa Katoliki.

Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani! Ni wakati sasa wa kusubiria hiyo mahakama kutenda haki. Na kama kuna upande hautaridhika na maamuzi ya mahakama, bado kuna nafasi ya kukata rufaa kwenye mahakama za juu.

 
Mtu anakurupuka eti anyongwe. i.e. auawe. Je, Mtuhumiwa kaua nani? Tuache mihemko na kuiachia mahakama itende wajibu wake kwa mujibu wa sheria zilizopo. Usiporidhika kakate rufaa.
 
Huo ndio ukweli na hizo ndizo taratibu za kuzingatia.
Laiti watu (hususan wale wenye mihemko) wangelitumia muda wao walau kidogo wajisomee historia ya kanisa na lilikopitia hadi hapa tulipo 2022 wasingeliona ni kitu cha ajabu sana kwa padre kutenda makosa likiwepo na hili linalotrend kwa sasa.
 
Zipo kesi nyingi za kutengenezwa (kusingiziwa). Shukuru Mungu hayajakufika. Ukweli utabainika na kuwekwa wazi. Tuache kuhukumu kwa mihemko
 
Ni mara ngapi sheria inapindishwa hata kama ushahidi ni wa ukweli? Mimi nasema kama ushahidi upo basi sheria ichukue mkondo wake yani pasiwe na kuchelewesha hukumu.
Kuna kesi nyingi tu huwa zinatengenezwa (kusingiziwa). Wote walipo jela usifikiri wameenda kwa haki
 
Ndiyo, na cha kusikitisha sheria hiyo hiyo inaweza ikamkuta hana hatia...
 
Kazi ya wakili ni kubadilisha ukweli kuwa uongo,na uongo kuwa ukweli.
Inategemea umemfuata vipi
 
Wamepambiwa watu kupenda wanawake, Mali, watoto, dhahabu na fedha........

Kwa hakika kwa mwanaume aliyekamilika kwa maana ya rijal kutokuwa na mwanamke ni mtihani sana pia ni katika Sera fikirishi sana katika madhehebu ya ukatoriki.

Nipo kiuhalisia sipo kidini, wanaume watakuwa ni mashahidi kwangu juu ya hilo

Ikiwa ni kweli, basi huo ni uchafu wa wazi na hatua Kali sana juu yake zichukuliwe ikiwa sio kweli, basi ni khery kwake
 
Kwenye sheria kila mtu hana hatia mpaka akutwe na hatia.

Everyone is innocent until found guilty.

Hawafungi kizembe tu..je kama alisingiziwa..je kama alilazimishwa etc.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tuliambiwa twendeni tukazaliane hatukuambiwa umri wa kugegedana ikisimama chomeka, dogo hajabakwa wazazi wake ndo Wana mawenge
 
Kwa mtu ambaye inaonekana umeelimika unashangaza ukicomnent hivi?

Na akipimwa akagundulika ni khanisi utasemaje?

Mahakama ndio chombo cha kutenda haki na kuthibitisha pasipo shaka yoyote kwamba mtuhumiwa ni guilty.
Itakuwa aliwahi bakwa huyo😁
 
Padri anajulikana anafanya hivyo vitendo hata mapdri wenzie wanajua. Awajibishwe aache kutuchafulia watoto na kanisa
Hao wanaojua si ndio wangeenda mahakamani kama mashahidi. Yani unacholalamika nini, kwamba mahakama zifutwe hapa nchini tuwe tunatumia hisia tu. Kwamba kesho naamka asubuhi nadai umeua kisha nakuua ama namna gani?

Mbona ni logic ndogo hapa inatumika. Kama una ushahidi na majina ya hao mapadre wanaojua, na watoto wengine waliofanyiwa vitendo hivyo si uisaidie mahakama. Kama ushahidi huna, si usubiri mahakama itumie taratibu zake, nyinyi mpipojua anafanya hivyo mlichukua hatua gani maana wazazi wa mtoto wameenda mahakamani.

Kesi haiendeshwi kwa hisia ndio maana mnafeli
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…