Hivi walioanzisha utaratibu wa mwanamke kulipiwa mahari walikuwa na sababu gani za msingi?

Nimekupata mtibeli. Ila itakuwa kivumbi na jasho utamaduni huu kupigwa stop
 
Sio vijana wa kibongo ambao wanategemea mwanamke wa mwaka 47 afanane na wa 2000. Wakati wenyewe wakiendelea kubadilika jinsi dunia inavyo badilika
Vijana wenyewe wana badirika ila hawataki iwe kwa mwanamke. Mwanaume akiwa na michepuko sawa haina shida ila mwanaume moto unawaka
 
mi naona mahari ifutwe ili twende sawa na ile 50/50
Unasema tu hata wewe hiyo 50/50 hutaiweza. Mwanamke akijikomboa kiuchumi basi hiyo 50/50 ni rahisi sana kwake.

Na wanawake wengi wamejikomboa na wengine wana mawazo ya kujikomboa ni suala la muda tu.

Sasa wewe upangiwe zamu ya kuosha vyombo kelele utakazopiga nchi jirani watasikia
 
Upigwe stop mara ngapi?

Sheria za nchi hazina kitu kinaitwa Mahari.
Lakini haikatazi Watu kufanya hizo Mila zao ikiwa wanaona haziwadhuru.
Ila ni ngumu kwenye jamii zetu kuoana for free wajomba na mashangazi hawawezi elewa hiyo kitu lazima pachimbike mtibeli
 
Zamu ya kutawadha watoto haaaah lazima kiwake 50/50 ni ngumu kuwezekana
 
Ila ni ngumu kwenye jamii zetu kuoana for free wajomba na mashangazi hawawezi elewa hiyo kitu lazima pachimbike mtibeli

Wanawachimba ninyi mnaoendekeza ujingaujinga na mawazo yasiyo na kichwa na miguu. Sijui laana, sijui baraka, sijui radhi, blah! Blah! Blah! Tuu.

Waambie huwaoi wao, kama mtoto wao anataka kutolewa Mahari na wewe hautaki muache, kwani ni lazima umuoe yeye au aolewe na wewe..
 
mamako aliolewa kwanjia Gani ndugu mtibeli
 
Utaratibu ambao vijana wa sasa mnatakiwa muufute ni wa michango ya harusi.
Mahari ni kama token ya appreciation kwa wazazi kwa kumtunza na kumkuza binti yao halafu huwa hata haimalizwi kama huna unatoa kiasi tu.
Mahari sioni shida yake sababu utazaliwa watoto, watabeba jina lako, watatunzwa, mke atakuhudumia n.k. na pia ni kama inarasimisha nafasi ya mwanaume katika familia sababu anayeolewa ndo analipiwa mahari.
 
Wataelewa tu taratibu ingawa madhara ni makubwa ni mwendo wa kugawana majengo ya serikali. Mmoja mochwari mwingine jela
Ndio maana vifo vya kwenye ndoa vimeongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…