Hivi wanawake wa dizaini hii kumbe wapo?

Hivi wanawake wa dizaini hii kumbe wapo?

Hatuwezi kujaribu kufanya hivyo kwasababu ndio maana Kuna mgawanyiko kati ya mwanamke na mwanaume .....
Na ndio maana mwanamke anakojoa huku amechuchumaaa, ili hali mwanaume anakojoa huku akiwa amesimama

Hiyo ndio inaleta utofauti. Zaidi ya hapo inakuwa ni kiburi tu Cha mwanamke kutaka kujilinganisha na mwanaume kitu ambacho kiuhalisia hakipo
Majukumu ya mwanaume ni yepi
 
Pole kwa yaliyokukuta lakini nakushauri ukitaka ndoa yako idumu na kama kweli unampenda mwenzio usiangalie madhaifu yake wewe timiza wajibu wako kama mke halafu endelea kumuomba Mungu ili aweze kumbadilisha mke wako kwa kumpa uelewa na kuwa na moyo wa kukusaidia mke wake. Uwe unamuomba Mungu kwa hilo na sio kukimbilia kulalamika
Hivi angekuwa ni mwanamke ndio anafanya hayo madudu ungemuambia mume amuombee mbona nyie ndio mnaongoza kulalamikia madhaifu ya wanawake
 
Mwanamke ameajiriwa taasisi binafsi, anaingia saa moja asubuhi anatoka saa kumi na dk 40 jioni, akirudi nyumbani mume anataka apikiwe, mpaka afike kwake ni saa kumi na mbili jioni akirudi apike yaani akae jikoni apike ugali, afue uniform zake, mume aje wale walale.

Mume hana shughuli yoyote anajilimia zake bustani za mboga mboga lakini hashughuliki na chochote cha nyumbani, choo anachotumia hadi aje adeki mke, chumba anacholala achilia mbali nyumba kuipitisha fagio ni mwiko, nyasi zikiota bibie ajipinde mgongo alime?
Tuambie kama ni wewe tuje tukupe mauwa yako
 
Huku mbeya nimeona wengi tu wakifanya hivyo...,even mi nilifanya hivyo ila nilipoona na kutunza familia nimeachiwa tena kwa salary hii hii ya ualimu....nilivyodai talaka na kusepa jumla hakuamini.Mtu anaponyenyekea usimwone boya mtunze
Kama ni kweli usemayo itabidi nije mbeya kufanya utalii wa ndani je nakaribishwa?
 
Nimeona clip ya wanawake wa US, Canada, Uk wanatafuta waume wa kuwaoa, na wako tayari kuwatumia Visa, nauli; ningekuwa singo ningechangamkia fursa.

Wanaume halisi tumebaki wachache​
 
Ndoa za Wapumbavu hilo ni kawaida,
Kwanini mwanamke afanye kazi tena ya kutoka saa 12 jion? Huyu mwanaume anakazi gani? Yeye ndiye alipaswa kua kazini huku mkewe akishughulikia maswala yote ya nyumbani kutwa nzima.
 
Mwanamke ameajiriwa taasisi binafsi, anaingia saa moja asubuhi anatoka saa kumi na dk 40 jioni, akirudi nyumbani mume anataka apikiwe, mpaka afike kwake ni saa kumi na mbili jioni akirudi apike yaani akae jikoni apike ugali, afue uniform zake, mume aje wale walale.

Mume hana shughuli yoyote anajilimia zake bustani za mboga mboga lakini hashughuliki na chochote cha nyumbani, choo anachotumia hadi aje adeki mke, chumba anacholala achilia mbali nyumba kuipitisha fagio ni mwiko, nyasi zikiota bibie ajipinde mgongo alime?
analipia mahari iliyotolewa.
 
Hao wanawake jina lao maarufu ni walezi wa wana
 
Back
Top Bottom