Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,650
- 21,014
Sijajuaga hii ishu. Watu wengi wanasema usiku tule vyakula laini laini. Lakini kuna hii ishu.
Mtu akisha kula chakula damu nyingi inaelekea tumboni kusaidia ishu za umeng'enyaji na ufyonzaji wa msosi. Kitendo hicho hufanya damu inayoenda kwenye sehemu zingine kupungua. Damu inayoenda kwenye ubongo ikipungua mtu anaanza kujihisi uchovu.
Hii ndiyo sababu mtu akila chakula hasa chakula cha nguvu lazima aanze kuhisi usingizi.
Sasa tukila chakula cha nguvu mchana, muda wa kazi na kuanza kusinzia si inaharibu uzalishaji na umakini wetu.
Tukila usiku chakula cha nguvu na kuanza kusinzia na huo ni muda wa kulala, si ndiyo safi!!.
Nimefuatilia nchi za magharibi nimeona kuwa kwao dinner ni chakula cha muhimu sana cha siku. Kunakuwa na mapochopocho ya kutosha. Mchana wanarashiarashia tu.
Kuna sababu za kitaalamu za kusema tule msosi mlaini usiku?