Hivi tatizo la kutosikia vizuri ni tatizo kubwa zaidi duniani?

Kuweza kuishinda hiyo hali inabidi kwanza uifunze nafsi yako kupokea watu kama walivyo. Usiwe mtu wa kuonesha kuchukizwa kwa namna unavyotendewa, maana unapoonesha negative reaction wao ndiyo huwa unawaburudisha zaidi. Kuwa mtu wa kutulia, usikunje sura, always be neutral pale unapotendewa vibaya, mwisho utamfanya akutendaye aanze kujiona kuwa alifanyalo anakosea.

Hii situation nilikutana nayo kwa mara ya kwanza nikiwa advanced level. Licha ya namna nikivyotendewa na baadhi ya wanafunzi ila sikuwahi kukorofishana na yeyote maana sikuwa naonesha kuwazingatia juu ya matendo yao.
 
Yes tatizo ni kubwa sana,nashangaa sioni serikali ikilipa kipaumbele walau kutoa misaada.Niliwahi kuhudhuria huduma moja inayotolewa na wafadhili kutoka Marekani STAR KEY ya vifaa vya kuongeza usikivu-hearing aids,watu walikuwepo pale ni zaidi ya elf 3,na walianza kufika pale kuanzia saa 11 alfajiri,mtu mmoja aliniambia Mwanza watu walijaza uwanja wa mpira,sasa kwa hali hii inaonyesha kuwa hali ni mbaya sana na tatizo ni kubwa...
 
Nilikuwa nakutafuta Mwarain wa Mwanza si ndiyo?
 
Najitahidi
 
Hakuna.labda madawa ya mizizi unywe unaambiwa sijui yanaenda kuamsha mishipa ya fahamu inayodili na usikivu
Mimi sijawahi
Dawa za asili zipo usiwe mbishi Kwa kila kitu Mimi mzee wangu alikuwa hasikii .

Ila kuna Dawa alitumia akapona .

Nipo Bukoba Ila nikifika DSM Kwa mzee nitamuuliza hiyo Dawa.

Dawa zipo na zinatibu
 
Nimekaa na kuishi na mtu asiesikia vizuri nakuelewa sana jinsi gani unajisikia
 
Imenisaidia sana hii,mtu akinisemesha na sikumsikia vizuri huwa namwambia ongeza sauti masikio yangu hayasikii vizuri,akimumunya maneno namwabia tena ongeza sauti mimi nina shida ya masikio,huwa ninaongea kwa ujasiri,kwahiyo hainiumizi sana ingawa mwanzoni nilikuwa naona aibu na kujitenga na watu ili nisijulikane hali yangu...
 
Sema tatizo lipo Kwa wengi sana
Sio kubwa sana.
Ni kweli.leo ukisema serikali iwape nauli wote Kila Kona wafike pale uwanja wa mkapa patafurika
 
Wengine vichwa vibovu
Matokeo ukimwambia aongeze sauti anakufokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…