Hivi wauza nyama choma mbuzi na supu ya mbuzi huwa mnafanya haya mambo ? 😂😭

Hivi wauza nyama choma mbuzi na supu ya mbuzi huwa mnafanya haya mambo ? 😂😭

Nisawa tu sababu hata kwa mamantilie kuko hivyo.
Niliwahi agiza wali mboga wa buku jero, ukaja ulikuwa wali wa maharage, na mboga za majani.

Ile natafuna nashangaa kuna mifupa ya samaki mdomoni mara mifupa midogo midogo ya nyama sasa nikajiuliza hii imekaaje nikadhani labda walikosea wakanichanganiyia samaki ya mteja mwingine wakati wa kutoa wakasahahu kucheki mifupa ila hiyo iliwahi tokea mara kadhaa Nilikuja kugundua baadae kumbe ule wali unaoagizwa na wateja waliokula wali samaki wakabakiza au wali nyama unarudishwa kwenye sufuria bila hata kuchambuliwa unachemsgwa tu asubui au mchana mteja mwingine unakumbana nao, chunguzeni vyakula vya migahawa bubu muone hata radha ni mbovu mpaka leo siri kwa mamantilie naenda town nikikosa muda naagiza chipsi au nashinda njaa mpaka kitambi kimeisha
Dah! Ila watu katika dinia hii wanatafuta pesa kwa namna ya kijinga sana.
 
Moja ya mambo yanayochangia watu kukosa furaha ni kutaka kujua mambo ambayo hawapaswi kuyajua.

Wagogo tunasema Curiosity killed the cat.
Wandengereko wa kule ndanu ndani nao wakasema ukichunguza sana anachokula bata hutokula nyama yake.(Sijui kama nimepatia)
 
Wakuu, jana nilikuwa sehemu maarufu kwa nyama choma ya mbuzi. Watu huwa ni wengi kiasi kwamba wengine husafiri zaidi ya kilomita 100 kwenda kula mbuzi choma, hasa weekend! 😂🐐

Nikiwa nimekaa na jamaa zangu, mara nikawaona vijana wakipita meza hadi meza kukusanya mifupa iliyobaki baada ya wateja kula. Cha ajabu, walikuwa wanaikusanya kwa umakini mkubwa sana, wakiwa na vyombo vilivyozungushiwa foili! 😂

Jamaa yangu akamuuliza yule dogo aliyekuja kukusanya mifupa kwenye meza tuliokaa

"Dogo, hii mifupa mnapeleka wapi?

Akajibu, huwa tunapikia chakula cha mbwa." Dogo akaondoka zake chap.

Baada ya kuondoka, jamaa yangu mwingine akasema kuwa amewahi kushuhudia maeneo fulani ya Pwani ya Kusini mifupa hiyo ikichambuliwa, minofu iliyobaki ikachanganywa, utumbo nyama nyingine na kutengeneza supu ya mbuzi inayouzwa kwa watu! 😭😂

Wakuu, nilijiuliza sana:

Je, inawezekana mtu akaenda kunywa supu kwa furaha, kumbe nyama iliyotumika imetokana na mabaki ya chakula yaliyokusanywa kwenye sahani za wateja wengine?

Kama kweli kuna wanaofanya hivyo, hii si biashara tena, ni kuhatarisha afya za watu kwa ajili ya faida!

Ndugu zangu wauza nyama choma na supu ya mbuzi, tunatambua umuhimu wa kutafuta kipato, lakini msiweke faida mbele ya afya za wateja. Mabaki kutoka kwenye sahani za wateja yanaweza kuchafuliwa na vijidudu, na kuyachemsha tena hakuhakikishi usalama wake.

Hata hivyo, sina ushahidi kwamba wauza nyama katika eneo nililotembelea wanafanya hivyo, na sina haki ya kuwatuhumu wote bila uchunguzi.
Ikishachemshwa tunakula ilimuradi hatuumwi.
 
Kaka msosi kula nyumbani, mtaani kubali tu kula uchafu.
 
Kama huna hela acha kabisa kula nyama za barabarani, wali maharage na mchicha mbona msosi mzuri sana na bei rahisi.
Supu au wali nyama kuku kula hoteli ya maana.
 
Siku za nyuma Migahawa ya Kariakoo walikuwa wanauza wali wa jana.
Lakini walikuwa wanachagua wateja wa kuwauzia.
Wakiona una kaushamba furani weita, ataagiza chakula jikoni kwa kusema "Wali jaa mchuzi moto"
Au ataagiza "Wali ng'ombe" kwa maana wewe ndiye ng'ombe😂.
Tabia hiyo sasa haipo tena.
Kwa kifupi migahawani kuna siri nyingi tusizozijua
 
Back
Top Bottom