Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000

Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000

Nazungumzia treni express na ya kawaida. Express haiwezi kusimama Pugu labda Morogoro tu then Dodoma. So far mabehewa waliyoleta yote yako sawa.
Kawaida hulali,madaraja mengine walala na msosi waletewa
 
Wajinga mko wengi sana, sehemu yoyote ya huduma ya jamii siyo lazima itengeneze faida, serikali inapaswa kutowa ruzuku ndio kazi ya serikali.
Upumbavu huu ndio umeua Tazara,mliambiwa watu Wana shida sana na usafiri wa treni kuliko Mabasi?

Huduma ya jamii ambayo Wananchi wanaweza kuimudu yaani Mabasi na ikaleta faida vs Huduma ya jamii ya kutumia mabilioni ya Dola kujenga na kuendelea kuendesha Kwa ahsraa ni matumizi ya hovyo ya Rasilimali, pumbavu sana
 
Wao Trc walipendekeza nauli iwe sh ngapi?
Ila walau wengefanya 45000 Dar-MAKUTUPORA,maana siyo Dodoma mjini ni mpaka Makutupora.
Makutupora ni mbali kutoka Dodoma,ni karibu kabisa na kupanda mlima Saranda.
Makutupora ni karibia na Singida.
Yani waweza sema ushaingia Singida.
Si wameweka bei 37,000/-?
Inafaa hiyo hiyo.
 
Stand ya Moro naskia itakuwa mwanzoni mwanzoni mwa mji kama ilivyo Stand ya mabasi ipo mwanzoni ukitokea Dar, sasa kivumbi n kutoka Moro - Dom mana Moro n kubwa.
Kituo cha Morogoro ni Mkundi darajani.
Kutoka Mkundi darajani mpaka Msamvu ni chini ya 5 kilometres.
 
Hii Treni itafeli haraka sana
1. Bei hazikuzingatia gharama za soko. Kutoka Pugu hadi Dar ni '' senti 30 dollar'' not realistic
2. Bei zimepangwa kisiasa na si kiuchumi
3. Treni ilitakiwa isimame katika vituo ya Ruvu, Morogoro, Kilosa, Dodoma. Hivyo vingine viachwe kwa ''ya Mwakyembe''
4. Ubora wa Treni utakwisha katika miezi si zaidi ya 3 na '' maintanance '' itaanza mapema sana, hasara itafuata

Biashara inaongozwa na soko na si siasa. Hii imeshafeli

JokaKuu

..Ni vigumu sana treni za abiria kuendeshwa kibiashara.

..treni za mizigo ndizo ambazo huendeshwa kibiashara.
 
Mabasi biashara haiwezi doda labda kwa ambao hamjui ubovu wa kila biashara ya serikali. Tuombe uzima turudi hapa baada ya mwaka useme mabasi yalivyododa. Haitokaa itokee.

Watakuwa wanakula hasara, baadhi ya miundombinu itakufa mapema sana na hawatofanya matengenezo haraka, ratiba zitakuwa hazieleweki, wabongo wataleta umaskini kwenye hizo treni kisa ni za umma. Serikali ilete uswahili kwenye ndege sembuse treni
Sawa kabisa ndege tu chali na ndiyo usafiri wa kuzingatiwa hasa sisi hizo mambo bado sana, kuna mabehewa yalinunuliwa mapya kabisa kutoka huko huko south Korea kwa reli ya MGR safari yake ya kwanza tu watu waliiba mapazia na kuharibu kioo.
 
Hii daraja la kawaida itakuwa ile inasimama kila kituo kuanzia Pugu,Soga...mpaka Makutopora.
Express bei lazima itakuwa juu zaidi.
Likianza Express notajaribu. Chap hadi Moro.
 
Now I can gues from mwanza to dsm by this transport. Pitia na upige kura yako hapa
 
Back
Top Bottom