Hivi wataalam wa kilimo toka SUA wana impact gani! Mbona hawasikiki?

Food Science and Nutrition wanacho kinaitwa FONATA
 
Chaa ajabu wengi unawakuta wanafanya kaZi bank!! Ushahidi ninao
Sasa kama hujawajengea mzingira mazuri katika sekta yao wafanye nn!? Na ukizingatia wanauwezo wa kufanya hizo kazi nyinginezo kuliko waliozisomea kama kozi mama.
 
....Kitu ambacho nimejifunza kwa vijana wa kizazi hiki, hawapendi masomo ya sayansi, achilia mbali hao waliosomea kilimo kukipenda na kukiendeleza wakitoka chuoni kama SUA, au hata hao wanaobaki kufundisha. Huku makazini unakuta graduate wa kilimo au mifugo halimi wala hafugi, sasa atamsaidiaje mkulima?
 
SIASA imetelekeza kilimo.unafikiri wasomi watafanya nini?ifutwe udsm maana ndo imewaleta kina CHENGE,MWAKYEMBE,MUHONGO,TULIA,MAGU, wanafiki tuu hawana nia njema na hii nchi
Ahahaaah..... Una hasira sana mkuu
 
we unataka amiliki nini??
Kiwanda cha kutengeneza tomato sauce maana kila mwaka nyanya zinaozea mashambani! Pia sio vibaya akamiliki mashamba ya mfano na sisi ambao hatukubahatika kusoma tujifunze kwake!
 
Ukitaka mtu aliesomea kilimo mwenye impact tafuta mtu aliesomea vyuo vya kati hasa mwenye diploma alieanzia certificate
Fani ya Sayansi katika ngazi ya Certificate and diploma wapo vizuri sana ukilinganisha na ngazi ya degree, kwa sababu awa wamekaa sana katika field work na wanajua matatizo na changamoto zote
 
Chuo ni UD tu
 
Kiwanda cha kutengeneza tomato sauce maana kila mwaka nyanya zinaozea mashambani! Pia sio vibaya akamiliki mashamba ya mfano na sisi ambao hatukubahatika kusoma tujifunze kwake!
Kuna factor nyingi sana za kuangalia kabla hujamiliki hicho kiwanda cha kuchakata mazao. Huwezi tu kuanzisha kiwanda kisa nyanya zinaozea shambani mkuu, je kuna supply ya kutosha mwaka mzima? Sasa hivi nyanya moja ni 200/-
Kuna masoko ya uhakika?
Kuna mazingira rafiki ya kuanzisha viwanda kwa wanaomaliza vyuo?
Kuna Umeme wa uhakika?
 
Chaa ajabu wengi unawakuta wanafanya kaZi bank!! Ushahidi ninao
SUA wana kozi za uchumi pia, agricultural economics and agribusiness. Mabenki kama CRDB au NMB wana mikopo ya kilimo kwa wateja wao na watu hawa wanafaa kwa kazi hizo kwa hiyo usishangae sana mkuu.
 
Mtoa mada hana ufahamu kabisa kuhusu SUA na kilimo kwa ujumla.
-ukiugua unatafuta tiba kwa haraka sana , lini ulitafuta msaada wa kitaalamu kwa afisa kilimo ukakosa. Afisa kilimo ni mtoa ushauri hivyo hana nguvu ya kulazimisha ushauri wake kufuatwa ukizingatia gharama za technology _ kuingiliana kwa siasa na utaalamu ni tatizo _ na mengine mengi nitafute nikujuze hivi hakuna mkulima anaeweza kujua kwamba nikiwa namimea mingi shambani nitavuna mavuno mengi ? Kwa nini anapanda ovyo (mchafukuoga)
 


hivi ndo mnavofikili kisiasa kuhusu kilimo kwa kuwalaumu wataalamu wa kilimo bila kutafuta nini kinakwamisha hili tatizo,
moja ya sababu kuu ni SERA za kipumbavu zinazotungwa na wanasiasa wasiokuwa na elimu pamoja na uchungu juu ya kilimo.

serikali yako inapanga bajeti ya kilimo na kuipa pesa kidogo halafu bado hyo asilimia ndogo iliyotekelezeka ni 30 asilimia tu, then mwaka wa fedha ujao tena itapitisha bajeti ya uongo na kweli.

mkuu, kumbuka kilimo ni kazi ambayo inaambatana na utafiti wa kila leo ili kuendana na dunia, leo hii viwavi jeshi(armyworm) vinaibuka na kushambulia maeneo mengi na mikoa mingi lakini wizara inatoa macho tu haijui ifanyeje.

KILIMO,UFUGAJI NA UVUVI utake usitake lazima pesa itumike kwenye utafiti ili tuweze kufikia malengo....
 
Fani ya Sayansi katika ngazi ya Certificate and diploma wapo vizuri sana ukilinganisha na ngazi ya degree, kwa sababu awa wamekaa sana katika field work na wanajua matatizo na changamoto zote
Sasa hao technologies za kupeleka kwa wakulima wanazipata wapi kwa kuwa wao hawana uwezo wa kuzidevelop na kwanza sio kazi yao. That's where SUA and other research stations come in. SUA wana-develop technologies na kuzipeleka kwa wakulima through On farm Research. Link kati ya SUA na wakulima ni hao Field Officers kama Village Extension Officers ambao wanahusishwa kwenye On farm Research. Mkuu VEO wapo kwa kuwa SUA and other Research entities kama Agriculture Research Institutes zipo, otherwise they would cease to exisist .
 

siasa mbaya sana, eti serikali inashindwa hata kuweka green house 2 kila halmashauri , mabwawa ya samaki na mashamba ya kuku kwa ajili ya kufundishia wananchi na kuwa kama sehemu ya mapato inakalia porojo za kisiasa na kukomoana na
upinzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…