Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Ipo sana kwenye familia,ila ni jambo baya sana kwa mzazi kuonyesha mapenzi makubwa kwa mtoto mmoja kuliko wenzie,wale wanaobaguliwa au kuonyeshwa mapenzi kidogo,hii huwakaa moyoni na ukubwani watalipa kisasi kwa wazazi,watakuwa hawana mapenzi na wazazi wao kabisa,huwa ni mbegu mbaya wazazi wanakuwa wamefanya,
 
Hata kwenye familia bukiachilia baba na mama.
Ndugu kukuchukia.
Nimezoea.,sijali wala nn
 
Ndugu yangu wa kwanza alipendwa sana,na wadogo zangu pia,mie nilikuwa nachukuliwa kama mtu bwege bwege hv,na kilichoniuma ni wazazi kuona ni kitu Cha kawaida kunitamkia kuwa mie ni mjinga mjinga,kubwa jinga huku wanacheka,wakichukulia kama utani,kitu kibaya kikifanyika,wa kwanza kushukiwa ni mie,hii kitu iliniuma sana na inauma sana mpaka leo,matokeo yake nilianza kujenga roho ya kuwa independent nikiwa mdogo sana,nikaona hapa kitu pekee Cha kuniokoa ni kitabu,nilisoma sana hakuna aliyeweza kunifikia kwa uhodari kwa ndugu zangu,nilibamiza mitiani na ndugu zangu hakuna aliyeweza kuwa na mafanikio ya kitaaluma kama Mimi.
Tumeishakuwa watu wazima,lakini kwa madhara yale ya kubaguliwa nikiwa mtoto huwa Sina uchungu na mapenzi kwa wazazi kabisa,mpaka wenzangu huwa wanashangaa,nikisikia mtu anasema anampenda mama yake kuliko kitu chochote,huwa nashangaa sana,sasa hv nimeishakuwa mzazi najitahidi sana kuonyesha mapenzi Sawa kwa kila mtoto wangu,kila mtoto Nampa nafasi ya kuwa anavyotaka yeye sio kulazimisha awe kama wenzie.
 
Mkuu umeandika kwa hasira sana na jazba, hakika psychology haidanganyi.. inawezekana kabisa ulichokikosa wewe ni up3ndo na ukaribu connection yako na wazazi/mzazi.

Upendo ni Amri kuu na ya Kwanza!
 
Inasikitisha sana hata wazazi huwa wanakosea sana kwenye malezi yao kwa watoto!

Kumuita mtoto mjinga, taahira over n over , au kumuonyesha kumbaguwa wazi wazi...unamjengea picha mbaya mtoto!!
 
Mimi nimezaliwa peke yangu sina experience hiyo. Ila kama mzazi mzani hauwez kua sawa kuna mahali utazidi tu. Hiyo ni hali ya kawaida kwa mzazi yeyote unawapenda watoto wako wote ila mzani utazidi tu kwa mwingine.

Mara nyingi wa kwanza anapendwa zaidi na wa mwisho ni kudeka deka kunaweza onesha anapendelewa sana ila mfungua njia upendo mwingi hua kwake.
 
Toto la mwisho Hujambo?!!!.
 
Mkuu umeandika kwa hasira sana na jazba, hakika psychology haidanganyi.. inawezekana kabisa ulichokikosa wewe ni up3ndo na ukaribu connection yako na wazazi/mzazi.

Upendo ni Amri kuu na ya Kwanza!
Sio kwel mkuu.wazazi wangu have been so lovely considering i am the only born kwa mama yangu i was one of the best kwa baba yangu ambako tuko wengi but i was the first kid to excell in almost everything compared to my bloods.mzee wangu ni moja ya vitu alipendea but haikua na maana hakuwapenda wengine
So sijawah kosa upendo hata kidogo

Ila tu i hate hiz mambo za kuendekeza sana watoto i really do hate..that is y vijana now days wanakuwa wapumbavu sana mpaka kwenye maisha ya kujitegemea na kujisimamia..even simple life manners tu ni tatizo.
 
Ipo sana hii kitu,kuna siku nliwahi kumtolea uvivu dingi nikamwambia niliwahi kukusikia siku moja unaongea kuwa katika sisi watoto wenu mtoto flani unampenda zaidi kuliko wengine,nikaona mzee mzima anajihami kikubwa,lakini ukweli ni kuwa familia nzima hilo wote tunalijua kuwa yule ndio kipenzi chake.Sasa na mimi juzi kati yamenikuta,mtoto wangu mkubwa nimesikia analalamika kuwa nampendelea zaidi mwenzake wacha nianze kujiahami,ila nimejitafakari nikagundua kuwa yuko sahihi nilizidisha kidogo mahaba upande mmoja...
 
Sawa ww me au ke
 
Nimekupata mkuu..
Inawezekana watu wana udefine upendo kwa namna nyingine wanajikuta wanalea watoto kimayai mayai.. mwishowe wanaharibikiwa kiakili saikolojia hata kiafya..
Unakutana na mtoto mdogo darasa 2~4 ana kilo za mtu mzima, yani mama kanenepeana na mtoto kanenepean inabidi wote waanze maozeiz ya kukata kitambi road walk😂😂..
Malezi mengine hayafai kama mtoto kuwa na obesity ni kosa la mzazi kumuhatarisha afya mtoto
 
Mimi Nina watoto wawili huyu wa kwanza wakati nampata nilikuwa niko njema kwahiyo nikampeleka hizi shule za English medium, wa pili nikawa nimefulia kwahiyo nimempeleka shule za kayumba roho inaniuma kwa nini yule asome shule ile huyu asome shule hii kwaiyo nimeamua mwaka ujao wote kayumba ili niweke mizani Sawa. Kuwapeleka wote siwezi maana kila siku watabaki nyumbani kwasababu ya ada.
Sina upendeleo ni hali ya maisha imebadilika,asiejua atahisi hivyo hata huyu mtoto wangu wapili badae atajua nilimbagua ila kumbe sio ,jiwe ndio kasababisha.
 
Hii mada nilimchanaga Bi mkubwa kitambo sana kama miaka 10 nyuma ila mpaka leo analalamika kuwa nilimwambia hanipendi [emoji28]...
Huu upendeleo upo, na sio kwamba tunasema mzazi hakupendi La hasha! wanatupenda ila kuna upendeleo fulani sijui ndo tuseme ubaguzi.

Halafu mnaosema Last born wanapendelewa, nakataa hii hoja kwa experience! mimi mwenyewe Last born, mimi mwenyewe ndo nmepewa jina la mama ake Bi mkubwa, Halafu mimi huyo huyo ndo mtoto wa kike pekee kwetu. Ila huo upendeleo haujanidondokea kabisa kote kote..

Naamini binadamu anakupenda akiamua tu, hahitaji sababu za msingi, mana unaweza kuwa na msaada na mzazi ukafanya kila kitu ila ndo ivyo huna kura za ndio, wakati huo huo kuna bro anapita bila kupingwa[emoji1787][emoji1787] na hana sifa hata moja!

Katika kitu namuomba sana Mungu nikiwa mama, jambo la kwanza naomba nisiwe na huu utopolo maana najua fika unavyouma! ukiwa kipenzi cha mzazi hata ukikosea unawekewa defence, sasa ukute kipenzi chao halafu umefanikiwa [emoji86] wengine wote mnakua mafisi.
usipokua kipenzi cha wazazi basi Merit unazofanya zinakua za wote, ila ubaya unakua wako...Na katika kitu ambacho wazazi hawajuagi ukionyesha kumpenda sana mtoto unamtengenezea uadui na wenzie.

Na ukiwa last born halafu hujafanikiwa utajuta utatumwa wewe na mmeo na watoto wako kwenye vikao vya familia, mimi binafsi naitambua nafasi yangu kwetua ni mpanga mipango na mtekelezaji mkuu.. zile Responsibility za familia zote mimi ndo nizibebe
 
Katika TV series ya "The Crown", ya Ufalme wa Uingereza, kuna episode moja Malkia Elizabeth alikuwa anaongea na mume wake Prince Philip(ambaye amefariki hivi karibuni), Malkia Elizabeth alikuwa anaangalia TV, walikuwa wanaonesha mtoto wa Waziri Mkuu Margareth Thatcher alivyopotea jangwani.

Malkia akasema ameshangaa sana Thatcher kusema huyo aliyepotea ni mtoto wake anayempenda kuliko wote. Malkia akasema suala hilo ni "interesting". Prince Philip akas3ma mbona kawaida tu hiyo. Malkia akasema inakuwaje Mama asema anamoenda mtoto mmoja zaidi ya mwingine, hususan kwa mapacha?Prince Philip akamuuliza Queen mtoto wake anayempenda kabisa ni yupi?

Malkia akakataa katakata kwamba ana mtoto mmoja anayempenda zaidi.

Prince Philip akakataa, akamwambia mkewe lazima kuna mmoja unampenda zaidi.

Malkia akakataa, akamuuliza mumewe , yeye Philip anampenda nani zaid?

Prince Philip akasema hilo swali rahisi sana, akasema anampenda binti yake (Princess Anne) zaidi.

Nikasema haya mambo yapo mpaka kwenye falme huko.

Clip ipo Youtube hapa chini.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…