Raila ni lazima aliliwe na kupewa heshima ya pekee na Wakenya wote.
Alikuwa kiongozi wa upinzani, na mbunge wa wananchi kwa muda mrefu, akitetea haki za Wakenya, kama anavyofanya Lisu.
Raila aliwahi kuwa waziri mkuu wa Kenya. Chini ya Serikali yake, Hakuna mkosoaji aliyetekwa na kuuawa, au kutekwa na kupotezwa, wala hakuwahi kuwabambikia kesi wapinzani wake, kama wanavyofanya watawala wa Tanzania.
Anamzidi Lisu kwa sababu tu Lisu hajawahi kuwa kiongozi wa Serikalo. Lakini angalao anafanana na Lisu katika kupigania haki za wananchi bila woga. Anatofautiana kabisa na watawala wa Tanzania kwa sababu watawala wa Tanzania ni wadhulumaji wa haki za wananchi.
Mungu wa huruma umjalie pumziko jema mtumishi wako Raila, kwani aliuishi upendo wako kwa kupigania haki za wasio na sauti. Tunaomba ukayafutie mapungufu yake kwa yale mema aliyoyatenda, ya kujitoa sadaka kwaajili ya gaki za Wakenya. Tunaomba Jina lake Raila likawe mbegu ya kuitafuta haki Afrika Mashariki yote, na Afrika nzima iliojaa udikteta na dhuluma dhidi ya binadamu. Mungu wetu, tunaomba uyapokee maombi yetu. Tunaomba siku moja Afrika nzima ichomoke kutoka kwenye tawala dhalimu zinazoteka na kuua binadamu kwa vile tu binadamu hao wamehoji au wamewakosoa. Tunaomba laana ya damu za hao waliouawa zikawe juu ya watawala hao na vizazi vyao.