Kimsingi sipingani na hoja yako.
'In fact' ningefurahi sana kukatokea hata hawa tunaowaona kama misukule sasa hivi, akina Mtungi, akina Kabuti, na wao angalao wakionyesha dalili tu, hata hafifu za kukataa kuwa vikaratasi vya chooni vya kufutia uchafu. Tukianzia hapo, itatuwia rahisi sana kubadili upuuzi huu unaoendelea sasa.
Tuseme, huyo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, siku hiyo, aamuke awe amedhamiria kuwa UZALENDO ni muhimu zaidi ya kitu kingine chochote maishani mwake; na asimame pale mbele; Kama alivyofanya CHEBUKATI wa Kenya, na kutamka ambayo hayakutegemewa na yeyote kwenye sekunde ile ya mwisho; kwamba liwalo na liwe.
Nani ataacha kufurahia uamzi wa aina hiyo siku hiyo! Tendo hilo pekee, litaanzisha mtiririko wa maamuzi hasi dhid yai watawala hata katika vyombo vingine siku hiyo