Hivi wazazi mnaoleaga hivi watoto huwa mnajielewa kweli?

Hivi wazazi mnaoleaga hivi watoto huwa mnajielewa kweli?

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,994
Reaction score
4,446
Katika pita pita zangu nimekutana na watoto acha niwaite tu "broiler"

Wana tabia za ajabu sana ila kilichonishtua ni kuona wazazi wao wanachukulia normal sana hawashutuki wala hawajali juu ya tabia za ajabu ajabu walizo nazo watoto wao.

Nimeshangaa rafiki yangu kanialika chakula cha usiku lakini vituko anavyovifanya mtoto wake nimebaki nimeshangaa sana ila sasa wazazi wake wako comfortable kabisa. 😂

Just imagine mtoto anakuja anakwapua kijiko cha mgeni Kisha wazazi wanamuagiza Binti wa kazi akalete tena kijiko kingine 🙄.
Mara mtoto anamshika mama yake mkono asile , mara amwage chakula ,mara achukue sahani ya chakula ajitwishe kichwani aanze kuzunguka sebleni na wazazi wake wala hawamfanyi chochote wanamuangilia tu hawamkanyi wanaendelea kumbembeleza aje kula😂.

Mtoto anaamka usiku kama saa kumi hivi anaamrisha apewe simu acheze game na kuangalia cartoon na wazazi wake wanatii. Alafu cha kusikitisha zaidi hyo mtoto ni wa kiume first born miaka kama mitatu hivi.

Mimi ninachojua umri sahihi wa kumjenga mtoto mwenye adabu ni kuanzia mwaka 0-5 ukishindwa kutengeneza msingi wa tabia njema kwa mtoto wako katika kipindi hiki ni dhahiri mtoto atakusumbua wewe, jamii yako na taifa kwa ujumla.
 
Akikua ataacha mkuu..bado mtoto so acha wavumilie huo utoto wake
Wazazi malezi ya kikamanda hawayawezi.kikubwa utulivu basi.
Though wengi wanaolelewa hivyo huwa na tabia Fulani zenye kukera,ila Dunia inawanyoosha wananyooka.

Kuna watoto nlikua nao walijengwa zaidi kitabia na dada Yao wa kazi.mama Hana muda labda weekends
Lakini alivyoondoka bado haikutosha.mama alibaki na malezi zero.
Binti wa miaka 12 anafokeana na Mzee wa miaka 70.
Nenda huku sitaki,usifanye hiki Fanya kile sitaki.
Anawakuta mnaangalia tv anawafurusha wote anakwapua remote aangalie anachotaka.ukimuuliza kwanini anajibu sababu mama angu ndio alielipia kingamuzi allivyokuja alikuta kimekata(ubinfsi kwaao na Kwa watu wengine)
Mtoto wa miaka 8 akiamka anatafutwa fagio afagie anaona kabisa usiku tuliacha uchafu sebuleni.ila wa miaka 13-15 akiamka anawasha tv anangalia tamthilia.hajui kufagia,kupika chai,kuosha vyombo.hajui kupika chochote.
 
Katika pita pita zangu nimekutana na watoto acha niwaite tu "broiler"

Wana tabia za ajabu sana ila kilichonishtua ni kuona wazazi wao wanachukulia normal sana hawashutuki wala hawajali juu ya tabia za ajabu ajabu walizo nazo watoto wao.

Nimeshangaa rafiki yangu kanialika chakula cha usiku lakini vituko anavyovifanya mtoto wake nimebaki nimeshangaa sana ila sasa wazazi wake wako comfortable kabisa. 😂

Just imagine mtoto anakuja anakwapua kijiko cha mgeni Kisha wazazi wanamuagiza Binti wa kazi akalete tena kijiko kingine 🙄.
Mara mtoto anamshika mama yake mkono asile , mara amwage chakula ,mara achukue sahani ya chakula ajitwishe kichwani aanze kuzunguka sebleni na wazazi wake wala hawamfanyi chochote wanamuangilia tu hawamkanyi wanaendelea kumbembeleza aje kula😂.

Mtoto anaamka usiku kama saa kumi hivi anaamrisha apewe simu acheze game na kuangalia cartoon na wazazi wake wanatii. Alafu cha kusikitisha zaidi hyo mtoto ni wa kiume first born miaka kama mitatu hivi.

Mimi ninachojua umri sahihi wa kumjenga mtoto mwenye adabu ni kuanzia mwaka 0-5 ukishindwa kutengeneza msingi wa tabia njema kwa mtoto wako katika kipindi hiki ni dhahiri mtoto atakusumbua wewe, jamii yako na taifa kwa ujumla.
Wazazi wa kisasa wanakwambia hawataki watoto wao wapitie 'shida' walizopitia wao.
 
Mimi hapo nisingekaa aisee
Mimi napenda watoto sanaa

Ila upuuzi na upumbavu sipendi kabisa mtoto kosa analifanya day 1 una mchekea anaona aah kumbe ni kawaida

Na ujue watoto wana akili anafanya kitu then anakuangalia uta react vipi

Tabia ya mtoto wa umri mdogo ni malezi mabaya maana huyu huwezi kusema kafundishwa tabia mbaya na makundi
 
Ndiomaana sitakagi kukaa na mtoto wa mtu nitaonekana namtesa! Juzi nmekaanga zangu samaki nikawaweka ndani, mtoto wa rafikiangu mdogo tu miaka mi5 wakike kaingia jikoni kakata samaki kabugia, nilimtandika fimbo mama yake kaja kamkuta ana alama ya fimbo kaishiwa raha kabisa! Yani nikishamwambia kama unamuacha mtoto hapa ukitoka kazini lazima ukute nimemnyoosha tu, siwezi kulea upumbavu mimi!
Usimpige kwa nguvu sana shetani hachelewi kujipenyeza
 
Utasikia jamani alivunja simu yangu na tv ukutani Junior ana manguvu kama ya Babake. Pumbaffffff wa kwangu wamezaliwa na kukulia Ulaya na hawavunji simu wala TV.Hakuna upumbavu nisiopenda kusikia kama simu alivunja mtoto.
Kwanza hiyo simu, mtoto anapewa ya nini?

Nikikuta mwanangu anachezea simu kizembe hiyo ni vita ya tatu ya dunia.

Na hiyo vita inamuhusu alietoa simu kumpa mtoto, na pia mtoto mwenyewe.
 
Sasa ndio uwaite "Broiler"?
Kama ni miaka mitatu, hao wazazi wapo sahihi. 😊
Watu wamezoea mikwaju kama ng’ombe mtoto akae kama yuko polisi
Siafiki mtoto asiadhibiwe ila tupunguze umwinyi jamani ndo maana tuna kizazi cha uoga sana,
Watu hata haki zao wanashindwa kudai sababu wamejengewa nidhamu za uoga tangia utoto!
 
kuna mwingine kamwaga maandazi ya mtu kwenye deli afu nikasikia ni mtoto mwache nilitamani nimnyanyue nimtie mtaroni nimtoe, mwingine kajimwagia supu ya moto hataki, anataka chips

ntamtia fimbo mpaka akumbuke maharage ni mboga na mchicha ni zao la kibiashara
 
Watu wamezoea mikwaju kama ng’ombe mtoto akae kama yuko polisi
Siafiki mtoto asiadhibiwe ila tupunguze umwinyi jamani ndo maana tuna kizazi cha uoga sana,
Watu hata haki zao wanashindwa kudai sababu wamejengewa nidhamu za uoga tangia utoto!

Ni mtazamo wa mtoa mada; simpingi lakini, sukubaliani nae kwa mtoto wa miaka mitatu. Alipokwapuliwa kijiko, alitaka Junior apigwe kitasa, sasa Junior angechukua soda yake ndo pangewaka. 😊
 
Back
Top Bottom