Hivi Tanzania nani akifa atapata heshima ya upendo kama ninayoiona kwa Raila Odinga

Hivi Tanzania nani akifa atapata heshima ya upendo kama ninayoiona kwa Raila Odinga

Inategemea na wakati; Kwa aliyofanya Raila kabla, Ukiondoa issue ya Usaliti wa Gen Z emefanya makubwa sana ingawa hata hivyo kama nilivyosema inategemea timing hata Lowassa tuliyeambiwa ni Fisadi na mlaji alivyozikwa tuliambiwa ni shujaa ingawa sasa hivi katika mafaili yanayovutwa tunaambiwa ni muasisi wa mtandao....

Moral of the Story Tenda Wema (what you thing is right) Uende zako Usingoje kurudishiwa... Kumbuka pia wanasiasa wengine huu ndio wakati wao wa kuuza Sura....
 
Kenya ukabila umetawala, huyo wanaemlilia ni kutoka katika kabila lao na ni kiongozi wao, hivyo hao wanao omboleza ni watu kutoka kabila la Raila pekee. hapa tanzania kiongozi akifa anaombolezwa na watu wote bila kujali kabila,dini au qangi, hakuna jipya katika msiba huo bali ukabila umetawala.
 
Naangalia kinachoendelea kwenye maombolezo ya Raila. Yananijia maswali madogo ..je hapa Tanganyika/Tanzania, nani aliye madarakani/ serikalini akifa ataliliwa na watanzania?
Simuoni!
Kuna mstaafu mmoja hivi Wa hapa Tanzania ajaribishe tu kufa aone watu watakavyo fanya party za wazi wazi na kushangilia .....

Kifupi Kwa Sasa hivi Kwa hapa Tanzania hakuna msiba utakaogusa mioyo yetu Kwa huzuni labda Kwa furaha
 
Back
Top Bottom