Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Mwaka flani yaliteka basi na kuwapora Kila kitu Hadi nguo Kisha yakawaambia waanze kuimba wimbo wa "Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe."
Huku wakiwa uchi mhanga mmoja wa tukio Hilo alikuwa wa kijijini kwetu. Waliimba badae yakatokomea na nguo maporini gari iliyokuja na kuwakuta wako uchi ilibidi itoe taarifa police wakaja na mashuka Yale ya minadani mwaka2002 kama sikosei
 
We jamaa umenikumbusha mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani walikuja majamaa wale mbavu nene imepanda hewani watatu na kila mmoja na sub machine gun yake full kujiamini , walikuja kwa boss wa boti za uvuvi yule mpemba alikua anakaa na pesa ndani kama milioni 150 hivi ,basi wawili wakaingia ndani , alafu moja likabaki nje

Mpemba akaminywa na mkewe kilio kikamtoka majirani wa kwanza kufika kutoa msaada wakakuta jamaa halina hata time tena limewasha sigara chuma mkononi ,
Basi wale wa kwanza wakaanza kurudi mbio kwa mayowe makubwa sanaaaa " jamani ni majambazi sio wezi kimbieeeni basi unajua kilichotokea? WA MWISHO ALIKUA WA KWANZA🤣🤣🤣🤣
 
NambA 1, 2 na 5 ni hao hao, wameelewana kufanya yao kwa jinsi tofauti!
 
Bonge moja la Documentary niliifuatiliaga kitambo kidogo ilikua mwaka 2021 UKITAKA UIELEWE USIRUKE RUKE ANZA NAYO MWANZO NI KAMA MOVIE VILE
 
Huu mwaka ulioweka ni sahihi?


Maana hii tabia inasemwa ni ya Rais aliyetangulia mbele ya Haki (2015-2020).
 
Ujambazi wa silaha hakuna nyakati hizi either umepungua ila misala imehamia mitandaoni kwa sasa. Ndo watu wanakovamiwa.
 
Yamebaki makaburi na picha za kumbukumbuku.. Hiyo awamu iliyopita haikuwa na msalie mtume.. Walifuatwa waliko wakamalizwa huko huko kimya kimya
Hawa waliobaki kwa haya tunayopitia hata sisi wanatuonea huruma
Sure ,awamu ya jiwe ilifanikiwa sana kulala nao "MBERE" ,hata Panya Road nao walitangulizwa mawinguni...Ukicheka na Nyani utavuna mabua ,walikuwa wakikamata jambazi wanachukua chain yao yote wanaenda kula VYUMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…