Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

hawezi kukuelewa hapa mkuu akili zao zimejaa mashindano wanataka kila kitu tufanye sawa
Wewe unaweza kutafuta pesa na huku unamsaidia mkeo kazi za nyumbani? Kama wewe hauwezi kwanini unataka yeye aweze?
 
Ndio as long as anafanya majukumu yake ya nyumban na ananieshimu kama mume sio alete propaganda zake za usawa kisa na yeye ana earn


Halafu nilichogundua wanawake nyie ni selfish kwahyo mkuu Siku mume akikwama kwa sababu imezoeleka sisi ndo watoaji kama hana huwez msaidia?
Wewe mke wako hata kama anatafuta pesa bado utamhudumia kama kawaida?
 
Watakutenga wenzio hizo akili za kiume 🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️
 
Atakupanda kichwani kama hautimizi jukumu lako kwake mwanaume unatakiwa umhudumie mkeo hata kama ana pesa zake mnapoacha kuwahudumia wake zenu kwa kisingizio cha kuwa kila mtu ana pesa zake hapo ndipo mnapotengeneza usawa wenyewe ni lazima muonyeshe utofauti
 
So ulitakaje ss ikiwa Mungu alishawaumba Wanawake hivyo na kuwathibitishia watazaa kwa uchungu na watatawaliwa na Me daima na tamaa za Ke zitakuwa juu ya Me ilihali sisi Me tuliambiwa tule kwa jasho [emoji848]
Mbona kuna wanaume siku hizi hawali kwa jasho lao wanakula kwa jasho la wake zao hao nao unawaongeleaje?
 
Sawa mkuu nimekuelewa.
 
Africa hatuna huo upumbavu bali yote hayo yameratibiwa na shetani kupitia Mawakala wake ughaibuni, ndiyomaana ss hv pamebakiwa na mvunjiko wa ndoa kwa kila mwaka ni zaidi ya 45%-67% hadi kuunda upya ndoa za mikataba.
Hapo nimeongelea mengi sasa ni upumbavu upi huo unaousemea kati ya hayo niliyoyaongelea? Au unasemea yote?
 
Yes waziri mkuu hawezi kuwa sawa na rais kinafasi na kimajukumu pia na kumbuka rais ndo ana majukumu mengi kuliko waziri mkuu sasa inakuwaje ndoa za leo unakuta mwanamke ndo anafanya majukumu mengi kuliko mwanaume?
 
Hahahaha uko sawa mkuu hatupungukiwi kitu ila kwani na wanaume nao wakitafuta pesa na bado wakasaidia wake zao kazi za nyumbani wanapungukiwa kitu gani?
Utakapoingia maeneo ya kazi utajifunza kitu my dear. Wanawake wachache sana huwa kweli wamafikia hata 75% ya utendaji wa majukumu ya kazi bila msaada huko maofisini.

Pili, wanawake wanavyanzo vingi sana vya kupata pesa sababu wanadhamana ya miili yao katika utafutaji wa pesa. Ndo maaan hata hizi interviews siku hizi ni changamoto sana kwa mtoto wa kiume kupita.

Mwanamke anaweza pata msaada wa kifedha toka kwa baba, mama, kaka, dada, mjomba, bosi, marafiki, workmates na kadhalika ila trust me mwanaume nje ya kipato chake vyanzo vya kupata pesa ni vichache sana...... Na yeye hutoa zaidi.

Kwa kusema hivyo nataka kukujuza kuwa wanaume wanatafuta kwa jasho sana na kwasasa hali ni ngumu inazidi kuwabana wao zaidi kuliko wanawake.

Sasa huyu mtu ambaye anatakiwa kukaa chini kubuni vyanzo vipya vya mapato daily unataka tena akae na kuwaza vyombo havijaoshwa, sijafua nguo, usafi wa nyumba, sijakuna nazi, sijapika.

Aaaaaaah hebu kuwa serious kidogo..... Nadhani upo kinadharia zaidi.

Kimsingi wanaume wanaoa lengo kuu likiwa ni kupata usaidizi wa 100% wa majukumu ya kazi za ndani na mtu wa kumliwaza. Hiyo ya kutafuta pesa ni kiherehere chenu tu maana sidhani mwanaume anae jitambua atakaa kukushurutisha utafute kazi eti ulipie bili zote za nyumba ili hali yeye analala na kuamka na kukunja nne akitizama egoli kwenye tv. Hapo utakuwa umetunga uhalisia na si ukweli wa maisha halisi.....

So kama vipi naomba tuzungumze mambo practical katika jamii yetu na si maigizo.
 
Binadamu tumeshawekewa sheria na amri na Mungu aliyetuumba tuzifuate rejea maandiko usitake kuanza kutolea mifano ya wanyama kwa sababu tu inawafaidisha wanaume hilo siyo lengo la Mungu binadamu na wanyama ni aina mbili tofauti ya viumbe
Kuhusu maandiko mwanaume kaumbwa kutawala , mwanamke kma msaidizi t
Pia ukisem ufuate maandiko bas vitu vingi tumeenda kinyume na maandiko
 
Tangu lini Msaidizi akadai haki sawa ili alingane na Me[emoji848]
 
Mpenzi, hivi umeshawahi jiuliza sehemu kubwa ya bajeti ya mwanamke kimatumizi huwa inaenda wapi?!
Kati ya watu wote walioniuliza maswali kwenye huu uzi wewe ndo umeuliza swali la msingi kuliko yote na ndo swali nililokuwa nalingojea haya ngoja nikujibu

Asilimia kubwa ya bajeti ya mwanamke inaenda kwenye matumizi yake binafsi kwa sababu tumeshaaminishwa kuwa jukumu la kutafuta pesa na kuhudumia familia ni la mwanaume

Na jukumu la kufanya kazi za ndani na kulea familia ni la mwanamke hivyo basi hata ikitokea mwanamke akitafuta pesa hatohudumia familia hiyo pesa itakuwa ya kwake binafsi

Kwa sababu hata kazi za ndani anafanya peke yake wakati mume wake anaweza kumsaidia hivyo tunarudi pale pale kuwa chanzo cha haya yote ni mgawanyo wa majukumu
 
Hivi akatokea kaka jambazi ghafla hapo unadhani nani atacheza nae twist?!

Je, mfano nyumba ni ya kupanga, unadhani nani kodi atalipia?!

Je wadhani asilimia kubwa ya mshahara wa mwanaume huenda wapi?!
Mimi nimemaanisha kwamba wanawake wanaostahili kusaidiwa kazi za nyumbani na waume zao ni wale ambao wanatafuta pesa na pesa zao zinachangia katika maendeleo ya familia na haziishii kwenye matumizi yao binafsi tofauti na hapo basi mke hastahili kusaidiwa majukumu yake na mume wake
 
Ngoja nikalewe Kwanzaa kisha nirudi..[emoji124] [emoji124] kweny huu uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…