Hivi wanawake wa dizaini hii kumbe wapo?

Hivi wanawake wa dizaini hii kumbe wapo?

Mwanamke ameajiriwa taasisi binafsi, anaingia saa moja asubuhi anatoka saa kumi na dk 40 jioni, akirudi nyumbani mume anataka apikiwe, mpaka afike kwake ni saa kumi na mbili jioni akirudi apike yaani akae jikoni apike ugali, afue uniform zake, mume aje wale walale.

Mume hana shughuli yoyote anajilimia zake bustani za mboga mboga lakini hashughuliki na chochote cha nyumbani, choo anachotumia had aje adeki mke, chumba anacholala chilia mbali nyumba kuipitisha fagio ni mwiko, nyasi zikiota bibie ajipinde mgongo alime?
Huyo jamaa ana Umwinyi ... anyway kila ndoa ina kanuni zake.
 
Huku mbeya nimeona wengi tu wakifanya hivyo...,even mi nilifanya hivyo ila nilipoona na kutunza familia nimeachiwa tena kwa salary hii hii ya ualimu....nilivyodai talaka na kusepa jumla hakuamini.Mtu anaponyenyekea usimwone boya mtunze
Ila walimu, wengi wenu, sijui kwanini huwa mnapata majanga ya aina hii.

Bado mikopo ya kausha damu walimu ndiyo waathirika wakubwa.
 
mimi binafsi ni mwanamke lakini tungeshindwana mapema sana yan ningechoka wiki tu mume angechagua either tusaidiane kaz za nyumban tuendelee na ndoa au aniache tu niondoke siwez kua mtumwa
Yaani uvunje ndoa kisa kazi za ndani tu ?...huwezi kufikiria kutafuta mfanyakazi ?
 
hivi nyinyi mnaweza? jaribuni siku moja tu muone mziki wake
Hatuwezi kujaribu kufanya hivyo kwasababu ndio maana Kuna mgawanyiko kati ya mwanamke na mwanaume .....
Na ndio maana mwanamke anakojoa huku amechuchumaaa, ili hali mwanaume anakojoa huku akiwa amesimama

Hiyo ndio inaleta utofauti. Zaidi ya hapo inakuwa ni kiburi tu Cha mwanamke kutaka kujilinganisha na mwanaume kitu ambacho kiuhalisia hakipo
 
Kuna watu hawajuagi kujiongeza,huyo mwanaume ilipaswa apige mishe zote za home,labda angemwachia ya kufua ili mwanamke awe anafua wkend
mimi ndio nachojiuliza sawa asbh ukishampeleka mtoto unaenda shamba mchana kutwa kusonga ugali size yake hawez anakaa na njaa had mke arud jioni wapike ugali wale kuna watu wana mioyo ya kuvumilia sana
 
Back
Top Bottom