Hivi Wanasayansi wa Nyuklia wa Iran wamekosea Nini kustahili kuuawa na Israel?

Kwa akili yako unazani kuua hao wataalamu itakuwa wamewamaliza na hawatatokea wengine?
 
Nyie jihadists tatizo mnajifanya hamuelewi wakati mnaelewa vizuri sana kwamba sababu ya Iran kutaka kumiliki silaha za nyuklia lengo lake ni kuifuta Israel kwenye ramani ya dunia, kwa hiyo mnategemea Israel iende tu ilale katika mazingira kama hayo. Never.
 
Fikiria tukijiweka kwenye nafasi ya Israel, tuchukulie kwamba Tanzania imezungukwa na nchi jirani zote za Afrika Mashariki ambazo ni maadui zetu. Kila siku unasikia viongozi wao wakitoa kauli za kututishia na kutamani kutuangamiza kabisa. Aisee, hata kama ni mbwa wetu kuguswa tu, lazima tungechukizwa kupita kiasi. Usiombe kiwango hicho cha hofu na ukosefu wa usalama, ambapo kila upande wa ukanda unakuona kama adui.
 
Nchi zote zilizoizunguka Israel kuzitoa Lebanon ni marafiki na wanaisaidia Israel kuwapiga wapalestina.
 
Ni ubabe tu, Israel ana nyukria na hataki kuchunguzwa, kama Iran akisema aue hao wanasansi ya Israel, itakua international outrage kua wameua raia
Anao uwezo huo. Anatupa makombora kama hamas
 
Iran hata asipokua na nuclia akitaka kuifuta Israel kwenye ramani anaitandika tu si umeona kinachotokea. Hili suala la Nuklia ni sababu tu inatafutwa ili kuiangusha utawala wa Iran.
 
Iran alishaweka wazi msimamo wake kuwa akipaatia fursa ataifuta Israel katika uso wa dunia. Chuki ya Irani kwa Israel ni kubwa sana. Hivyo hata hizo silaha za nuclear anazounda, pamoja na malengo mengine, mojawapo ni hiyo ya kuingamiza Israel. Hivyo Israel inachofanya ni kuzuia huo mpango wa Irani dhidi yake usifanikiwe.
 
Elimu inakua transmitted…Ataua ila bado wataendeleq kuzalisha wanasayans wapya as long as iran ina wananchi wake….Hyo Elimu ya Nuclear itafundshwq tu na kua developed.
 
Kauli ya kuifuta Israel imekuja baada ya uonevu wa Israel dhidi ya wapalestina na nchi zote za mashariki ya kati. Israel ana mpango wa " greater Israel" kutawala mashariki ya kati Iran isiposomama itatawaliwa.
 
Nchi zote zilizoizunguka Israel kuzitoa Lebanon ni marafiki na wanaisaidia Israel kuwapiga wapalestina.
Kwa mfano, maandamano makubwa ya umma yaliyofanyika mwezi Oktoba 2023 katika ukanda mzima wa Kiarabu yalihusisha karibu kila nchi ya Kiarabu, zikiwemo hata hizo ulizozitaja. Maandamano hayo yalitokea wakati wa mgogoro kati ya Hamas na Israel. Ingawa uhusiano uliopo kati ya baadhi ya nchi hizo na Israel ni wa kidiplomasia, kwa upande wa itikadi na hisia za wananchi, takriban asilimia 99 ya nchi za Kiarabu zina chuki au upinzani mkali dhidi ya Israel.
 
Kuna shida yeyote Iran kuwasaidia wapalestina wapate Uhuru wa nchi Yao? Nadhani wewe ndio ufanye homework vizuri kujua kwanini wapalestina wananyimwa Haki Yao ya kuwa na taifa huru.
huo mgogoro ni zaidi ya unavofikiria unaongea juu juu sana
 
Elimu inakua transmitted…Ataua ila bado wataendeleq kuzalisha wanasayans wapya as long as iran ina wananchi wake….Hyo Elimu ya Nuclear itafundshwq tu na kua developed.
Hili ni jambo linalochukua muda, kuandaa mwanasayansi mwenye uzoefu na uaminifu wa hali ya juu si kazi ya siku moja. Na kwa wakati huo ambapo Iran inaanza kuwaandaa wataalamu wa aina hiyo, unadhani Israel watakuwa wamelala? Hapo ndipo unapogundua kwa nini operesheni za Israel zimekuwa zikilenga kimkakati kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Iran.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…