na wapuuzi kama nyie eti tutashitakiwa Miga, mbona accecia walifutiliwa mbali na hawakwenda mahakamani Kudai fidia,Kama walikuwa halali na hawaibi?
Kwanza mpuuzi ni wewe unayeshindwa hata kuandika kwa Kiswahili fasaha, kenge wewe!!
Pili, ni mpumbavu tu ndie anaweza kusema mbona hao Acacia hawakwenda huko MIGA manake kila mwenye akili timamu anafahamu Acacia hawakuwa na sababu ya kwenda kwa sababu Serikali ya Mtukufu ilishaingizwa chaka, ama kwa kutofahamu au watu walishakula chao!!
Hivi ungekuwa wewe ndo Acacia, ungeenda MIGA kufanya nini wakati:-
1. Mliambiwa mnadaiwa kodi TSZ Trilioni 450 lakini mnatoa kishika uchumba cha Sh 700 Billion, ambayo haifiki hata 0.5%, tena unakubaliwa kulipa kwa mafungu halafu mnapigiwa makofi!
2. Mmefanya share transfer au mmeuza 34% ya share wakati Sheria inasema unapouza share unatakiwa kulipa 30% kama Capital Gains Tax, lakini hamkulipa!
3. Mmeambiwa itabidi mjenge kiwanda cha kuchenjua hayo makinikia hapa hapa, nanyi mnasema haitalipi, na kwahiyo mnaruhusiwa muendelee kupeleka makinikia Japan!
Sasa kama unatumia kichwa chako sawasawa, na wewe ndie Acacia mwenyewe, hapo ungeenda MiGA kufanya nini?! Soma ile framework uone kilichoandikwa!!
Hivi kwa akili yako pamoja na favors zote hizo bado ulitarajia Acacia waende MIGA ambako kesi zinachukua zaidi ya miaka 5 wakati pale bandarini kulikuwa na makinikia yanayochangia 30% ya mapato yake!!
Lakini kama msingefanya ujinga wa kutoa favors zote hizo, Acacia wangeenda tu kwa sababu wasingekubali kulipa anything like trillions ambazo mlikuwa mnafurahia kwamba mnawadai!
Soma thread hii hapa kuhusu nini alisema Tundu Lissu na ujue ni kwanini jamaa walikuwa wanajidai sana! In short Lissu aliwaambia kama kweli tupo serious na hizi kampuni za madini, basi tujiondoe kwanza MIGA kwa sababu ukishajitoa kule, wanakuwa hawana pa kukimbilia zaidi ya kwenye mahakama zetu wenyewe!!
Lakini kwavile bado tulikuwa MIGA, Acacia na Barrick bado waliendelea na danadana zao, na serikali ilikuwa inahofia ku-press hard kwa sababu, ingawaje wewe mpiga makofi hujui lolote, wenyewe ( serikali) walifahamu hawa ukiwakandamiza hadi wakose pumzi, watakachofanya ni kukimbilia MIGA ambako TUSINGETOKA kwa sababu hata ukaguzi wenyewe ulikuwa wa upande mmoja, na usingekuwa na nguvu zozote kisheria!
Halafu ndugu yangui
TUJITEGEMEE, Serikali ya Mzalendo Magu ilipeleka wapi 30% yetu ya Capital Gains Tax?