Hivi ulishawahi kupenda mtu, mpaka ukimwona unamwogopa!

Sasa mbona kuna mtu nampenda sana inawezekana yeye hanipendi au 😭🀣🀣🀣
Hata kama naye anakupenda, lakini upendo wenu ukiwekwa kwenye mizani, lazima utakuta mizani ya upendo wako itahang juu, kwa mwenzako itakuwa chini.

Penzi kamwe halijawahi na halitakuja kulingana katika wapendanao.
 
Kuna demu nilimpenda kinoma nikawa,nikimwona moyo unashtuka,lakin nilikuja kutafakari nikaona...nitakuja kuumia kizembe sana nikaanza kumtafutia kasoro mpaka nikamsahau.

..ila yule binti ni mrembo ana akili,ngozi poa,anaongea taratibu, sijawahi tangu nikuwe mkubwa.... ona watoto wa arusha ni noma 🀩
 
Habari wakuu.

Hivi ulishawahi kupenda mtu,yaani mpaka wewe mwenyewe hujiamini kama upo naye ,ukiombwa chochote , unatoa bila kupepesa macho, na hata kama huna unashindwa kusema, hivi ulitokaje kwenye huo mtego kuna ndugu yangu anaangamia hapa !
Hapana.
 
Kuna mmoja hivi anaitwa fay nilimtongoza miaka kadhaa akanichomolea lakini nilimpenda sana yaani hata namba yake ipo kichwani,nilimwambia niko radhi hata kufa kwa ajili yako lakini hakunipenda now kashaolewa huko na ana mtoto ila bado naview status zake moyo bado umependa ndo hivyo mke wa mtu now.
 
Ishu ni kibunda tu mwanaume ukikosa confidence inapungua, huwezi kujiongopea, unaweza ukawa nacho ila unaona kabisa kwa mwanamke ulienae bado hakitoshi ila anahisi unauwezo hapo ndio kipengele, anakuamini alaf wewe hujiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…