Hivi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaweza kuonesha chochote cha kujivunia kwa kipindi ana mamlaka haya? Anayekiona atuoneshe!

Hivi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaweza kuonesha chochote cha kujivunia kwa kipindi ana mamlaka haya? Anayekiona atuoneshe!

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Binafsi sioni ajenda ambayo aliisimamia yeye kama Waziri Mkuu na ikafanikiwa. Hakuna Mkoa utaenda au nchi kwa ujumla ukakuta mtu anasema hii imefanyika kwa sababu ya Majaliwa.

Anayejua anijuze.

Mzee pinda anakumbukwa kwa kilimo kwanza, Lowassa shule za Kata.
 
Fitna kwa Kassim Majaliwa zimeanza baada ya yeye kukaa kimya kwenye hili sakata la kuuza bandari.

Mnamchukia kwa sababu amegoma kushirikiana na nyinyi wezi, mashetani msiowajali watanzania. Tunasimama na Waziri Mkuu wetu dhidi yenu!

SAMIA ATUPISHE!
 
Sasa agome au asigome hana jeuri ya Kuzuia,sana sana Rais ananweza mvumilia Hadi 2025
 
Ngoja nikusaidie kukumbusha alichokifanya. Wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani ilikuta vijana wengi wanateketea kwa unywaji wa viroba, na ni PM majaliwa ndio aliyepiga marufuku ya utengenezwaji wa vile viroba. Hii ni kazi kubwa sana aliyoifanya ya kuokoa maisha ya watu.
 
Uendeshaji wa nchi yetu ni kwa a collective responsibility, na sio kwa individual initiatives, anayefanya kila kitu ni Mkuu wa nchi, Rais wa JMT, hivyo kila kinachofanywa na wasaidizi wa rais, wanafanya kwa niaba ya rais, hivyo credits, sifa na utukufu ni kwake tuu, rais wa JMT na sio kwa watendaji individual.
P
P

Yapi maoni yako kuhusu DP World?

Au na wewe umeshalambishwa bahasha?

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom