Sasa kwann usimwambii mwenzio kama humpend ili ajue na yy aanzishe maisha yake anaweza pata mtu atakae mpenda kuliko unavyomfanyia kumbuka huyo mchepuko wako nae ukimuoa utajikuta unamuona wakaida na hutompenda ...siku zote mapenz ya uhawara huwa hayaishi hamu hata mkae miaka 20 sababu kila mtu yupo kwake mkikutana kila mtu anakua hot hamjagusana kitu kimelegea ila ndoa uvumilivu mwenzio anashinda na wtt kaz za nyumban zote Zake stress kwenda mbele na bado mda wa tendo huwez kumpa maneno matamu yakumsahaulisha stress zake we ukigusa kiuno ukiona halegei unaweka mate unamaliza mchezo ..kwa stail hyo utamchukia mkeo maisha yako yote ...wanaume weus hamjui kuwapet pet wake zenu ni wabinafsi mnajijali nyie tu.
Haya mambo ya ndoa ni kuomba Mungu akupe mtu mnayefanana. Ni kama mchezo wa bahati nasibu, kama mdogo wako anateswa na mumewe basi yupo mwanaume vike vile anateswa na mkewe kama mdogo wako.
Kazi niliyokuwa nafanya awali ilikuwa kwenye NGO inayohusika na maswala ya kutoa ushauri wa kindoa na kusaidia kinamama walotelekezwa pamoja na watoto na pia watoto wa kike walio katika mazingira hatarishi.
Swala la ndoa ni swala pana, dhana ya kusema wanaume pekee ndiyo wanaocheat ilinitoka hapo.
Kuna wanawake wanapendwa jamani, mume anajitoa kwa kila hali na kwa kila jambo mpaka unasema huyu dada ana bahati jamani. Lakini mwanamke hasikii haelewewi anacheat, anatoroka nyuumbani kwa visingizio vya kijinga anaenda kwa kudumu.
Mpaka mwanaume anakuja kulalamika then mke anaitwa na psychologist anahojiwa kuna tatizo gani kwenye ndoa anasema hakuna!! Kinachokufanya ufanye uovu ilhali mumeo anakupenda ni nini, anajibu basi tu shetani kanipitia sirudii tena na baada ya siku mbili karudia. Yaan ni kero tupu.
Huo ni mfano mmoja lakini tatizo kubwa ni kwamba wanaume wengi huwa hatuzungumzi matatizo ya ndoa. Wengi tunajaribu kusolve wenyewe ndani kwa ndani na kuugulia na hata wengine unakuta tunajikuta tunakuwa walevi tukijaribu kutafuta faraja. Mbaya zaidi ukianza kunywa pombe hapo napo ndipo mwanamke anapatia kisingizio kwa kusema huyu bwana mlevi na kwa sababu unaonekana hakuna wa kupinga. Kesi ishahama.
Kwa wanaume wengi ukiona tatizo limetoka nje yaani kaanza kulisema basi ujue lishamfika mtu kooni. Hali hii husababisha jamii kuhisi kuwa watendwa ni wanawake tuu na wanaume hawatendwi.
Nimeshuhudia kesi nyingi sana wanaume wanakuja wanaongea wanalia, wake zao wanawatesa yaan mke hapendeki hata afanyeje na hata mke akiitwa akiulizwa tatizo nini hana jibu.
Nasikitika ile NGO ilikuwa moja tu mkoa ule ila sasa ishafungwa miaka kadhaa iliyopita.
Dhana ya wanaume weusi sijui nini na nini na kwa kuchukulia mfano mmoja wa mdogo wako bado hukutenda haki. Ingekuwa wazungu pekee ndiyo wapo smart kwenye mahusiano basi nchi zao zisingekuwa na migogoro ya ndoa!!
Nitajaribu kuattach takwimu ya migogoro ya ndoa ambayo ipo officially nchi za weupe uone jinsi ilivyo mingi na hiyo ni ile imefikishwa idara husika upate picha idadi ya wanaume wa kizungu wanaolalamikiwa kwa unyanyasaji wake zao!!
Cha msingi hapo wewe shukuru Mungu umebahatika mtu anayekujali. Mwenye caring inayokuridhisha lakini zaidi ya yote mmeendana vinginevyo kunao wenzio wanalalamika vile vile kuwa wanaume wa kizungu hawana maana.
Vice versa, wanawake pia wananyanyasika sana. Kama hujaoa/hujaolewa omba sana Mungu pia kuwa makini na historia ya familia unayoenda kuoa/kuolewa. Ukikuta familia nzima ina historia ya kutokudumu kwenye ndoa kimbia hapo ujue kuna pepo. Mfano baba na mama waliachana, watoto wapo saba wanaoa na kuacha na wakike wanaolewa na kuachwa hakuna anayeishi kwenye ndoa ya furaha.
Ukija kwa mababu nako hivyo hivyo. Hapo kimbia tuu