What i can say ni kwamba wakulima wa kitanzania hawataki kibadilika ndio maana kilimo hakisongi ,ukifanya utafiti wakulima wamefundishwa sana na taasisi za binafsi na za kiserikali but ukipima impact ya mafunzo ni zero sababu mtu amachofundishwa sicho anachokifanya ,na hapo ndipo anaepima kilimo kama mtoa mada kwa impact huoni kama kuna kilichofanyika . First ni watanzania tujifunze kubadilika na kupokea elimu ndipo kilimo kitasonga.
Huwezi amini mpaka leo hii wenzetu wanatoka kwenye hybrid wanaenda kwenye G.M.O (siungi mkono lakini gmo) ila sisi bado tunatumia mbegu za kichanjani,bado tunakamua mbegu kwenye mazao ya shambani na kuzipanda tena . Kila mtu angekua kwenye hybrid ungeona impact ,kila mtu angejua anatoa nn shambani ungeona impact. Ila mtanzania anatumia milioni 2 kuzalisha zao akivuna anauza milioni 1 na anajisifia amepata faida ,inasikitisha sana kwa sisi ambao tuko field na tunaona hali ilivyo na hakika binafsi ndio inanipa morali ya kuongeza bidii kubadili mindset za farmers