Hivi Vijana wa CHADEMA Wanatumia kitu gani kinachoharibu uwezo wao wa kufikiri na kujenga hoja? Mbona hawana adabu wala hekima?

Hivi Vijana wa CHADEMA Wanatumia kitu gani kinachoharibu uwezo wao wa kufikiri na kujenga hoja? Mbona hawana adabu wala hekima?

Acha kudanganya watu hapa na kufanya upotoshaji, bila Shaka habari ya kushuka kwa Bei ya mafuta inekuumiza na kukusononesha Sana moyo wako
Thubutu yake kwa hii nchi..!! Kushuka mafuta?. Kwa tunaojua mapigo ya akina miguru na makatani,hapo wanamtafutia target mama . Hiyo ni danganyatoto. Na hapo kwa akili za WaTz ni kweli tutapumbazika kama wewe ulivyopumbazika. Lakini nakupa miezi mi3 tu bei itakuwa juu zaidi ya ilivyokuwa mwanzo. Tupo hapa hapa jukwaani utakuja kuniambia mkuu
 
Juliana shonza,mwampamba (jokate)dadeki nyie wanyiha nyie🙆🙆🙆🙆
 
Lakini Vijana wa UVCCM wao ni wema sana ndo maana wanajisifia kuua watu na kuwapiga mpaka kuwaumiza vibaya halafa UWT wanawatetea wauaji [emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ondoa mawazo ya kikabila na ukabila katika akili yako maana tulishapita huko, usitake kutuletea Zimwi la ukabila hapa, Hapa Ni hoja kwa hoja, Muache dada yangu mh Juliana Shonza mtetezi na Tumaini la akina mama mkoa wa Songwe,
Juliana shonza,mwampamba (jokate)dadeki nyie wanyiha nyie🙆🙆🙆🙆
 
Ndio maana alisema iwe ndani au nje ya chama akimaanisha Ni lazima tuijenge utamaduni wa kuheshimiana na kukosoana kwa heshima na adabu, kunyooka nao maana yake kutoa taarifa mahali husika ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa utaratibu wa kisheria
Kwani ndugu yangu Lucas mwashambwa "kumsema vibaya Rais" mantiki yake ni nini hasa toka kwa mwanaCCM mwenzake Bi Tulia Ackson..?

Hebu tuchukulie mfano mtu fulani aseme hivi kwa uhuru wake;

"...Serikali ya Rais Samia ni dhaifu sana, ya hovyo sana na haizingatii wala kutilia maanani utawala wa sheria na kidemokrasia. Mfano, juzi kati hapa polisi wake wameua watu kule Serengeti kinyume cha sheria. Pamoja na haya, Rais Samia kimyaa na hii inaonesha kuwa ni amri yake. Kwa hiyo huyu mama hafai kuwa Rais wetu na yuko kimakosa hapo alipo. Kwa hiyo ndugu zangu, huyu mama akigombea nafasi hii tena mwaka 2025, asipewe kura hata moja na lazima aondolewe kwa sanduku la kura mwaka 2025..."

Hivi kwa maneno haya huyu mtu anakuwa "amemsema vibaya Rais" na kwa hiyo kwa mujibu wa Spika Dr Tulia Ackson, basi vijana wa CCM mnaweza kuruka naye kumshughulikia na kumpoteza kabisa mtu huyu..?

Hebu jaribu kutufafanulia mantiki ya kauli ya mwanaCCM mwenzako alikuwa ana maana gani...!
 
Kwani ndugu yangu Lucas mwashambwa "kumsema vibaya Rais" ni kama vipi kwani?

Hebu tushukurie mfano niseme hivi;

"...Serikali ya Rais Samia ni dhaifu sana na haizingatii wala kutilia maanani utawala wa sheria na kidemokrasia. Huyu mama hafai kuwa Rais, lazima aondolewe kwa sanduku la kura mwaka 2025..."

Hivi kwa maneno haya ninakuwa "nimemsema vibaya" Rais na kwa hiyo kwa mujibu wa Spika Dr Tulia Ackson, basi vijana wa CCM mnaweza kuruka na kumpoteza mtu huyu..?

Hebu jaribu kutufafanulia mantiki ya kauli ya mwanaCCM mwenzako alikuwa ana maana gani...!
Kabla ya kuhitaji nikufafanulie embu nenda kapitie maandiko katika kurasa za akina mdude za mwezi mzima halafu uniletee majibu hapa, ukitoka hapo nenda kawasikilize na kuwasoma pia akina pambalu na kakikundi Jake ndio utaelewa nacho zungumza hapa, kapitie post zao mbalimbali uone nacho kizungumza
 
Kabla ya kuhitaji nikufafanulie embu nenda kapitie maandiko katika kurasa za akina mdude za mwezi mzima halafu uniletee majibu hapa, ukitoka hapo nenda kawasikilize na kuwasoma pia akina pambalu na kakikundi Jake ndio utaelewa nacho zungumza hapa, kapitie post zao mbalimbali uone nacho kizungumza
Lucas mwashambwa tetea hoja yako kwa hoja..

Usiniambie mimi niende kwa kuna Mdude au sijui Pambalu nk. Mimi siwajui hao. Kama kuna waliosema, basi hayo ni maoni yao na kwa mtindo (style) yao ya kutoa maoni..

Kama unadhani umetukanwa au uko offended na maneno ya kina Mdude au ya mtu mwingine yeyote, na unahisi ni kinyume cha sheria, basi mshauri mtu huyo aende mahakamani ili apate haki yake...!

Lugha mbaya na ya matusi yenye athari hasi ktk jamii kwa mapana makubwa ni ile ya Spika Tulia Ackson kwa sbb directly alikuwa ana - instigate violence (machafuko) ktk jamii..

Pigia kelele hao ndugu. Na kama huoni hilo, basi wewe ni kiziwi na kipofu wa ufahamu...!
 
Lucas mwashambwa tetea hoja yako kwa hoja..

Usiniambie mimi niende kwa kuna Mdude au sijui Pambalu nk. Mimi siwajui hao. Kama kuna waliosema, hayo ni maoni yao na kwa mtindo (style) yao ya kutoa maoni..

Kama unadhani umetukanwa au uko offended na maneno ya kina Mdude au na mtu mwingine yeyote, na unahisi ni kinyume cha sheria, basi mshauri mtu huyo aende mahakamani ili apate haki yake...!

Lugha mbaya na ya matusi yenye athari hasi ktk jamii kwa mapana makubwa ni ile ya Spika Tulia Ackson kwa sbb directly alikuwa ana - instigate violence (machafuko) ktk jamii..

Pigia kelele hao ndugu. Na kama huoni hilo, basi wewe ni kiziwi na kipofu wa ufahamu...!
Sasa hapa nashindwa nikisaidiaje maana unasema huwafahamu hao, wakati kwenye maada yangu imejikita katika kuwazungumzia vijana wa chadema namna walivyokosa adabu na hekima kwa Tabia zao za kutukana matusi na kuweza kumtukana yeyote atakaye tofautiana nao mtizamo, Sasa Kama unasema huwafahamu Basi hata maada hii itakuwa ngumu Sana kuielewa
 
Sasa hapa nashindwa nikisaidiaje maana unasema huwafahamu hao, wakati kwenye maada yangu imejikita katika kuwazungumzia vijana wa chadema namna walivyokosa adabu na hekima kwa Tabia zao za kutukana matusi na kuweza kumtukana yeyote atakaye tofautiana nao mtizamo, Sasa Kama unasema huwafahamu Basi hata maada hii itakuwa ngumu Sana kuielewa
Nilikuelewa kwa kusoma heading ya mada yako tu, nikaelewa wewe ni mtu usiyejua utakalo wala uandikalo..!!

Ngoja nikufundishe kitu kimoja ktk sanaa (art) ya uandishi...

Kwamba, unapoandika juu ya tabia ya mtu fulani iwe nzuri au mbaya, basi ni lazima uwe na mifano halisi kuthibitisha hilo ktk maandishi yako..

Wewe hujafanya hivyo. Andiko lote mwanzo mwisho ni unataja Jina la mtu tu na kumpaka ubaya bila kuthibitisha kwa mifano ubaya huo..!

Cha ajabu, sisi wasomaji wako tunapokuuliza mifano ya ubaya wa mtu huyo, unatuambia tumtafute huko aliko...!

Umeshindwa nini kutoa hadharani hayo unayoita matusi ya kina Pambalu au sijui Mdude hapa ili uthibitishe ubaya wa watu hao, kwamba ni watukanaji..???

Kwa sababu it's possible kuwa unachokitafisiri wewe kuwa ni "tusi" au "matusi" ni ujinga wako tu wa kukosa ufahamu. Weka hizo statement unazotafsiri kuwa ni matusi ili usaidiwe kueleweshwa/kutafsiriwa...

Lakini kwa kutofanya hivyo, mimi sioni ubaya wowote kukuita wewe kuwa ni MWONGO na MZUSHI tu...

Pole sana...
 
haya ndo matokeo ya kubatizwa kwa moto.akili zao hazipo vizuri usiwalaumu sana.
Waliteseka
 
Ndugu zangu nimeuliza nipate kusaidiwa kupewa majibu maana nikiangalia na kufuatilia kwa makini naona hatari kubwa Sana iliyopo mbele ya chama hiki, wataalamu wanasema kuwa ukitaka kujuwa urefu wa maisha ya chama chochote Basi huna budi kuangalia uwezo wa kiuongozi wa vijana waliopoo katika chama husika ambao ndio hasa watakao kuwa viongozi wa kesho

Lakini ukiangalia na kutupia jicho kwa vijana waliopoo ndani ya chama hiki na ambao ndio viongozi kwa Sasa kiukweli unasikitika Sana na kuwaza sijuwi wanakula vitu gani huko chamani kwao,

Ni vijana waliokosa adabu hekima busara unyenyekevu na staha, Ni vijana waliojaa matusi utazani wameopolewa kwenye pipa la Pombe ya kienyeji, Ni vijana ambao kwao yoyote na wa umri wowote na wa cheo chochote anaweza kutukanwa matusi yote yanayoandikika na yasiyo andikika, Ni vijana waliojaa mihemuko na kuripuka Kama Moto wa gesi,

Kibaya zaidi vijana Hawa wa chadema Ni Kama hawana mlezi, hawana mtu aliyesimama Kama mzazi wao kimalezi, Hawana mtu wa kuwaongoza na kuwafunda, hawana mtu wakuwapa maelekezo, hawana mtu wa kuwachunga ili wakue kiuongozi, hawana mtu wakuwafunga breki ya midomo yao, Hawana mtu anayeweza Akazungumza wakamsikiliza na kumheshimu, hawana wazee huko, Ni vijana waliozibuka na kuzuzuka, Ni vijana wanao jazana ujinga muda wote, Ni vijana waliokosa muunganiko wa ubongo na midomo yao, hawana muunganiko wa akili na vidole vyao

Ni vijana wanao hisi kuwa huo ndio ushujaa, ukamanda wenyewe, ujana wenyewe. Chadema itafika muda kitakosa viongozi na kwa kuwa Hawa ndio kwa umoja wao wa kujazana ujinga na kukosa adabu na heshima watajikuta mmoja wao anakuwa kiongozi mkuu wa chama, hapa ndipo chama hiki kitakapozidi kupiga mueleka Zaid ya hapa kilipo, ndipo kitazidi kusereleka kuelekea shimoni, ndipo kitakapozidi kusambaratika, ndipo kitakapozidi kupuuzwa Zaid ya hapa

Maana hakuna atakaye kuwa tayari kuwasikiliza watu Kama Hawa waliojaa matusi, watu ambao wapo tayari kumtukana yoyote yule kwa matusi ya nguoni bila kosa lolote kisa tu katofautiana nao, hakuna ambaye yupo tayari na atakuwa tayari kwenda kwenye mkutano wao kusikiliza mimatusi tu, hayupo mtu wa namna hii hata siku moja

Sina cha kuwashauri vijana Hawa waliokosa adabu na hekima maana hiyo siyo kazi yangu, Nachoweza kuwaasa ni kimoja tu kuwa watukanane huko huko lakini ikija kwenye mamlaka ya nchi lazima waiheshimu Sana maana wasije wakafikiri kuwa Rais wa nchi Ni sawa na Rais wa Bao, lazima wajuwe kuwa Rais Ni mkuu wa nchi na kiongozi wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama aliye apa kuilinda nchi hii kwa nguvu zake zote ili iwe na amani na utulivu, hivyo hakuna anayeweza kuwavumilia watu wanao hatarisha usalama wa Taifa, lazima watawajibika na kuwajibishwa kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Muulize Tulia aliyeagiza wapigwe!
 
Ukiona mtu mmoja unajiona upo sahihi against watu 100 sio lazima kuwa na PhD kutambua wewe mmoja una shida na hujijui kama una shida
 
Mimi nadhani vijana wa CHADEMA waachwe jinsi walivyo kwasababu pia huwa hawapigi kura. Wakianza kuwa na busara watatupa shida. Au hamkumbuki enzi za BAVICHA ya kina Zitto na Mdee walivyosumbua? Hawa BAVICHA wa nyakati hizi ni wazuri kwa sababu kupitia matusi yao ndo jinsi wanavyozidi kukosa kura. USIWASIKITIKIE
 
Lucas,

Kama wewe ni mzalendo kweli na upendo na nchi yako hatua ya kwanza ni kuachana na chamapinduzi na kujiunga na juhudi za kupata ukombozi wa kweli wa mwananchi, sio siasa nyepesi nyepesi na kansa ya ufisadi. Matusi na maneno machafu humtoka mtu pale ambapo anaona mambo ya hovyo yanaendelea na kuna watu wanaosifia mambo hayo kama wewe. Maana anakuona ni mtu mzima na mwenye akili lakini unashindwa kutumi akaili zako binafsi kuona kwamba kinachofanyika ni uzwazwa. Ili nisiongee maneno matupu nakupa mifano hai:

1. Mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la JHNPP tuliambiwa na serikali inayoongozwa na ccm akuwa ingekamilika mwaka jana mwezi wa sita (or early), kwa sasa taarifa mpya ni 2024 na gharama zimekuwa mara mbili yake, unafahamu kwanini? Kama hufahamu tafuta maarifa hayo.

2. Viongozi TOP wa nchi yetu wametunga sheria naikapitishwa na bunge la ccm ya kupata kinga ya madaraka yao hata watakapostaafu, hii maana yake ni kwamba ikitokea presidaa au yyt kafanya ufisadi wa kutisha, HAKUNA WA KUMSHTAKI WALA KUMYOOSHEA KIDOLE. Kwa akili yako ya kawaida kabisa (achana na ya shuleni) unaona hili ni sahihi, wanaogopa nini kiasi cha kulindwa na sheria.

3. Katazo la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kinyume na katiba ya nchi. Hii ni kwamba mtu anaamka asubuhi na kuamka nchi iendeshwe vipi, anajua wazi anavunja katiba lakini ni hawafu mwenye nguvu kuliko katiba.

The list is so so big, ukihitaji mengine nitaweka. Sasa huku kuona na kuendelea kuwa chawa inakera, mtu anashindwa kujizuia kutukana.
 
Back
Top Bottom