Bondpost
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 7,019
- 10,455
Aliyenunua ndege cash ni Nani??? Tusimtwike mama wa watu lawama asizostahili. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe.Hivi hili taifa halina wachumi au watalaamu wa mipango?
Hivi waliopo madarakani hawana huruma na wananchi?
Taifa bado maskini kabisa ambalo huduma za kijamii na kiuchumi bado zipo duni kabisa linakwenda kukopa Tril 1.3 na kujenga vyoo vya shule na madarasa huku likitumia Cash kununua ndege za matrilion ya shilingi!
Taifa letu limemkosea nini Mungu?
Kama ni ishu ya kufanya biashara ya ndege itakayolipa kwanini tusikope hizo ndege halafu tukatumia cash tuliyonayo kujenga vyoo na madarasa?
Yule mshamba wa ndege ndio alikuwa ananunua tu bila kuwa hata na plan yeyote, shirika limejikuta Lina mandege hayana vibali vya kuruka kwenda nchi kadhaa.
Zinazurura tu Leo unakuta moja kaichukua waziri Mkuu, nyingine Makamu wa Rais, nyingine bi mkubwa anazurura nayo kupiga shanting ya Dar to Dodoma, hizo nyingine zinazurura tu hakuna kitu.
Mwaka juzi walireport loss ya revenue na mwaka jana loss tupu imebidi wasamehewe madeni wanayodaiwa na serikali ili kucover hizo loss zao Ila hakuna kitu.
Wangepakia watoto wanapoenda mashuleni na vyuo bure.