Hiyo fedha unayoihangahikia na kuitolea macho kila ipo siku utagundua kuwa fedha si lolote, si chochote, ni suala la muda tu

Hiyo fedha unayoihangahikia na kuitolea macho kila ipo siku utagundua kuwa fedha si lolote, si chochote, ni suala la muda tu

Nimeona watu wenye fedha waliotumia zaidi ya milioni 100 kujitibu lakini fedha haikufua dafu wakafa.

Nimeona matajiri ambao kila mtu angetamani kuwa kama wao lakini hao Matajiri hawajawahi kupumzika hata wiki moja kuitafuta fedha.

Hii maana yake zile fedha zao mamilioni na mabilioni bado hayajaweza kuwapa jawabu la maisha. Wanaendelea kutafuta pesa na hawatapata jawabu na utulivu mpaka kifo kiwakute

Kwa hiyo masikini ndiyo wana majawabu ya maisha kuhusiana na utajiri?
 
Umegongelea kabisa. Wanavyoongea ni kana kwamba masikini hafi.
Hawajui hata maandiko yametaja vitu viwili kuwa ni ulinzi. Navyo ni hekima na fedha. Wenye vitu hivyo angalau hawateseki kama wasiokuwa na vitu hivyo.
Kweli.
 
Sure pesa sio kila kitu ila ni mbadala wa mengi.

Mkuu usiwe unakubaliana na kauli zinazofanya Afrika iwe hivi ilivyo. Hakuna sehemu ambako vitabu vinaruhusu uzembe na ugoigoi. Maandiko yanataja kabisa kwamba "kama hekima ilivyo ulinzi, ndivyo pesa nazo zilivyo ulinzi - Muhubiri 7 : 12"
 
Ni kweli pesa sio kila kitu ila ukiwa nazo unaheshimika mpaka na waliokuzidi umri kwahiyo kuna faida nyingi za kuwa na pesa kuliko ukiwa hauna pesa!
 
Nimeona watu wenye fedha waliotumia zaidi ya milioni 100 kujitibu lakini fedha haikufua dafu wakafa.

Nimeona matajiri ambao kila mtu angetamani kuwa kama wao lakini hao Matajiri hawajawahi kupumzika hata wiki moja kuitafuta fedha.

Hii maana yake zile fedha zao mamilioni na mabilioni bado hayajaweza kuwapa jawabu la maisha. Wanaendelea kutafuta pesa na hawatapata jawabu na utulivu mpaka kifo kiwakute
Tafuta sana pesa kwaajili ya nafas uliyonayo. Maana inawezekana upo hapo ili watu wengine wapate ajira watimize ndoto zao kupitia wewe so kila unachofanya humu dunian kifanye katika viwango vya juu kabisa maana umewekwa hapo muda huu wewe utimize mipango ya Mungu juu ya watu wake. So unapewa hela sio za kuharibu watu bali kutimiza mpango mpana wa Mungu kwa Dunia yake. Usisahau Sehem ya vitu vingi Mungu hufanya kwa kushirikiana na either Malaika au binadamu au tuseme viumbe vyake. Mungu anashirikiana na wazazi kukuzaa vivyo hivyo Mungu atashirikiana na wewe kuleta mabadiliko flan kwenye Jamii yako. Wewe unaweza kuhis ni wewe lakin nakuhakikishia unatumikia kusudio la Mungu kwa watu wake. Muhim kuwa na kias na usibadili matumiz ya neema kuwa laana.
 
Back
Top Bottom