Hivi wenzetu mnaoweka status WhatsApp mnafaidika nini? Mna utoto mwingi sana

Hivi wenzetu mnaoweka status WhatsApp mnafaidika nini? Mna utoto mwingi sana

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817
Hii kitu imenishinda kabisa.

Kitu hunishangaza ni kuona mwanaume anaweka status, ile huduma imekaa kikike sana. Tena kwa mabinti wa seco labda na vyuo.

Wanawake imekuwa kama sehemu ya kupigana vijembe na hata midume nayo imeanza hizo pigo za kike.

Show off za kijinga jinga zimejaa kwenye WhatsApp status.

Kuna wale wanawekaga kila tukio lake la kila siku hata kama yuko njiani anatembea na mtoto wake.

Kwa nini uexpose kila kitu kuhusu maisha yako kwenye mitandao? Privacy is paramount.

Kuna wale watakuja kusema wanaweka biashara zao. Hakuna uhusiano wowote katika kufanikiwa kibiashara na WhatsaApp status. Watu wanapiga biashara way back hata kabla ya hizo status hazijaja utatuambia nini?

Kwa mtu aliye mature enough hawezi kufanya huu ujinga wa kuweka status.
​
 
Ni mtizamo wako..
Kuna watu mnachukizwa tu na mambo yasiyo ya msingi, mfano mwenzio akinenepa roho inakuuma. Mwenzio akufanikuwa unaumia , mwenzio akitingisha tako wakati wewe huna kishudu unaumia so si jambo jipya la kuhitaji mjadala wa kitaifa.
 
Huu mwaka wa kumi sasa sipo group lolote la watsapp, sijawahi kupost status, watsapp imejaa vumbi nishaisahau, sijawahi kupost chochote instagram tangu mwaka 2014


Usiwwshangae hao watu ni wapo kwenye Fast thinking, tulio ktk slow thinking huwa tunawasoma na kupita kimya kimya
 
Na wewe unaesoma stutus tukuchukuliaje...kwenye biashara unaenda sana mbinu zako za miaka kabla technology haijakuwa na ilivyo Sasa NI mbingu na ardhi...sikuhizi information zipo za kutosha unaweza kusahaulika...Sasa hivi nasoma jf nipo kitandani lakini miaka 13 nyuma ilibidi nitoke kitandani kikakae kwenye PC...wanafaidika wanoveiw na wanaifanyia biashara...
 
Huu mwaka wa kumi sasa sipo group lolote la watsapp, sijawahi kupost status, watsapp imejaa vumbi nishaisahau, sijawahi kupost chochote instagram tangu mwaka 2014


Usiwwshangae hao watu ni wapo kwenye Fast thinking, tulio ktk slow thinking huwa tunawasoma na kupita kimya kimya
Nakuelewa sana mkuu ulichoandika. Hiki ni kipimo cha maturity
 
Kila zama na zama zake, punguza sukari, Anza mazoezi, hudhiria sana Ibada, jitahidi usivunjike maana Itakua kazi kuunga, hizi ni zama zao Wana namna ya kuishi maisha Yao vijana, japo Wana limits ya kushea vitu, lakn kama mtu anapost kuelimisha, kuchekesha Kuna tatizo gani? Basi wasitumie kabisa mitandao ya kijamii!!
 
Hii kitu imenishinda kabisa.

Kitu hunishangaza ni kuona mwanaume anaweka status, ile huduma imekaa kikike sana. Tena kwa mabinti wa seco labda na vyuo.

Wanawake imekuwa kama sehemu ya kupigana vijembe na hata midume nayo imeanza hizo pigo za kike.

Show off za kijinga jinga zimejaa kwenye WhatsApp status.

Kuna wale wanawekaga kila tukio lake la kila siku hata kama yuko njiani anatembea na mtoto wake.

Kwa nini uexpose kila kitu kuhusu maisha yako kwenye mitandao? Privacy is paramount.

Kuna wale watakuja kusema wanaweka biashara zao. Hakuna uhusiano wowote katika kufanikiwa kibiashara na WhatsaApp status. Watu wanapiga biashara hata kabka ya hizo statu kuja utatuambia nini?

Kwa mtu aliye mature enough hawezi kufanya huu ujinga.
​
Mimi mwenyewe sipendelei kuweka chochote kwenye status page hata kubadili profile picture. Inaweza nichukua mwaka ndio nabadili kwa kuwa najua mwili wangu na sura vinabadilika muonekano. Hata hivyo ni tunaacha watu wawe huru. Zamani Album za picha zilipatikana sebuleni ili mgeni akija aangalie matukio leo Album ziko mtandaoni.

Ila wale wanaotangaza biashara kwenye status page zao wacha wafanye ndio faida chanya za utandawazi tusiwe primitive sana. Hatuwezi kuikataa technology na kuendelea kufanya mambo kizamani. Badala ya kuwatembela au kuwapigia watu simu kuwa una bidhaa fulani unauza unapost kwenye status wateja wanapatikana.
 
Hakuna uhusiano wowote katika kufanikiwa kibiashara na WhatsaApp status.
Inategemea na biashara unayofanya, Pia na aina ya watu ulonao, kama circle yako ni ya watu wa hovyo huwezi ona umuhimu wake.
Kwa mtu aliye mature enough hawezi kufanya huu ujinga.
Siyo kila kitu ambacho wewe hukipendi ni ujinga, kuna vitu vikikupita accept kwamba siyo mikato yako.
Kuna wale wanawekaga kila tukio lake la kila siku hata kama yuko njiani anatembea na mtoto wake.
Aina hii ya watu una Mute status zao haziwezi appear kwenye updates. Binafsi niligombana na wife kisa sikupost picha za harusi wala engagement 😆😆😆
 
Back
Top Bottom