Kuna hawa wadada wanafanya kazi sheri na vijana wakiume mda wote wana hasira huduma zao mbovu sana leo nimepitia pale sheri moja kufika nikamwambia niwekee mafuta ya kiasi fulani nikawa na scan nalipia kwa lipa namba nimelipa vizuri nikamwambia nishalipia kwa lipa namba
Wakaanza kunifokea kwanini unalipia kwa lipa namba na usemi maneno yalikuwa mengi sana nikakosa cha kumjibu na muangalia amalize kuongea akaja kijana mmoja kusikiliza kuangalia muhamala umefika ila kilichomfanya anifokee sikukiona nikaona ana shida na mawazo mengi sana hii sio mara ya kwanza sheri nyingi sana kauli mbovu sana
Neno "sheli" linatokana na jina la kampuni ya mafuta ya kimataifa iitwayo Shell, ambayo ni mojawapo ya kampuni kubwa za kuuza mafuta duniani, ikiwa na nembo ya ganda la kaa (shell kwa Kiingereza).
Wakati biashara ya mafuta ilipoanza rasmi, Shell ilikuwa kampuni ya kwanza au mojawapo ya kampuni zilizotawala soko.
Kwa sababu ya umaarufu huo, watu wakaanza kutumia neno "sheli" kama jina la jumla kwa vituo vya mafuta — hata kama havimilikiwi na kampuni ya Shel
Si vituo vyote vya mafuta vinapaswa kuitwa "sheli".
Kila kituo kinapaswa kuitwa kwa jina lake halisi — kama vile TotalEnergies, Lake Oil, Oryx, Puma Energy, Gapco n.k.
Kwa sababu ya mazoea, watu wengi Tanzania wanatumia neno "sheli" kumaanisha kituo chochote cha mafuta bila kujali jina halisi.
Mfano
Kisahihi: "Ninakwenda kununua mafuta Lake Oil."
Kijamii: "Ninapita sheli pale Sinza."
Hitimisho
Kitaaluma na kiheshima kwa kampuni, ni vizuri kutumia jina halisi la kituo cha mafuta.
Kwa matumizi ya kawaida ya mtaani, watu bado wanatumia "sheli" kama jina la kawaida la vituo vya mafuta, lakini si sahihi .
Pole mkuu kwa huduma mbovu uliyoipata,wahudumu wengi wapo hivyo sababu mishahara yao ni midogo hivyo tegemeo Lao kubwa ni bakshishi! inaelekea na maboss wao wanalijua hili! maana vituo vingi tumewekewa wanawake kutuhudumia.