Hivi wapo wanaofanikiwa kupata wenza makini (serious) mitandaoni?

Hivi wapo wanaofanikiwa kupata wenza makini (serious) mitandaoni?

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kwa siku za karibuni kwenye mitandao mbali mbali kumeshamiri maombi ya kuhitaji Wenza...natamani kujua kama kuna utafiti umefanyika kujua mafanikio ya mfumo huu.

Maombi haya yamekuwa yakiambatishwa na vigezo lukuki huku vingi ya hivyo ni ngumu hata kupatikana kwa Mtu mmoja.

Pia kinachochanganya zaidi ni pale unapokuta eti hata binti wa mika 21, 22, mpaka 25 kukuta nae anatafuta Mchumba au Mwenza wa kuishi nae mtandaoni.

Sikatai kwamba wapo wanaofanikisha matakwa yao lakini pia wapo wengi wanaokwama kutokana na kutoka kabisa kwenye uhalisia na kubaki tu kama Wacheza kamari.

Kwa vyoyote ni ngumu kwa Mtu kumkubali Mtu kwa kusoma tu maelezo yake mtandaoni...sidhani kama yeye kwa kuandika tu anahitaji Mwenza Mcha Mungu basi Msomaji ajiridhishe kuwa Muombaji ni Mcha Mungu.

Nadhani kunahitajika namna nyingine zaidi ya kutafuta Wenza zaidi ya hii ya mitandaoni, yaani hata kama itaanzaia mtandaoni basi kwa kipindi maalumu Waombaji na Wahitaji wakae chini ya uangalizi wa Wajuzi wa mambo kabla hata ya kukutana.

Na baada ya hicho kipindi wote watakuwa na nafasi ya kupitia matokeo (results) ya aina ya Waombaji na Wahitaji wao...bila shaka kwa njia hii itakuwa ni rahisi zaidi kwa Mtu kuchagua Mtu mwenye kuendana nae badala ya Mtu kulazimika kwenda kwa asiyemju kabisa.
 
Kwa siku za karibuni kwenye mitandao mbali mbali kumeshamiri maombi ya kuhitaji Wenza...natamani kujua kama kuna utafiti umefanyika kujua mafanikio ya mfumo huu.
Eb wenye uzoefu wajibu tuone
 
Yes wapoo.

Kuna mtumishi aliwaanzishia vijana wa dhehebu lake group la wachumba WhatsApp,na wameshatoa couples zaidi ya 6 now.

Ishu ya mahusiano haina formula ndugu,ni vile wewe umejipambanua mbele ya jamii,hakika utapata wakufanana nae.

Muhimu,muombe MUNGU akusimamie katika kufanya maamuzi yako.
 
Kumbeee
 
Hoja yangu hapa ni je wanapata muda wa kufahamiana kabla ya kila mmoja kumruhusu Mwenzake kuwa nae miaka 40 au zaidi aliyobakiza?.

Maana hii mitandao imeleta mfumo mpya wa Mtu kujidadi mwenyewe.
 
Hoja yangu hapa ni je wanapata muda wa kufahamiana kabla ya kila mmoja kumruhusu Mwenzake kuwa nae miaka 40 au zaidi aliyobakiza?.

Maana hii mitandao imeleta mfumo mpya wa Mtu kujidadi mwenyewe.
Ni kama unavyoonana na mtu kwa mara ya kwanza kanisani/msikitini/supermarket/mwendokasi humjui hakujui likewise mtandaoni mtachat then mtapeana no na mambo mengine ya kufahamiana zaid yanafata.

Tofauti ni mmoja mmeonana live na huyu mmekutana mtandaoni umeona labda picha ikakuvutia.

Maana hata huyo unayeonana nae live sio kama utamuona leo then kesho unatangaza ndoa, lazima mtachunguzana mkiona mnamatch then chereko chereko zinafata.
 
Mbona mara kibao..

Mara nyingi watu hushindaa kazini na jioni uchovu mwingi so unaenda straight home..Hivyo unaona isiwe tabu utafute marafiki au mpnz mtandaono mpeane company.

Anyway, wa mitandaoni ndo hawa hawa wa mtaani sema muda wa kujuana ndo shida.
 
Karibu kila mwezi thread ya namna hii inaanzishwa Jf, hata wenye kutoa majibu nadhani wamechoka sasa
 
😂😂😂😂😂😂 Hata Nusu sijafika 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Duh..basi ngoja nitulie atakuja. Jamani eeeeee am so serious kwenye hilo suala. Aliye-qualify aje PM. Nitahakiki umri aje na kitambulisho cha NIDA
 
Duh..basi ngoja nitulie atakuja. Jamani eeeeee am so serious kwenye hilo suala. Aliye-qualify aje PM. Nitahakiki umri aje na kitambulisho cha NIDA
Unataka umfanye nini mbaba wa watu[emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom