Hivi Padri mtuhumiwa wa ubakaji na yeye ana Wakili?

Hivi Padri mtuhumiwa wa ubakaji na yeye ana Wakili?

Wakili anayemtetea hana Watoto wala mke.​

Atakuja kuelewa hilo somo siku mtoto / mke wake atakutana na Padre.​

Nyie ndio ambao mkisikia kelele ya mwizi barabarani mnakimbilia mawe, mafuta na kiberiti....

Tulia sheria imtahiri mtuhumiwa kabla ya hukumu
 
Sawa. Ila mara nyingi haki hupindishwa huko mnakoita mahakamani.
Kama ni mkristo utakuwa unajua kabisaa hata shetani aliwahi kuwa malaika tena mkuu.

Siyo kila anayesimamia sheria ana heri ndo maana zipo mahakama za juu za kukata rufaa
 
Sikatai wao ni binadamu na wanahisia kama wanaume wengine akiona uvumilivu umemshindaa ni bora akakutwa na mwanamke wa umri wake basi sio watoto wadogo kuna wanaojiuza huko wengi tuu tena hao tunasema hawadaiwi na mtu ww chukua kafanye unalotaka akisepa amesepa.
 
Sawa mkuu ila na sisi wenye elimu finyu tulonayo tunaona kabisa kuna mahala mahakama haitendi haki.
Ni kweli hilo lipo ila kuna kukata rufaa Lakini tena wakati mwingine gharama za kuendesha kesi au kuzungushana mahakamani watu wengi wanaachana na kesi hiyo kwa kuzingatia kwamba kesi huweza kumfilisi mtu - inakutia umaskini.
 
Kweli natamani hata mahakama za kimila zirudi. Ukikutwa na hatia unacharazwa au kunyongwa mambo yanishia hapo. Mambo sijui ya kufananisha kesi ya mwaka fulani sijui iliendaje ni kupoteza muda
 
Yaani mnavyomtetea huyo padri nyie wakristo aisee, ngojea siku afanyiwe hivyo mtoto wako au we mwenyewe ukizima
Acha ujinga wewe.ukristo umeingiahe hapo?.Watu wanachokitaka ni sheria kufwata mkondo.kama kafanya ikathibitika hatua zichukuliwe.na kama ni tofauti hapate haki yake.haya mambo wala hayahusu dini kwasababu yanaweza kimkuta yoyote hata uko misikitini.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Uwakili ni kazi ya ajabu sana kwakweli, yaani unaanzaje kumtetea mtu katili kama huyo Padri, anaeweza kubaka watoto wadogo?

Mimi ni Mkatoliki kabisa ila naomba sana sheria isipindishwe kwa huyu mtu, apewe adhabu stahiki iwe fundisho kwa wote wanaonyanyasa watoto kihisia kwa sababu ya mwamvuli wa dini.

Leo mahakamani amejificha mpaka pua huiioni kama angekua hajatenda hivyo kwanini ajifiche? Wapo wengi aina yake huko makanisani wenye mapepo kama yake, wanaowaka tamaa kwa watoto ipo siku yao.

Yaani natamani hata mahakama wamtoe kwa wazazi na wananchi wa huko Moshi huyo mtu wamponde mawe. Kuna mtu amesoma naye Seminary anashangaa kwanini hata alifikia level ya upadri wakati tabia yake ya uchafu alianza zamani.

Wakili acha kutetea upumbavu wakati ushahidi upo, maana mtoto au watoto hawawezi kudanganya na tena kwa mtu waliyeaminishwa ni mtu wa Mungu mjue mpaka wamesema wamenyanyaswa haswa.
Mbona jambazi lililoua kikatili huwa na wakili? Si hivyo tu, likipatikana na hatia na kuhukumiwa kunyongwa, kesi hupelekwa mahakama ya rufaa na bado 'mtuhumiwa' anapewa wakili wa Serekali, labda yeye mwenyewe achague kuwa na wakili wa binafsi. Vitu anavyotuhumiwa kufanya Padri huyu ni viovu sana na havikubaliki kabisa si katika jamii ya kawaida tu bali hasa katika mazingira ya dini. Pamoja na hayo, bado ni haki yake kuwa na wakili.
 
Kweli natamani hata mahakama za kimila zirudi. Ukikutwa na hatia unacharazwa au kunyongwa mambo yanishia hapo. Mambo sijui ya kufananisha kesi ya mwaka fulani sijui iliendaje ni kupoteza muda
Lakini Kuna fursa ya kumaliza kesi nje ya mahakama.
 
Huyo padri inatakiwa anyongwe kabisa, na wengineo wote wachunguzwe inawezekana ndio tabia yao
Wewe unakataa mambo ya hisia alafu maoni yako ni kujikanganya tu, swala la hukumu halitegemei mihemko au hisia bali kwendana na sheria na katiba ya nchi.

Vitu vingine vilivyo kwenye ngazi ya mahakama ni kuiachia mahakama itende kazi kwa weledi otherwise kama lengo lako ni ku-obsruct justice.

Haya mambo ya kuhukumu mtu bila pande zote kusikilizwa ni ya watu ambao hawana uelewa wa mambo na ulimbukeni.

Kama sheria inasema akikutwa na hatia kwa ushahidi usio na mashaka basi wamuhukumu kwa mujibu wa sheria na siyo vinginevyo.
 
Watetezi wa ushoga tushawazoea nyie
 
Ndio maana lazima upelelezi ufanyike na ikathibitishwe pasipo shaka mbele ya mahakama. Unaweza ukawa na bifu na watu wakakutegenezea zengwe usijue pa kutokea au ukategwa na wewe ukajaa.
Exactly.

Kwa ushahidi wa Mbowe wa hadi mitandao ya simu ulitosha kuaminisha watu ni gaidi, lakini tuangalie kilichotokea mahakamani, ushahidi ulikuwa proven wrong na ni wa kutungwa.
 
Kuwa na wakili sawa, shida huyo wakili kuwa kilaza kuja na point zake za kukariri ... " Naomba umpunguzie hukumu kwani mteja wangu anategemewa, au mteja wangu ni mgonjwa"
Ikitokea hivyo naomba judge amuunganishe hukumu na huyo wakili.
 
Back
Top Bottom