Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Wakuu, jana nilikuwa sehemu maarufu kwa nyama choma ya mbuzi. Watu huwa ni wengi kiasi kwamba wengine husafiri zaidi ya kilomita 100 kwenda kula mbuzi choma, hasa weekend! 😂🐐
Nikiwa nimekaa na jamaa zangu, mara nikawaona vijana wakipita meza hadi meza kukusanya mifupa iliyobaki baada ya wateja kula. Cha ajabu, walikuwa wanaikusanya kwa umakini mkubwa sana, wakiwa na vyombo vilivyozungushiwa foili! 😂
Jamaa yangu akamuuliza yule dogo aliyekuja kukusanya mifupa kwenye meza tuliokaa
"Dogo, hii mifupa mnapeleka wapi?
Akajibu, huwa tunapikia chakula cha mbwa." Dogo akaondoka zake chap.
Baada ya kuondoka, jamaa yangu mwingine akasema kuwa amewahi kushuhudia maeneo fulani ya Pwani ya Kusini mifupa hiyo ikichambuliwa, minofu iliyobaki ikachanganywa, utumbo nyama nyingine na kutengeneza supu ya mbuzi inayouzwa kwa watu! 😭😂
Wakuu, nilijiuliza sana:
Je, inawezekana mtu akaenda kunywa supu kwa furaha, kumbe nyama iliyotumika imetokana na mabaki ya chakula yaliyokusanywa kwenye sahani za wateja wengine?
Kama kweli kuna wanaofanya hivyo, hii si biashara tena, ni kuhatarisha afya za watu kwa ajili ya faida!
Ndugu zangu wauza nyama choma na supu ya mbuzi, tunatambua umuhimu wa kutafuta kipato, lakini msiweke faida mbele ya afya za wateja. Mabaki kutoka kwenye sahani za wateja yanaweza kuchafuliwa na vijidudu, na kuyachemsha tena hakuhakikishi usalama wake.
Hata hivyo, sina ushahidi kwamba wauza nyama katika eneo nililotembelea wanafanya hivyo, na sina haki ya kuwatuhumu wote bila uchunguzi.