Hivi tatizo la kutosikia vizuri ni tatizo kubwa zaidi duniani?

Pole! Umeongelea wasioona kuvaa miwani, vipi kwa upande wenu, hata vya kusaidia kusikia haviwezekani? Kila muamba Ngoma, huvutia kwake, unapokuwa na tatizo, unaweza kudhani hakuna mhanga kama wewe, ila kila anahisia hiyo kwa changamoto aliyonayo. Kama mna umoja wenu, angalieni ni eneo gani jamii haiwaelewi na vipi mnaweza kutoa uelewa kwako, pengine itamaliza kabisa unyanyapaa. Binadamu ni wabinafsi, yeye akiwa vizuri, haoni tatizo la mwenzie.
 
Nina situation kama hiyo na nimeshapitia matibabu nje, kama utaridhia twaweza kuwasiliana. Karibu PM iko wazi.
 
Hili ni kweli kabisa. Na ni hatua ya muhimu sana kwa mwenye tatizo kujua jinsi ya kuishi katika mazingira hata yale ambayo watu hawamfaham kabisa.
Nachokiona mwenye tatizo anapoliona tatizo lake la kutosikia vizuri kuwa kubwa kuliko lilivyo, inaishia kumkosesha mpaka ile confidence ya kimawasiliano na watu wapya pia inafanya akose ule ushirikiano wa kimawasiliano.
Sasa anayekuwa anawasiliana naye, by default anakuwa ameAssume kuwa anaongea/anawasiliana na mtu asiyekuwa na shida yoyote ila kumbe ni mwenye tatizo la kutosikia vizuri.
 
Mimi Pia ni Muhanga, Changamoto ni Nyingii Sana Ninazokutana Nazo , Nakumbuka Nilikosa Kazi Ya Ulinzi Kampuni Moja kubwa Kisa Usikivu wakati Written interview nilikuwa Nimefanya Vizuri tuu ila Wale Maboss Wakanitema, Daah Niliumia sana. Sasa Nimeamua kurudi shule Kusoma., Nipo chuo na bado Changamoto Ni Nyingiii Sana Sema Kinachonisaidiaga Mimi ni Mkimya Sana ( Introvert Pro Max ). Kwasasa Ninachomuomba MUNGU Nipate Ajira Kwenye huu Mtaala Mpya wa Elimu, Naamini MUNGU Atatenda.
 
Hiko hivyo ndio walimwengu ukishawaelewa awakubabaishi kitu🤸
 
Same to me kabisa inafika mahala mpaka unahisi ilo tatizo ni kubwa kuliko yote,

Yote uliyo andika ni ipogo hivyo lakini Mimi awanipagi shida yaani ni nunda haswa halafu najikubali kinoma anibabaishi mtu👊🤸
 
Mkuu wewe ni Mimi kabisa pale hear well clinic. Yule daktari aliniambia Mimi pia hivi hivi kwamba tunakupa Ila guarantee ya kupono ni nusu kwa nusu .
 
Nilishawahi kumzingua mtu fulani kwa kudhani ananidharau kumbe jamaa hasikii vizuri, kile kitu kilinitafuna sana hadi leo huwa najiona nina hatia tangu siku ile nikikutana na hali kama ile nikimsemesha mtu na nikamuona hanizingatii huwa nakua mpole na kurudia kumuuliza kistaarabu
 
kimsingi ni kwamba hali ya ulemavu kwa jamii nyingi za watanzania ni changamoto. Wewe unazungumzia suala la usikivu hafifu, kuna watu ni viziwi wasioona ulishawahi kujiuliza hawa ndugu kwenye jamii wanaishi vipi? cha msingi ni kukubaliana na hali uliyonayo nakuchukulia zile changamoto kama tu ni vikwazo vidogo kwenye mafanikio yako. Jamii yetu bado ina unyanyapaa mkubwa kwa watu wenye ulemavu.
 
Mimi Pia ni Muhanga, Changamoto ni Nyingii Sana Ninazokutana Nazo , Nakumbuka Nilikosa Kazi Ya Ulinzi Kampuni Moja kubwa Kisa Usikivu wakati Written interview nilikuwa Nimefanya
Akunyimae Kunde..., Sasa huoni kwamba huenda vibaka wangekunyemelea wewe bila kujua na kukupiga roba au mali kupotea kwa uzembe wa wengine ukazingiziwa kwamba haukusikia ?

Uzuri kuna mambo mengi ya kufanya mengine ambayo hayahitaji kabisa usikivu makini...
 
Dawa za asili zipo usiwe mbishi Kwa kila kitu Mimi mzee wangu alikuwa hasikii .

Ila kuna Dawa alitumia akapona .

Nipo Bukoba Ila nikifika DSM Kwa mzee nitamuuliza hiyo Dawa.

Dawa zipo na zinatibu
Mpaka ufike Dar Mzee? Kuwa serious kidogo. Mzee hana simu?
 
Inaitwaje hiyo hospital?
 
Hyo haikuwa na hearing loss kutoka upande wa neva ila alikuwa na uchafu kwenye masikio.

Wenye hearing loss kutokana na neva hawa wanapata matatizo mengine ambatano ; miguu kufa ganzi ,matatizo ya macho ,mwili mzima kufa ngani.

Halafu kupigwa tochi ni local sana tena hatua ya mwanzoni kabisa ,hata hospital za kata wanaweza kufanya hivyo then wanakupiga bomba.

Kuna kipimo cha kuangalia aina ya tatizo ,aidha ni symmetrical au asymmetrical hearing loss...Wanapima kwa kuangalia level za kusikia ,sana sana wanaangalia : je ,masikio yote yana uwezo sawa wa kusikia au moja lina tatizo tofauti na lingine...Ukifika hatua hii tambua ni neva na kinachofuata labda upandikizaji wa vifaa, operation (gharama sana)au kutumia vifaa vya kawaida typically amplifier .


Ukiona kapona kwa urahisi hivyo basi ni uchafu kwenye masikio ,ndugu yangu tumezunguka kote mpaka amekosa raha kwa sasa ila darasani ni kichwa sana ,wajinga wanaamini eti karogwa ila complications nyingine kma miguu anazo hawezi hata kukimbia .
 
Dawa za asili zipo usiwe mbishi Kwa kila kitu Mimi mzee wangu alikuwa hasikii .

Ila kuna Dawa alitumia akapona .

Nipo Bukoba Ila nikifika DSM Kwa mzee nitamuuliza hiyo Dawa.

Dawa zipo na zinatibu
Boss,dar unaenda lini?
Na jee huwezi kumwomba mzee akapiga picha hizo dawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…