Hivi wazazi mnaoleaga hivi watoto huwa mnajielewa kweli?

Hivi wazazi mnaoleaga hivi watoto huwa mnajielewa kweli?

Ni mtazamo wa mtoa mada; simpingi lakini, sukubaliani nae kwa mtoto wa miaka mitatu. Alipokwapuliwa kijiko, alitaka Junior apigwe kitasa, sasa Junior angechukua soda yake ndo pangewaka. 😊
Kwa mtoto wa umri huo ukisema kila kosa unapiga mbona utatoka sugu za mikono 🤣🤣🤣
Maana yeye ndani ya dk 5 kasahau anafanya tukio lingine!
 
Ndiomaana sitakagi kukaa na mtoto wa mtu nitaonekana namtesa! Juzi nmekaanga zangu samaki nikawaweka ndani, mtoto wa rafikiangu mdogo tu miaka mi5 wakike kaingia jikoni kakata samaki kabugia, nilimtandika fimbo mama yake kaja kamkuta ana alama ya fimbo kaishiwa raha kabisa! Yani nikishamwambia kama unamuacha mtoto hapa ukitoka kazini lazima ukute nimemnyoosha tu, siwezi kulea upumbavu mimi!
Hyo mama hajaku report kwa Dorothy gwajima😂😂
 
Usimpige kwa nguvu sana shetani hachelewi kujipenyeza
Hata simpigagi lakini namuona anajisahau sana akikaa muda mrefu hajatembezewa kidogo! Kuna siku nimempeleka training ya swimming acha asimame ajikojolee mbele za watu! Wakati anajua kusema tukiwa nyumbani! Huwa wanapima hawa mpaka uwe una mbust kidogo!
 
kuna mwingine kamwaga maandazi ya mtu kwenye deli afu nikasikia ni mtoto mwache nilitamani nimnyanyue nimtie mtaroni nimtoe, mwingine kajimwagia supu ya moto hataki, anataka chips

ntamtia fimbo mpaka akumbuke maharage ni mboga na mchicha ni zao la kibiashara
Mtoto anaemwaga chakula kusudi.

Mwambie wazi hata kama ni mdogo kumwaga chakula ni kosa kubwa sana.

Halafu mnyime chakula mpaka njaa Imkamate kisawa sawa, halafu mpe chakula asichokipenda akile.
 
Hata simpigagi lakini namuona anajisahau sana akikaa muda mrefu hajatembezewa kidogo! Kuna siku nimempeleka training ya swimming acha asimame ajikojolee mbele za watu! Wakati anajua kusema tukiwa nyumbani! Huwa wanapima hawa mpaka uwe una mbust kidogo!
Naunga mkono imagine ajikojolee mbele za watu na kusema anaweza
Ila watoto bhna kweli wana tabia ya kutupima
 
Watu wamezoea mikwaju kama ng’ombe mtoto akae kama yuko polisi
Siafiki mtoto asiadhibiwe ila tupunguze umwinyi jamani ndo maana tuna kizazi cha uoga sana,
Watu hata haki zao wanashindwa kudai sababu wamejengewa nidhamu za uoga tangia utoto!
Mtoto lazima akatazwe hata kama ni mdogo wanasikia sana! Anakudhalilisha mbele ya wageni mtoto anamyang’anya mgeni kijiko unamuangalia tu badala umkataze! Ukimkataza anajifunza taratibu anajua hiki kizuri hiki kibaya! Ukianguka hapo unaachia watu mzigo kwa malezi ya kijinga hayo, niamke saa 8 kukuwekea katuni kwenye simu😅 Siwezi!!
 
Mtoto anaemwaga chakula kusudi.

Mwambie wazi hata kama ni mdogo kumwaga chakula ni kosa kubwa sana.

Halafu mnyime chakula mpaka njaa Imkamate kisawa sawa, halafu mpe chakula asichokipenda akile.
wapo wengi mkuu, nakususa wanasusa afu mtu anamchekelea mtoto kama huyo ataweza kuishi na waty wengine kweli?

au kaharibu kitu cha mtu kwa kisingizio cha ni mtoto?
 
Kwa mtoto wa umri huo ukisema kila kosa unapiga mbona utatoka sugu za mikono 🤣🤣🤣
Maana yeye ndani ya dk 5 kasahau anafanya tukio lingine!
Sio kwamba lazma umpige zaman ilikuwa ukifanya kosa baba akaseme lazma uchutame mama akikukata jicho lazma ujue kuwa hapa umelikoroga
Lkn wazazi wa kizazi Cha broiler mtoto anafanya makosa yanajirudia mfulurizo wao wapo wanachekelea tu

We unaona hyo n sawa?
 
Mtoto lazima akatazwe hata kama ni mdogo wanasikia sana! Anakudhalilisha mbele ya wageni mtoto anamyang’anya mgeni kijiko unamuangalia tu badala umkataze! Ukimkataza anajifunza taratibu anajua hiki kizuri hiki kibaya! Ukianguka hapo unaachia watu mzigo kwa malezi ya kijinga hayo, niamke saa 8 kukuwekea katuni kwenye simu😅 Siwezi!!
Yes mtoto ni lazima akanywe sijakataa, ila hemu pitia comments za waja humu ujionee akili zao
Mtu anakazana ningepia hadi nifukuzwe 🤣🤣🤣 adhabu sio fimbo tu jamani.
Fimbo iwe ni adhabu ya mwisho kabisaaa hata mtoto mwenyewe aone kweli leo nimeyatimba!
 
Ungekakata hata mtama bwana kwani kanakufa🤣
nilikuwa nina mzgo mkononi

imagine nikiwa mdogo nimechukua glass nikazipanga nazipiga mateke, mama alinikuta kilichotokea nikawa na adabu mpk leo, siku nyingne nachapa kuku ety me ni mwalimu na kuku ni mwanafunzi oyaah

ningeachwa ningekuja kulisha mifugo sumu kisa ni mtoto
 
Back
Top Bottom