Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Nchi za kiafrica na tawala zake ,hata majambazi na wachawi kuna muda wanatuonea huruma
Ni kweli aisee. Matatizo ni mengi sana. Sisi mtaani kwetu tuliliwa na shida ya barabara, happ panaposumbua kuna wajomba kama watatu hivi waliwahi kusimama na mashine mida ya saa mbili ya saa tatu usiku mimi nilipishana nao kama dkk 10. Waliteka magari ya watu wanatoka kazini, na kupelekea moto balaa. Baada ya tukio damu ilikuwa imetapakaa hapo chini japo hakuua zaidi ya kutoa meno na kuvunja viungo vya wabishi wachache waliokataa kutii amri..

Hilo tukio lilisamababishaga hofu kwa kila mkazi. Magu ndio alikuwa anakalia usukani bado hajachanganyia vizuri, sasa hivi ushwari wa kutosha ila vibqka tu wachovu wanashambulia kwa kushtukiza ukikaa kizembe.
 
Kule niliwahi kupanda bus nyuma kuna Polisi wanaescort wako na mashine zao. Nikashngaa nini tena hii? Jamaa wakasema bila hivyo kutokq tunzewe hqdi nyakanazi tu hutoboi. Ila siku hizi tunakatiza tu bila mabunduki.
 

Walikuja na difenda?
ndio hao hao, siku hizi wanaitwa watu wasiojulikana kazi yao kuteka au kuua

nakumbuka tukio moja hv, pale ubungo waliiba benk wakatokomea tena hapohapo ubungo kukawa na cruza inasafirisha pesa zikapigwa sana risasi, trafik mmoja akawa shujaa kupambana nao, ktk majeruhi wengine wakakutwa lugalo wakitibiwa
 
Kwa kawaida majambazi huwa ni watu wenye ufanisi mdogo katika kazi mbalimbali ambazo ni halali lakini siku hizi wanapata pesa kirahisi kwa mfano baadhi ya watu wanapewa pesa kisa wanawasifia wenye pesa (wamekuwa machawa). Angalia mtu kama Mwijaku, Baba levo bila kumsahau Maulidi Kitenge.
Fauka ya hayo, kuna watu wamekuwa tena wanaume wazima wamekuwa mashuhuri kwa kuuza nyuma (mtu mmoja humu ndani hupenda kuita kinye###), nasikia kwa Tanzania yetu Mr pdidy ameshatembea na watu kadhaa na kuwawezesha kiuchumi, labda Mr pdidy asingekuwepo hawa jamaa wangukuwa majambazi.
Hivyo basi tunapokemea uchawa na matendo ya watu kugawa nyuma kama njugu tujitafakari ili tujue iwapo yanahasara tu au pia yanafaida.

ONA JEMA KWENYE KWENYE BAYA!!
 
Unamaanisha uchawa umechangia kupunguza ujambaka 😆😆😆
 
Majambazi walikua wanashikwa na silaha ila mahakama zikawa zinawaachia kwa errors ndogo ndogo za ushahidi, ikafika hatua ukikamatwa na silaha unataja wenzako mnapelekwa nje ya mji alafu taarifa zinarudi wamekufa katika majibizano ya risasi
 
Jaribu kuwa jambazi na hautoonekana tena kwenye uso wa Dunia wala habari zako
 
Jeshi la polisi halichek na nyani
Ukileta ujambazi tu unapotezwa tu biashara imeisha watakuwa majambazi wameambiana vikao vyao kaa mbali na ujambazi Tanzania unataka familia yako ione maiti yako na ikuzike vinginevyo waweza potea hewani kama ndege ya malyasia iliyopotea hewani haijawahi patikana hadi leo

Hakuna sehemu hatari duniani kwa sasa kwa jambazi kama kufanya ujambazi Tanzania

Kitakachomkuta jambazi hata kama kanusurika kufa lakini cha moto atakiona hata kama kufa hakufa lakini cha mtema kuni atakiona na mwenyewe atajipeleka ku trend media baada ya kuonyeshwa cha mtema kuni na ataapa kimoyomoyo kuwa ujambazi basi

Tanzania bila ujambazi inawezekana kaa mbali na ujambazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…