OSEFUKANY ameniomba hapo juu nirudie kwa sauti.
Lakini mimi nakuelimisha kidogo. Kuwa na wakili ama kuwakilishwa kwenye shauri LOLOTE Mahakamani au mahekalu ya Haki ni takwa la Kikatiba.
Mtuhumiwa yeyote hawezi kutendewa kama mkosaji hadi pale Mahakama itakapomhukumu kuwa ametenda kosa hilo.
Hivyo pamoja na ushahidi kuwepo, inapaswa mahakama ithibitishe pasina shaka kuwa mtuhumiwa ametenda makosa hayo na anastahili adhabu kwa mujibu wa sheria.
Subira yako itakuwa inawatendea haki wahanga ama waathirika wa tukio ambapo Mahakama katika UHURU wake itatimiza wajibu wake muhimu wa kutoa haki. Ukiendekeza upayupayu unaoufanya hapa ni wazi unakuwa unaishinikiza Mahakama tofauti na utaratibu wa kisheria ulivyo.
Kumbuka hukumu ya kesi ya Zombe na wenzake....