May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kwa siku za karibuni kwenye mitandao mbali mbali kumeshamiri maombi ya kuhitaji Wenza...natamani kujua kama kuna utafiti umefanyika kujua mafanikio ya mfumo huu.
Maombi haya yamekuwa yakiambatishwa na vigezo lukuki huku vingi ya hivyo ni ngumu hata kupatikana kwa Mtu mmoja.
Pia kinachochanganya zaidi ni pale unapokuta eti hata binti wa mika 21, 22, mpaka 25 kukuta nae anatafuta Mchumba au Mwenza wa kuishi nae mtandaoni.
Sikatai kwamba wapo wanaofanikisha matakwa yao lakini pia wapo wengi wanaokwama kutokana na kutoka kabisa kwenye uhalisia na kubaki tu kama Wacheza kamari.
Kwa vyoyote ni ngumu kwa Mtu kumkubali Mtu kwa kusoma tu maelezo yake mtandaoni...sidhani kama yeye kwa kuandika tu anahitaji Mwenza Mcha Mungu basi Msomaji ajiridhishe kuwa Muombaji ni Mcha Mungu.
Nadhani kunahitajika namna nyingine zaidi ya kutafuta Wenza zaidi ya hii ya mitandaoni, yaani hata kama itaanzaia mtandaoni basi kwa kipindi maalumu Waombaji na Wahitaji wakae chini ya uangalizi wa Wajuzi wa mambo kabla hata ya kukutana.
Na baada ya hicho kipindi wote watakuwa na nafasi ya kupitia matokeo (results) ya aina ya Waombaji na Wahitaji wao...bila shaka kwa njia hii itakuwa ni rahisi zaidi kwa Mtu kuchagua Mtu mwenye kuendana nae badala ya Mtu kulazimika kwenda kwa asiyemju kabisa.