Hivi Rais Samia angeamua kuanzisha uchunguzi wa tukio la Lissu kupigwa risasi, sukuma gang wangekuwa na hali gani? Shukurani kamsitiri

Uchunguzi uanze tu
 

maKu
 

Maswali ya jamaa ni mazito ila unayajibu ki wepesi sana, mimi pia naungana nae kuamini Magufuli hakua mjinga kiasi hiko kuamuru Lissu auliwe tena kipindi ambacho umaarufu wa the former kwa wananchi ulikua juu sana hasa baada ya ku deal na ishu ya makinikia katika namna ambayo wananchi wengi waliona ni sahihi na ya kijasiri sana.

Na sasa tunaelekea miezi 18 bila mzee na wote tunajua huyu mama hawezi kusita kufanya kitu chochote kitakachoshusha heshima ya JPM kwa wananchi, mbona hajaruhusu ufanyike uchunguzi huru kama alivyokurupuka kuchunguza ile miamala ya BOT?

Mimi katika vitu naogopa ni kuhukumu kitu nisichokua na uhakika nacho, kuna siku mambo yatajulikana, tutatafuta hizi comments tuzifute na kuzidelete kabisa!
 

Hoja zako zinafikirisha sana na hazitakiwi kupuuzwa hata kidogo.

.Nimelazimika kumlaumu au kumnyooshea kidole Magufuli kwa sababu zifuatazo.

1. Kuondolewa kwa WALINZI wa serikali eneo aliloshambuliwa Tundu Lissu.

2. Serikali kukataa kutoa msaada na kumhudumia Lissu baada ya kushambuliwa.

3. Serikali kutokufanya uchunguzi wa tukio hilo, na kutoa visingizio visivyo na mantiki.

4. Serikali kukataa kuita wachunguzi toka nje ambao wanaaminika na pande zote.

5. Serikali kumfukuza Lissu bungeni kwa madai kuwa haujulikani alipo.

6. Viongozi wa serikali na Ccm kutoa kauli za kumkashifu Lissu hata alipokuwa ktk mazingira ya ugonjwa hospitali.

Ikiwa ITATHIBITIKA pasipo na shaka kwamba waliojaribu kumuua Lissu sio watu wa serikali nitakuwa tayari kuomba RADHI ktk jukwaa hili.
 
Hakuna haja ya uchunguzi. Kila kitu kinajulikana
 
Mimi sijui hao waliyokuwa wanauliwa ni akina nani na walikuwa wanauliwa kwa sababu zipi na ndio maana nikakuuliza wewe mwenye kuwajua kwamba hata yule mume wa yule mama alionekana kwenye tv naye alikuwa mkosoaji wa Magufuli ndio maana aliuliwa?
Binafsi siwajui hao waliyokuwa wanauliwa wala sababu za kuuliwa kwao hivyo siwezi kuwa na jibu la swali uliloniuliza, matukio ya uhalifu yapo na watu wanauwana kwa sababu mbalimbali kwa aina tofautofauti.
 
Kwamba serikali kukataa kumuhudumia Lissu baada ya kushambuliwa ni moja ya sababu ya kwamba serikali ndio iliyohusika na shambulizi la Lissu?
 
Kwamba serikali kukataa kumuhudumia Lissu baada ya kushambuliwa ni moja ya sababu ya kwamba serikali ndio iliyohusika na shambulizi la Lissu?

..inaonyesha nia mbaya ya serikali / Magufuli dhidi ya Tundu Lissu.

..baada ya Lissu kunusurika pale Dodoma wakaona bora afe kwa kukosa matibabu sahihi ya kitaalam.

..Walitegemea Lissu atashindwa kugharamia matibabu. Matokeo yake wasamaria wema wakaingilia kati.
 
Dhana ni nyingi sana.
 
well said
Lissu asiangalie mbali. Uchunguzi wa tukio unaanzia na motive. Magu alikuwa hana motive ya kumpiga risasi Tundu Lissu. MAGU alikuwa ni Mkuu wa majestic na ni Rais, asingepoteza risasi 16 kama munavyodai Kwa Lissu. `Lissu asiangalie mbali wakati chama chake kina Gaidi anayeitwa Mbowe. Huyu ndiye mwenye sababu ya kuweza kumpiga risasi wakigombania uongozi wa chama chawo. Magu alikuwa busy kuisafisha Tanzania iliyokuwa ikinuka rushwa na wizi na kuokowa mali za Watanzani. Mmoja wa wezi akiwa GAIDI MBOWE. Mwacheni Magu alale salama na Tundu Lissu apambane na maisha yake ya ukimbizi.
 
Dhana ni nyingi sana.
Musisahau ni madakitari wa kitanzania ndiyo walio okowa maisha ya Lissu. Hakuna mtu angefaidika Lissu kufa zaidi ya Mbowe ambaye walipingana kwenye chama chawo Kwa matumizi mabaya ya fedha. Kila kukicha Magufuli mtu ambaye hawezi kuwajibu. Pambaneni na maisha yenu mpaka na nyinyi siku yenu ya kufa ikifika. Kila binadamu ni mpita njia hapa duniani. Ndiyo Hayati Magufuli hatunaye tena, but he was the best president for Tanzania and we miss him a lot.
 
Yote Tisa kumi nenda urudi.
Kila kitu ilipangwa!!
Hebu muulizeni Cyprian Musiba huenda Naye mojawapo wanaolijua! Alikuwa anajiamini sana sana! Je Leo hii yuko wapi Musiba wa Musiba domokayah!! Hovyo!!
 

Leo mkuu inaenda miezi 19 tokea huyu mzee ameondoka, aliekua spika wakati huo kwa sasa hayupo tena, Kipili.mba hayupo, Si. rro hayupo, aliekua RPC Dom hayupo, Ma.konda hayupo!! Huo uchunguzi kwanini haufanyiki? Nani analindwa kwa sasa?

Mimi bado naamini mzee asingeweza kamwe ku order kifanyike kitu cha kipumbavu namna hiyo tena kwa njia ile.

Ila pia sikulaumu, walau wewe mtu akifuatilia nyuzi zako unaonekana hukupenda wala hukukubali chochote alichokua anafanya huyu mzee way before hata hajawa rais, lakini naendelea kukuomba usimtupie mawe walau kwa hili kama hauna uhakika.
 

..yeye mwenyewe ndio alitengeneza mazingira ya kutupiwa lawama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…