Mkataba upi unaoweza kulinganisha na $190 Billion?!Yes ili kuweka good terms, na ndio maana wakatoa Dola milioni 300 na mkataba ulisainiwa upya ili kuinufaisha TZ kitu ambacho hakijawahi kufanyika tokea TZ imeanza kujihusisha na masuala ya madini
Hivi una habari hata Capital Gains Tax hawakulipa wakati sheria inasema ukiuza shares unatakiwa kulipa capital gain tax?
Na suala la mkataba kusainiwa upya, thanks to Sheria ya Madini ya mwaka 2010, ambayo ilianza kutumika 2012 ambayo inasema mikataba inatatakiwa kuangaliwa upya kila baada ya miaka 5.
Na hata suala la sisi kumilikishwa shares za "Acacia" ni matokeo ya hiyo Sheria ambayo ilianza kutumika 2012!
Kwahiyo SIO KWELI kwamba ni amsha amsha za JPM ndizo zilileta hizo mambo, bali aliingia madarakani wakati keshatenegenezewa sheria ya kufanya alichofanya! Labda apewe credit ya kupata 16% kama unaamini rais mwingine angewezesha kupatikana chini ya 16% lakini suala la kumilikishwa, lipo kisheria, na SHERIA HIYO HAKUINZISHA YEYE!!
Hapo kabla hilo halikufanyika kwa sababu, kama nilivyosema, hiyo sheria imeanza kutumia 2012, na review of dev agreement inatakiwa kufanyika after every 5 years.