#COVID19 Hizi chanjo za Corona zinaenda kuondoa herd immunity tuliyoipata nchini

Waacheni wenye taaluma za afya watuvushe kwenye janga hili.
Taaluma gani? Eti taaluma!!!

Wangekuwa wana taaluma ya kweli tungeona wanatengeneza chanjo zao badala ya kushabikia machanjo ya mabeberu!

Hii nchi haina wanasayansi, kuna makasuku tu wanaosubiri kusikia wazungu wanasema nini, basi na wao wanakuja mbio mbio kutudunga masindano.

Hawa wanasayansi uchwara hatupaswi kuwasikiliza. Hawana uhalali wa kitaaluma wa kusikilizwa.

Ni makasuku yasiyojitambua.
 
MsemajiUkweli ni nani aliyekufundisha hii sayansi ya kuwa mtu aliyechanja akipata korona na kuambukiza mtu mwingine ambaye hajachanjwa basi korona inakuwa ni ya hatari zaidi? Hakuna ukweli ukweli wowote kwenye hii ''sayansi'' yako. Inaonekana nyie ndiyo mlimwingiza chaka Magufuli (RIP) mara kabla hajafariki, mpaka akasema kuwa kuna watu walikwenda nje kuchanjwa na wameleta korona mbaya sana. Na suala la herd immunity... Magufuli binafsi alikataza hatua zozote kuchukuliwa na aka-declare kuwa Tanzania ni free from korona, lakini herd immunity ilikuwa haijafikiwa. Kufikia herd immunity inatakiwa japo asilimia 70 ya population iwe imeshaambukizwa virus! Mabadiliko ya msimamo wa serikali ya sasa yanonyesha kabisa suala la kukataa kukubali ukweli kuhusu korona ilikuwa ni msimamo binafsi wa Magufuli. Na pia inaonekana alichukuwa msimamo mbaya kabisa wa kutaka herd immunity ifikiwe kwa sababu ugonjwa wa korona ni mbaya sana na mpaka lengo la kinga-kundi ije kufikiwa, watakuwa wamefariki watu wengi. Na bahati mbaya zaidi msimamo wake potofu ukamrudia yeye na akawa victim wa jaribio la kutojali maisha ya watu ili kinga-kundi ifikiwe.
 
Wewe acha ubishii. Hatutaki sayansi za kitapeli this time round.

Binadamu wote wana KINGA-ASILI za mwili. Kila kijidudu kinachovamia mwili kinashughulikiwa na kumalizwa na autoimmune system.

Kitendo cha watu kuambukizana corona kila mahali, kilifanya watanzania wote kujenga kinga ya asili ya mwili dhidi ya kijidudu huyo.

Ndio maana haukusikia vifo, kwa sababu miili yetu ilishajizatiti na kujilinda naturally.

Unapoenda kudunga watu machanjo ya hovyo hovyo unaharibu na kuvuruga kinga ya asili iliyokwisha kujitengeneza.

Matokeo yake ni kusababisha VIFO na autoimmune diseases.

Hiyo ndiyo SAYANSI YA KWELI, sio hizi habari za kitapeli za machanjo mnazotuambia.

Sayansi za kihuni tumeshazikataa hazina nafasi.
 
🀣 🀣 🀣 🀣Unatia huruma sana. Mbona watu hawajajenga kinga asili ya UKIMWI? Wewe kilaza usijujua hata kula balanced diet unabishana na sayansi ya wabobezi kutoka kila pande ya dunia? Nchi nyingine zote duniani ni wajinga na wabishi ndiyo maana wanakazana kuchanjwa raia wao ila wewe na watanzania wachache tu ndiyo werevu. Anyways kusikia ujinga kama huu siyo uncommon sana kwenye jamii dumavu.
 
Mbona watu hawajajenga kinga asili ya UKIMWI?

Hata maana ya UKIMWI tu hujui, ukielezwa habari za autoimmune utaelewa wewe ngumbaru?

Wewe ndio aina ya madokta uchwara ninaowatafuta mitandaoni ili nipambane nao KWERIII KWERII.

Zile habari za kuwalisha watu matango pori siku hizi hakuna. Watanzania wameelimika na wanajitambua.

Ndio maana nina uwezo wa kukukosoa wewe tapeli mshamba usiyejua hata maana ya UKIMWI lakini unashabikia watu wadungwe machanjo ya hovyo hovyo!

Huna ufahamu hata wa Basics tu za VVU Vs UKIMWI, lakini na wewe unajiita mjuzi!

Tena si ajabu kuna mahali wanakuita virologist [emoji23][emoji23][emoji23]
 
🀣 🀣 🀣 🀣Du. Kweli awamu ya tano ilitutengenezea ''wataalam''.
 
Hakuna cha ajabu. Tunachanja dhidi ya TB, na kila mwaka kuna watu wanakufa kwa TB. Tuna dawa nyingi za kutibu malaria, lakini kila mwaka maelfu hufa kwa malaria hata baada ya kupata tiba.

Kwa upande mwingine, kama mtu ana akili, ajiulize ni wangapi wangekufa kama watu wasingechanjwa dhidi ya TB, au ni wangapi wangekufa kama kusingekuwa na dawa za kutibu malaria? Hiyo herd immunity ifanye kazi kwa corona pekee lakini isifanye kazi kwenye malaria, TB, malaria, surua, dysentry, typhoid, etc. Ni ajabu!!

Mtu anaongelea herd immunity akiwa kwenye dirisha la dawa akinunua dawa yamalaria! Unafiki wa hali yajuu.
 
macho_mdiliko Nayaheshimu mawazo yako lakini nakubali kutokubaliana.

Kwa nchi kama Tanzania huhitaji kufikia asilimia 70 ya watu ili kutengeneza Kinga Kundi.

Sidhani kama katika analysis yako umeangalia kuwa nchini kuna asilimia 6 tu ya wazee lakini kundi lingine nila vijana ambao kwao korona haiwaathiri kama wazee kutokana na lifestyle ya kutafuta maisha na vyakula vya asili.

Hata hili kundi la wazee wengi immune system zao ni nzuri sana kwa sababu wanakula vyakula ambavyo nivya asili kwa sababu wengi wanakaa vijijini. Ndio maana korona haijaathiri sana nchi za Afrika kama ambavyo ilitegemewa.

Afrika Kusini wanaathirika sana na korona kwa sababu immune system yao ni ndogo kutokana na maisha yao ambayo kwa kiwango kikubwa yanategemea vyakula vya kwenye supermaket ambavyo sio asili lakini pia wananchi wake wengi wana magonjwa mbali mbali kama ukimwi na kisukali kutokana na maumbo yao ya mwili kuwa makubwa(unene).
 
Kuna Makopo mengi sana humu JF siku hizi..
Sasa kama kuna kinga za asili kwanini watu wanapewa Vitamins za viwandani ili wanywe?! Hao nazo ni sumu za Wazungu za kuwaua nyie Makapuku!
Na huo mwili wako hauna kinga za kudungwa hospitali utotoni?!
Ebu jadili na wengine huko...
 
Hiyo chanjo unadhani itakufikia kesho? Chanjo kukufikia huko kijijini ni baada ya miaka zaidi ya miwili!
 
Waliosomea wakianza kuchangia waanzie na kuweka vyeti vya taaluma yao? Hivi ndivyo akili yako inamaanisha.
Kama una swali uliza kama hujaelewa acha kuuliza taaluma
Nashukuru kwa kunisaidia kumuelimisha zaidi.
 
Kwani watu wote wanaofariki wanafariki kwa sababu hakuna dawa za kuwatibu? Hoja yako niya kitoto/mufilisi!

Kuwa na herd immunity hakuzuii baadhi ya watu kufariki kwa korona kama ilivyo kuwa na madawa ya kutibu ugonjwa fulani haizuii baadhi ya watu kufa kwa ugonjwa huo.
 
Awamu ya 5 ilizalisha, na kuchochea kuongezeka kwa watu wasiyo na maarifa na wasiotaka kutumia taaluma zao au akili zao kutatua changamoto zao
Wewe unayetumia ''taaluma yako'' umetatua changamoto zote na kufanikiwa au ndio wale wale?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…