Hivi Pesa za kurithi na mali zake zina laana gani??

Ulimbukeni unawasumbua hao, wapo wengi tu wanatoboa kwa mali za urithi.

Mali ya urithu kama hujadhulumu, ukishindwa kutoboa ni ulimbukeni wako.
Yuko limbukeni mwingine, aliachiwa milioni 80 benk, canter ya tani 3.5, nyumba ya kupangisha vyumba kama 20 hivi, nyumba moja ya kuishi, viwanja, mashamba, gari ya kutembelea.
Kwa ulimbukeni wake vyoote hivi vikaisha, anakaa nyumba ya kupanga na ana madeni lukuki, kisa tu kula bata.
 
Sipendi kufatilia maisha ya watu lakini bora tuzungumze ili kama kuna njia au daaa ya kuzuia hili basi tunufaike nalo

Hapa mtaani kwetu Mtoni Kijichi TMK Dar kuna mjomba Wangu alistafu Jeshini kitengo maalumu alikuwa na watoto wawili wa kike na kiume.

Huyu mzee alitumia ujana wake vizuri, alipanga uzazi vyema, kajiwekeza na kusomesha watoto.

Basi mzee wa watu akifariki baada ya siku zake kufika.

Gari lake Mama watoto akauza, alikuwa, huyu wa kiume alikuwa south Afrika. Akarudi na akahamasisha wenzake wachukuwe kiinua mgongo cha mzee.

Wakatapa 150M na wakapiga zikaisha.

Mama yao akawa anahonga dogodogo wa kumkamua.

Yule Binti Mkubwa akapata Bwana akamnunulia Bwana wake Noah ya kutembelea.

Maisha yakaendelea. Binti anapiga bata si mchezo. Viwanja na hotel kali zote anazijua. Mameni ndio usiseme na yeye ndiye anawahonga.

Wakauza Nyumba na kiwanja alichoacha mzee 400M.
Wakagawana Binti na Kaka yake na Mama akala sehemu yake.

Huyu wa kiume akanunua Fuso la Mizigo kwenda Mtawara na Lindi.

Akafilisika Fuso akauza.
Mama amebaki choka mbaya, yule dada yuko hoi anakula karanga kila siku.

Je hizi pesa zina shida gani?
Sasa hapo laana iko wapi mkuu, mbona Kila kitu kikowazi ya kwamba hao ndugu zako hawakuwa wamezoea pesa ila pia Kila mtu alikua na maisha yake akilini mwake ambayo alitamani kuyaishi ila hakuwa anayaishi kwasababu pesa hakuwa nazo sasa walipopata bahati ya kupata pesa Kila mtu akawa anaishi yale maisha ya ndoto yake.

Walijisahau wakadhani tayari wao ni matajiri na wakaupgrade maisha yao, kitu ambacho si kweli...

Wapeni watoto wenu exposure ya mambo haya maana bila hivyo madhara yake ndio kama hayo.
 
Nina ka experience kwa jamaa yangu tulikuwa tunasoma wote chuo, yey akikuw akitumiwa pesa anabet analiwa, basi ataishi maisha magumu huyo ya kugongea msosi kwa wana mpak tarehe ya mwisho wa mwez atumiwe tena,

Sasa kuna siku sijui akaotea ka laki 2 na sehem, usiku hio, asubuhi kaamka akapotea kwenda town , kuja kurudi kesho yake, hana kitu, hapo kalala na dem lodge, kahonga, na kaenda kula vizuri kwa meya.

Anaporudi asubh anakua hana kitu, hapo tens ataanza kuwakopa ili a beti na nyingne imuwezeshe kula.
Hahaaaa ....hizi ndio laana sasa😅
 
Hazina laana,sema mtu mweusi ndio kalaanika,mbona waarabu,wahindi,wazungu wanarithi na wanaendeleza mali walizozikuta mfano Mo Dewji,Abood
 
Marehemu alikuwa na ukatiri na ubishi hataki mali zake ziguswe mwisho wa siku hakuna aliyeabaki anayejua management ya assets na cash.

Ukijaaliwa kupata mali hakikisha watoto wako wanajua mali umepataje na unafanya nini kubaki nazo. Sio watoto unawazurulisha tuition, pre form one, pre form 5, chuo, field alafu kazini. Ukifa hamna wanachojua ni kuzitapanya alafu wafunzwe na ulimwengu maana mwqlimu wao umekataa kuwafundisha.
 
Sipendi kufatilia maisha ya watu lakini bora tuzungumze ili kama kuna njia au daaa ya kuzuia hili basi tunufaike nalo

Hapa mtaani kwetu Mtoni Kijichi TMK Dar kuna mjomba Wangu alistafu Jeshini kitengo maalumu alikuwa na watoto wawili wa kike na kiume.

Huyu mzee alitumia ujana wake vizuri, alipanga uzazi vyema, kajiwekeza na kusomesha watoto.

Basi mzee wa watu akifariki baada ya siku zake kufika.

Gari lake Mama watoto akauza, alikuwa, huyu wa kiume alikuwa south Afrika. Akarudi na akahamasisha wenzake wachukuwe kiinua mgongo cha mzee.

Wakatapa 150M na wakapiga zikaisha.

Mama yao akawa anahonga dogodogo wa kumkamua.

Yule Binti Mkubwa akapata Bwana akamnunulia Bwana wake Noah ya kutembelea.

Maisha yakaendelea. Binti anapiga bata si mchezo. Viwanja na hotel kali zote anazijua. Mameni ndio usiseme na yeye ndiye anawahonga.

Wakauza Nyumba na kiwanja alichoacha mzee 400M.
Wakagawana Binti na Kaka yake na Mama akala sehemu yake.

Huyu wa kiume akanunua Fuso la Mizigo kwenda Mtawara na Lindi.

Akafilisika Fuso akauza.
Mama amebaki choka mbaya, yule dada yuko hoi anakula karanga kila siku.

Je hizi pesa zina shida gani?
Mali za urithi zikiwa zimewekezwa vema hazina shida kabisa.. Tatizo liko kwa wazazi.. Wanawekeza kwwenye mali na elimu ya watoto ya darasani bila kuwekeza kwenye Ufahamu na maarifa ya maisha
 
Mzee wangu Mshana hivi hivi wewe kama mzazi utawambia watoto wako kwamba umekopa ili ujenge, utawambia watoto wako umekopa Ila january waende shule. Utawambia watoto wako Hati hiko benki umeikopea??

Nilikuwa nasubiri comment yako.

Kukopa ili ulipe ada ni jau nyingine

Inaonekana umefosi sana hiyo shule sio level yako
 
Waswahili mnauwa hata baba zenu kisa mpate cha kwake halafu zote zinaisha
Ujinga na matatizo ya akili
Mirathi kama mlifundishwa maana ya maisha sio shida ila shida inakuja kama hamjui thamani ya hela

Sio tu mirathi hata ndoa ndio maana nyingi zinaharibika
Wanawake wengi hawajitumi wanategemea kulishwa tu na kusubiri ufe wazimalize
Ila wapo wasiojituma lakini wana misimamo thabit kwenye ndoa na kulinda mali za waume zao hata kuweka akiba kwa wanachopewa
 
Ukijaaliwa kupata mali hakikisha watoto wako wanajua mali umepataje na unafanya nini kubaki nazo
sio kila kitu kinafundishika ndugu.

mara nyingi mafanikio huja kwa jasho na damu na passion ya ndani kabisa ya mtu binafsi.

kifupi ni sacrifice yani roho ya kujikana.

hivi vitu vyooite havifundishiki.
 
Jasho na damu =kutoa kafara
 
Hapa mtaani kwetu Mtoni Kijichi TMK Dar kuna mjomba Wangu alistafu Jeshini kitengo maalumu alikuwa na watoto wawili wa kike na kiume.
Hao madogo walirithi mali ambazo chanzo chake ni ajira ya mzee wao,.....hii ni tofauti na wahindi,waha jamaa hawarithi tu mali bali wanarithi na kile chanzo cha hizo mali........so matumizi yao yanakuwa covered bila kugusa mali walizorithi....kosa jingine ambalo wazee wetu wanalifanya ni watoto kupata urithi baada ya mzee wao kufa,hii technically haijakaa sawa,urithi unatakiwa utolewe ukiwa hai ili uwe na muda wa kuwasimamia,kuwashauri na kuwaonya,mtoto ambaye ni pasua kichwa unamfuta kabisa kwenye list ya warithi,tukifata utaratibu ambao M-ngu ameuweka kwenye masuala ya urithi basi hizi changamoto za mali za urithi zitafika mwisho.
 
Waswahili mnauwa hata baba zenu kisa mpate cha kwake halafu zote zinaisha
Ujinga na matatizo ya akili
Mirathi kama mlifundishwa maana ya maisha sio shida ila shida inakuja kama hamjui thamani ya hela

Sio tu mirathi hata ndoa ndio maana nyingi zinaharibika
Wanawake wengi hawajitumi wanategemea kulishwa tu na kusubiri ufe wazimalize
Ila wapo wasiojituma lakini wana misimamo thabit kwenye ndoa na kulinda mali za waume zao hata kuweka akiba kwa wanachopewa
Tumia pesa yako kulinda afya yako Dini yako na raha zako enjoy your sweet, hamna mwanamke wakikulindia mali zako ukifa bila yeye kuingiza mwanaume mgine impossible..........

Kuna jama moja hapa mjini hana kazi ila kwasababu ni smart alf mcha mungu yeye kazi yake ni kusitri wajanne wenye uwezo wa mali kwasasa ana wake watatu wajanne wako wilaya mbili tofauti, ila mimi nilikuja kumjua baada yakuuliza rafiki yangu anae uza bucha pale jirani, mara kadhaa na muona anabadili magari nyama wana nunua kilo 5, 5, mara tatu ni kamuuliza mshikaji huyu ana kazi gani kaniambia hana kazi ila ameoa wajana wa tatu wenye mali kwahiyo hana mda wakufanya kazi zaidi ya kutumia mali za wanaume wenzake walio dedi kuwasimamia wajjane na kuwastiri katika maisha yao.
 
Hao madogo walirithi mali ambazo chanzo chake ni ajira ya mzee wao,.....hii ni tofauti na wahindi,waha jamaa hawarithi tu mali bali wanarithi na kile chanzo cha hizo mali........so matumizi yao yanakuwa covered bila kugusa mali walizorithi....kosa jingine ambalo wazee wetu wanalifanya ni watoto kupata urithi baada ya mzee wao kufa,hii technically haijakaa sawa,urithi unatakiwa utolewe ukiwa hai ili uwe na muda wa kuwasimamia,kuwashauri na kuwaonya,mtoto ambaye ni pasua kichwa unamfuta kabisa kwenye list ya warithi,tukifata utaratibu ambao M-ngu ameuweka kwenye masuala ya urithi basi hizi changamoto za mali za urithi zitafika mwisho.
Mzee baba umemaliza Kila kitu
 
Hakun laana ,
Maajiri wengi huwa na mifumo mizuri ya kurisishasha.
Sis watu wa kundi la kawaida mara nyingi wanaobaki wanakuchukilia urithi kama pesa ya bonus.

Ngoja nisubr nami nione nitatokaje😊🎩
 
Back
Top Bottom