Hivi uandishi wa habari Tanzania ni tofauti ma nchi nyingine? Kazi hasa ni zipi?

markp

Senior Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
194
Reaction score
327
Kwa wataalamu wa mambo ya sanaa pamoja na sayansi ya uandishi wa habari napenda mtujulishe kazi zao zina mipaka kiasi gani kwa viongozi wa nchi?

Habari zinazoandikwa na kuripotiwa ni zile zinazojitokeza zenyewe tu by nature hakuna habari za uchunguzi za kisiasa.
wanachunguza mambo ya afya za wanadamu utafikiri wao ni madaktari, habari za michezo utadhani wanamiliki timu

Linapofikia kuchunguza au kuuliza maswali magumu na muhmu kwa viongozi wa serikali wanaogopa kama watuhumiwa.

Unakuta habari zimeenea kwenye mitandao ya kijamii mfano wa hili la naibu spika kugombea uspika wakati bado amehodhi nafasi yake ya unaibu. Waandishi wanapajua nyumbani kwake wanajua ofisi yake ilipo wanashindwaje kwenda tu kumuuliza swali ambalo linawasumbua wananchi mjini na vijijini?

Maswala ya haki za muungano kwa bara na visiwani imekuwa mjadala kwenye mitandao na mitaani kuna tetesi kuwa mama anapendelea hivi wandishi wa habari.

Hawana aksesi ya kuuliza mambo kama hayo kwa viongozi ili kupata majibu.

Matokeo ya watu kupewa kesi za ugaidi au uhujumi uchumi ni uzembe wa waandishi wa habari utadhani hawana umoja.

Mwandishi wa habari anashindwa kuhoji kero za wananchi kwa viongozi wa serikali wanaona ni kazi ya wapinzani na wabunge. Matokeo yake mpinzani akihoji na vile anaitwa mpinzani anapewa mkesi wa ugaidi.

Mbunge akihoji anatakiwa ajiudhuru mwananchi ukihoji unapotezwa au kuwekwa kwenye kiroba unatupwa baharini ukome.

Mwandishi wa habari ni mtu wa kipekee anayeweza kupenya popote na kuleta majibu kwa wananchi ili kuuza habari. Wetu hawa wanatoa ripoti zisizo na ripoti.
 
Naomba P na Kabendera na wengine waliowahi kuwa wahanga wa mihimili watusaidie uzoefu🤔.
 
Kwa mfano unaambiwa nitawatoa kazini wapumzike ili wajiandae vizuri 2025 halafu baadae unaambiwa hapana wanakazi nyeti ya usimamiz, utafuta gazeti.
 
Bongo hatuna waandishi ndugu, hili jambo la tulia hapo kenya ungekua mjadala kwenye maredio na mativii.
 
Kupindi Ndugai ameitisha press conference ya kuomba msamaha, waandishi wa habari wangemuuliza Ndugai swali hili:

"Je, nini maoni yako kuhusu serikali inayoongozwa na rais Samia kukopa"

Waandishi walitakiwa wamuulize hilo swali Ndugai, kwa sababu alikuwa anaanza kujiuma uma kwamba alisingiziwa, kwamba yeye hajasema!, amenukuliwa vibaya.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa wataalamu wa mambo ya sanaa pamoja na sayansi ya uandishi wa habari napenda mtujulishe kazi zao zina mipaka kiasi gani kwa viongozi wa nchi?

Habari zinazoandikwa na kuripotiwa ni zile zinazojitokeza zenyewe tu by nature hakuna habari za uchunguzi za kisiasa.
wanachunguza mambo ya afya za wanadamu utafikiri wao ni madaktari, habari za michezo utadhani wanamiliki timu

Linapofikia kuchunguza au kuuliza maswali magumu na muhmu kwa viongozi wa serikali wanaogopa kama watuhumiwa.

Unakuta habari zimeenea kwenye mitandao ya kijamii mfano wa hili la naibu spika kugombea uspika wakati bado amehodhi nafasi yake ya unaibu. Waandishi wanapajua nyumbani kwake wanajua ofisi yake ilipo wanashindwaje kwenda tu kumuuliza swali ambalo linawasumbua wananchi mjini na vijijini?

Maswala ya haki za muungano kwa bara na visiwani imekuwa mjadala kwenye mitandao na mitaani kuna tetesi kuwa mama anapendelea hivi wandishi wa habari.

Hawana aksesi ya kuuliza mambo kama hayo kwa viongozi ili kupata majibu.

Matokeo ya watu kupewa kesi za ugaidi au uhujumi uchumi ni uzembe wa waandishi wa habari utadhani hawana umoja.

Mwandishi wa habari anashindwa kuhoji kero za wananchi kwa viongozi wa serikali wanaona ni kazi ya wapinzani na wabunge. Matokeo yake mpinzani akihoji na vile anaitwa mpinzani anapewa mkesi wa ugaidi.

Mbunge akihoji anatakiwa ajiudhuru mwananchi ukihoji unapotezwa au kuwekwa kwenye kiroba unatupwa baharini ukome.

Mwandishi wa habari ni mtu wa kipekee anayeweza kupenya popote na kuleta majibu kwa wananchi ili kuuza habari. Wetu hawa wanatoa ripoti zisizo na ripoti.
Hata magazeti ya maana hutana hata moja, gazeti la mwananchi linajitahidi ila nalenyewe bado na lipa 30% Radio zimeja vipindi vya michezo na habari za wasani,......ndo hapo ndo tunataka kujiliganisha na jilani wetu Kenya uhuru wa habari bado sana Tz ndo nchi peke wasomi na wasio wasomi hawatofaoutiana sana kimawazo na kifkra
 
Back
Top Bottom