Hizi ajira hazifai kugombewa na watoto waliosoma English Medium Schools[ EMS]

🤣🤣🤣🤣

Naunga mkono hoja
 
Upeo mkubwa huwezi poteza mamilioni ili uje upate laki 2 ya masimango huu ni upuuzi wa kiwango cha juu
Watu wote kupata elimu bora ni jambo la muhimu na pengine muhimu zaidi, bila kujali gharama inayotumika na itakayorudi. Ina maana wewe watoto wako elimu kwao umeifanya kama biashara?
 
Mtoto anayesoma hapa hafanikiwa kwa sababu ya Shule bali kwa sababu Kwao kuna Hela.

Tujue kutofautisha.

Tutafute hela watoto wasome pazuri ila sio kwamba hiyo shule inamchango mkubwa kwenye kutoboa, big no.
Mtoto anasoma shule ya English Medium darasa Lina wanafunzi wanane ana enjoy vipi mtoto hapo? Hujui mtoto anaenda shule kucheza kusocialize na wenzake? Shule nzuri Kwa mtoto ni shule ambayo ata interact na watoto wenzake Kwa wingi na kucheza michezo yote ya watoto
 
Elimu bora ni nini
Kumuelimisha mtu mafundisho fulani inabidi awe ana msingi wa kuyapokea. Kama hujui elimu bora, si ajabu kuona unapiga hesabu za ada na mishahara, na hauna msingi wa kuelimishwa. Inabidi tuanze nyuma kabisa kabla haujaelezwa kuhusu elimu bora
 
100% Fact
 
Bila kusahau kombolela😁
 
Kumuelimisha mtu mafundisho fulani inabidi awe ana msingi wa kuyapokea. Kama hujui elimu bora, si ajabu kuona unapiga hesabu za ada na mishahara, na hauna msingi wa kuelimishwa. Inabidi tuanze nyuma kabisa kabla haujaelezwa kuhusu elimu bora
Jibu swali Wacha sarakasi. Elimu bora ni nini?
 
EMS ni tofauti na hizo ulizotaja shule za IST. EMS hazina tofauti na shule za serikali ila ni shule ambazo zina standard ya miundombinu ambayo hata serikali yenyewe inajua ndiyo inapaswa kuwa standard ya shule.
Ukitaka kujua hilo tazama shule ya serikali kama Olympio, unaona miundombinu yake ni sawa na shule private za EMS.
Hivyo watoto wengi wa EMS bado wataendelea kugombea ajira na watoto wa shule za kawaida za serikali kwa sababu hakuna anything special zaidi ya kwamba wazazi hawakutaka wasome kwa kuhangaika sana hasa kwa suala la miundombinu.
 
Ajira ni free market, competition itakuwepo
Na zinapotangazwa hawasemi watoto wa shule fulani wasigombee

Matter of fact sidhani kama mzazi mwenye uwezo wa kupeleka mtoto IST , atakuwa hana uwezo wa kumpachika mwanae kwenye high position
 
Kujua lugha ya kimataifa ni muhimu sana hasa kama nchi yako sio superpower au yenye ushawishi mkubwa duniani
 
Ajira ni free market, competition itakuwepo
Na zinapotangazwa hawasemi watoto wa shule fulani wasigombee

Matter of fact sidhani kama mzazi mwenye uwezo wa kupeleka mtoto IST , atakuwa hana uwezo wa kumpachika mwanae kwenye high position
Kawazungumzia WA Shule za EMs za mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…