Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Katika kipindi hiki cha kampeni za urais, nimekuwa nikimwona huyo jamaa aliyevaa ‘Kaunda suti’ ya buluu hapo kwenye picha, akiwa pembeni ya Tundu Lissu karibu kila sehemu.
Nikiangalia mavazi yake pamoja na hako ka peni alikokachomekea kwenye mfuko wake wa shati, naona ana fit profile ya wale walinzi kutoka serikalini ambao huwalinda viongozi wa nchi.
Najua kwa nchi kama Marekani, wagombea urais wa vyama vikuu [Republican na Democrats na pengine hata wale wa kujitegemea kama Ross Perot] hupatiwa ulinzi wa Secret Service.
Sasa kwa Tanzania sijui. Kama kuna anayejua, itapendeza akitujuza wale ambao hatujui.
Manake kila nikimwangalia huyo jamaa naona kama vile anatoka kwenye hicho kitengo cha walinzi wa viongozi.
Kama anatokea huko, ni jambo ambalo ni la mwaka huu tu hususan kwa Tundu Lissu au ni ndivyo ilivyo miaka yote ya uchaguzi?