Hivi TBC kazi yake ni kumwonyesha Magufuli peke yake?

Hili li channel la TV linaboa vibaya mno!!
 
Mwambieni jamaa yenu, aache matusiiii atamulikwa tuuuu . hata vyombo vingine vitamtupilia mbali asipojirekebishaaa.
 
Sasa haya ni matumizi mabaya ya kodi. Kama vipi wananchi tukatae huu ubaguzi.
Nyie si mlisusa maana ndo tabia yenu.
Acha wenzenu wale.

Nyongeza: Utakuwa ni ubwege wa kiwango cha kati, kama uwe madarakani halafu ushindwe kutumia zana zako zote kupambana na mshindani wako ambae anajivunia mdomo tu!!
 
kama yeye ni rais anafanya kampeni za nini?
Ametangaza kununua Ndege kujenga bwawa la umeme reli flyover lakini kaona watanzania wanajua miradi yote mikubwa imejaa 10% ufisadi mwingi hawataki kuichagua CCM ndipo kaamua kuzunguka kutengeneza mazingira ya kuwalazimisha watanzania waipende CCM kwa nguvu
 
Mkuu umejuaje kama TBC 1 inamuonesha Magufuli tu? Ninyi si mliishaacha long time kuiangalia?
TBCCCM hupendelea CCM kwa 89% hizo asilimia kidogo ndizo huonyesha vyama vingine
 
Lakini kodi za wapinzani kuendesha na kuwalipa mishahara hao wafanyakazi wa TBC wanazitaka siyo??
 
Nyie si mlisusa maana ndo tabia yenu.
Acha wenzenu wale.

Nyongeza: Utakuwa ni ubwege wa kiwango cha kati, kama uwe madarakani halafu ushindwe kutumia zana zako zote kupambana na mshindani wako ambae anajivunia mdomo tu!!
Kutumia zana zako ambazo hulipwa mishahara kwa kodi za watanzania wote ni ushetani ni matumizi haramu ya pesa za umma
 
Kabla ya kuja na kusema inaendeshwa kwa kodi zetu je umeangalia invoices zote za TBC ukakuta hakuna inayowahusu CCM?
Si ndiyo nasema basi wapinzani wasiwe wanalipa kodi maana tumesikia wasipochagua chama fulani watateseka miaka mingine mitano na taa za barabarani watakuwa wanaiona kwenye movie.
 
Mwambieni jamaa yenu, aache matusiiii atamulikwa tuuuu . hata vyombo vingine vitamtupilia mbali asipojirekebishaaa.
Matusi yapi? Hakuna matusi kwenye upinzani Yaani ukweli mnageuza uonekane ni matusi? kama ni matusi yapo CCM
 
Aisee hiki chombo kuna shida kubwa! Na kwa hakika siku tutakapopata UHURU wa kweli, mimi nafikiri taasis ya kwanza kufanyiwa ukaguzi wa hesabu kwa huduma zote ilizozitoa kwa CCM ni hii TBC! Watuonyeshe pesa zote zilizokwishalipwa na CCM kwa kutumia chombo hiki kama mali binafsi ya chama ilihali wanayo Channel Ten! Na kama hakuna malipo itabidi tuanzie hapo!
 
si mliwafukuza
 
si mliwafukuza
Kwani mwanao akikufanyia vitendo haramu vya kishetani utaacha kumfukuza? TBCCCM walifukuzwa baada ya kuwa wanakatakata Matangazo kienyeji kishamba shamba, walihujumu mkutano wa chadema ulitegemea nini hapo? au ulitaka wafanye hujuma kisha wakumbatiwe?
 
sasa wakija tena una uhakika gani kama hawatahujumu?
 
Matusi yapi? Hakuna matusi kwenye upinzani Yaani ukweli mnageuza uonekane ni matusi? kama ni matusi yapo CCM
Kumbe KUWATUKANA WATUMISHI WA UMA NI TAKATAKA ZA JALALANI ,kwenu hii ilani ya chama chenuuu?
Hovyo kabisaaaa.
 
hao wengine hakuna kitu, wanatafuta kura za huruma hata ilani zao hazieleweki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…