Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000

Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000

Hii daraja la kawaida itakuwa ile inasimama kila kituo kuanzia Pugu,Soga...mpaka Makutopora.
Express bei lazima itakuwa juu zaidi.
Muda ni mali wengine tutalipa waweke japo treni moja ya express usiku tuwahi Dom asubuhi
 
Hii daraja la kawaida itakuwa ile inasimama kila kituo kuanzia Pugu,Soga...mpaka Makutopora.
Express bei lazima itakuwa juu zaidi.
Treni moja Ila mabehewa ndiyo Yana daraja mjumbe
 
606a318f0b80463c95d1a0443a2445f6.jpg
 
Tanzania Railways Corp to ndugu Masanja Kadogosa hiyo train ni ile ya kuokoteza kila kituo so haijali muda, kwa niaba ya tunaopenda mwendokasi naomba wekeni Express Train angalau asubuhi na jioni.

Mtaona faida yake kuliko hiyo inayosimama kila penye town center na penye serikali ya mtaa/kijiji.
 
Dar-moro itajaza Kama behewa za mbuzi,mabasi biashara itadoda
Mabasi biashara haiwezi doda labda kwa ambao hamjui ubovu wa kila biashara ya serikali. Tuombe uzima turudi hapa baada ya mwaka useme mabasi yalivyododa. Haitokaa itokee.

Watakuwa wanakula hasara, baadhi ya miundombinu itakufa mapema sana na hawatofanya matengenezo haraka, ratiba zitakuwa hazieleweki, wabongo wataleta umaskini kwenye hizo treni kisa ni za umma. Serikali ilete uswahili kwenye ndege sembuse treni
 
Naona wanatoa nauli za kawaida tuu, nauli za VIP zikoje? Ratiba vipi
 
Ksbls ys yote semina elekezi itolewe watu wataanza kuchafua kukojoa na haja kubwa hovyohovyo mabehewa yakaanza kunuka
Kabisa, wawekwe watu wa kutosha kufanya usafi wa hali ya juu, na sheria ziwe kali kukomesha watakaofanya uharibifu, makelele na uchafu, security wa kutosha waliopewa training ya hali ya juu waajiriwe wa kutosha na fine ziwe zinazidi nauli kukomesha wahuni na waharibifu
 
Nauli nzuri mno, mimi napenda watuambie safari ngapi kwa siku! Tunataka asubuhi tuwe tunaenda Dom , mchana tunakula bata kisha usiku saa 6 tupande treni ya express kurudi Dar. Treni za kusimama kila kijiji hatupendi, wengine tumezaliwa town huwa tunaboreka sana kutuweka bush masaa kadhaa.
Endelea kubeti na kunywa visungura.
 
Back
Top Bottom