Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe mke wako hata kama anatafuta pesa bado utamhudumia kama kawaida?
Watakutenga wenzio hizo akili za kiume 🙆🏽♂️🙆🏽♂️🙆🏽♂️Nahisi nipo nje ya mada kidogo lakini sometimes wanawake tunajichanganya
Tunataka haki sawa kwa wote wakati huo huo tuna ile kauli mbiu yetu eti wanawake tukiwezeshwa tunaweza...SMH!😔😔
Kwanini tuhitaji kuwezeshwa wakati tuko na mikono na miguu miwili mixer ubongo kama wanaume
Atakupanda kichwani kama hautimizi jukumu lako kwake mwanaume unatakiwa umhudumie mkeo hata kama ana pesa zake mnapoacha kuwahudumia wake zenu kwa kisingizio cha kuwa kila mtu ana pesa zake hapo ndipo mnapotengeneza usawa wenyewe ni lazima muonyeshe utofautiKwa mwanamke kufanya kazi si lazima. Naweza kukustopisha na maswali sitaki.
Ila hali za sasa ndio kwa kiasi kikubwa huchangia haya yote.
Wote mna degree, pesa wote mnazo. Yaani automatically kuna ile akili huwaijia kuwa hanibabaishi(mwanamke ni chombo dhaifu). Hata kama haikuwa dhamira yako. Hapo ndipo kiburi huzaliwa na kujikuta unataka umpande.
Wewe unaweza kutafuta pesa na huku unamsaidia mkeo kazi za nyumbani? Kama wewe hauwezi kwanini unataka yeye aweze?
Mbona kuna wanaume siku hizi hawali kwa jasho lao wanakula kwa jasho la wake zao hao nao unawaongeleaje?So ulitakaje ss ikiwa Mungu alishawaumba Wanawake hivyo na kuwathibitishia watazaa kwa uchungu na watatawaliwa na Me daima na tamaa za Ke zitakuwa juu ya Me ilihali sisi Me tuliambiwa tule kwa jasho [emoji848]
Sawa mkuu nimekuelewa.But Edelyn, me sidhani kama hao wanaume wa kuachia mwanamke majukumu wapo wengi kiasi hicho. Na asilimia kubwa wanawake wanaopitia scenario za kulipia gharama za maisha bila msaada wa mwanamke huwa ni wale wanaochagua wanaume wa kuishi nao.
Ni mara chache sana mwanaume atakaye kufuata na kukutaka na kukuomba uwe wake atakutegemea wengi wanakuwa wapo tayari kukuhudumia na hata kama alikuwa hajiwezi ni rahisi sana kwake kuniongeza ili akufurahishe.
Golden rule ni mwanaume akuchague uwe wake, ila naona wadada wengi leo mnachagua wanaume wa kuwa nao az if mnachagua magari na mind you ukichagua mwanaume nakupa guarantee ni mara chache sana atakupambania maana wewe si chaguo lake ila ulikuwa available kwake na wanaume huwa hatuchagui chakula tunakula chochote kinachokatiza na kuzagaa mbele ya macho.
Hapo nimeongelea mengi sasa ni upumbavu upi huo unaousemea kati ya hayo niliyoyaongelea? Au unasemea yote?Africa hatuna huo upumbavu bali yote hayo yameratibiwa na shetani kupitia Mawakala wake ughaibuni, ndiyomaana ss hv pamebakiwa na mvunjiko wa ndoa kwa kila mwaka ni zaidi ya 45%-67% hadi kuunda upya ndoa za mikataba.
Yes waziri mkuu hawezi kuwa sawa na rais kinafasi na kimajukumu pia na kumbuka rais ndo ana majukumu mengi kuliko waziri mkuu sasa inakuwaje ndoa za leo unakuta mwanamke ndo anafanya majukumu mengi kuliko mwanaume?Me huwa nashangaa sana. Sababu hizi kelele zote huwa zinakuja kama watu wanaendekeza mashindano ya kitoto. Katika maisha ya ndoa kuna mambo mengi sana ya muhimu ya kufanya. Ukiona mwanamke unapata muda wa kurumbana na mume wako, na kufanya vituko, hebu jiulize ni nani anasimamia majukumu ya familia yaani household operations.... Na hilo ni jukumu kuu la mama.....
Ni sawa leo waziri mkuu atake kuwa sawa na raisi.... Haiwezekani in practicing ingawa ukiweka kinadharia inakuwa kama kweli.
Utakapoingia maeneo ya kazi utajifunza kitu my dear. Wanawake wachache sana huwa kweli wamafikia hata 75% ya utendaji wa majukumu ya kazi bila msaada huko maofisini.Hahahaha uko sawa mkuu hatupungukiwi kitu ila kwani na wanaume nao wakitafuta pesa na bado wakasaidia wake zao kazi za nyumbani wanapungukiwa kitu gani?
Kuhusu maandiko mwanaume kaumbwa kutawala , mwanamke kma msaidizi tBinadamu tumeshawekewa sheria na amri na Mungu aliyetuumba tuzifuate rejea maandiko usitake kuanza kutolea mifano ya wanyama kwa sababu tu inawafaidisha wanaume hilo siyo lengo la Mungu binadamu na wanyama ni aina mbili tofauti ya viumbe
kwenye pesa kivipi,hebu toa mfanooKwenye suala la pesa mishipa inawatoka hatari, utaitwa kila majina. Ila sio kwenye mambo mengine.
Mapoyoyo[emoji23]Huo ndo ubwege tena hao ndo wanakaa jikoni na wake zao mapoyoyo
Tangu lini Msaidizi akadai haki sawa ili alingane na Me[emoji848]Wanaume wa leo mnataka mpate wanawake wenye akili ya maisha na wanaojua kutafuta pesa ili wawasaidie katika kuhudumia watoto na mahitaji ya nyumbani lakini ninyi hamko tayari kusaidia kufanya kazi za ndani na kulea watoto sasa hapo hamuoni kuwa wanawake ndo wanakuwa wanafanya majukumu mengi kuliko wanaume? Kitu ambacho hakitakiwi maana mwanamke aliumbwa kama msaidizi tu kwa mwanaume
Mapoyoyo[emoji23]
Kati ya watu wote walioniuliza maswali kwenye huu uzi wewe ndo umeuliza swali la msingi kuliko yote na ndo swali nililokuwa nalingojea haya ngoja nikujibuMpenzi, hivi umeshawahi jiuliza sehemu kubwa ya bajeti ya mwanamke kimatumizi huwa inaenda wapi?!
WAKIWA WANAKOJOA WASICHUCHUMAE WASIMAME KAMA SISI WANAUME KAMA WANASHINDANA NA SISI[emoji57]Mnadai isawa wakati huo mnatutegemea tuwawezeshe na kuwahudumia.
Mmekuwa na katabia cha kupenda kushindana. Yaani nikifanya hivi na wewe ufanye vile.
Mimi nimemaanisha kwamba wanawake wanaostahili kusaidiwa kazi za nyumbani na waume zao ni wale ambao wanatafuta pesa na pesa zao zinachangia katika maendeleo ya familia na haziishii kwenye matumizi yao binafsi tofauti na hapo basi mke hastahili kusaidiwa majukumu yake na mume wakeHivi akatokea kaka jambazi ghafla hapo unadhani nani atacheza nae twist?!
Je, mfano nyumba ni ya kupanga, unadhani nani kodi atalipia?!
Je wadhani asilimia kubwa ya mshahara wa mwanaume huenda wapi?!
Na ndiyo huzalisha mitoto mitukutu isiyo na hata chembe chembe za mishipa ya adabuWanawake wanaopenda haki sawa ndo wanaotaka kuwa na wao wanakoroma kwenye familia.
Familia ambayo mwanamke anakoroma hiyo sio familia bora