Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000

👍
 
Hii daraja la kawaida itakuwa ile inasimama kila kituo kuanzia Pugu,Soga...mpaka Makutopora.
Express bei lazima itakuwa juu zaidi.
Wote wa madaraja tofauti si mnavutwa na kichwa kimoja, kikisimama mnasimama wote?
 
Wao Trc walipendekeza nauli iwe sh ngapi?
Ila walau wengefanya 45000 Dar-MAKUTUPORA,maana siyo Dodoma mjini ni mpaka Makutupora.
Makutupora ni mbali kutoka Dodoma,ni karibu kabisa na kupanda mlima Saranda.
 
Wao Trc walipendekeza nauli iwe sh ngapi?
Ila walau wengefanya 45000 Dar-MAKUTUPORA,maana siyo Dodoma mjini ni mpaka Makutupora.
Makutupora ni mbali kutoka Dodoma,ni karibu kabisa na kupanda mlima Saranda.
Dom had makutupora haizidi 30 km na hesabu za latra kwa km ni 69.51 hivyo hapo haizidi 2000
 
Hii Treni itafeli haraka sana
1. Bei hazikuzingatia gharama za soko. Kutoka Pugu hadi Dar ni '' senti 30 dollar'' not realistic
2. Bei zimepangwa kisiasa na si kiuchumi
3. Treni ilitakiwa isimame katika vituo ya Ruvu, Morogoro, Kilosa, Dodoma. Hivyo vingine viachwe kwa ''ya Mwakyembe''
4. Ubora wa Treni utakwisha katika miezi si zaidi ya 3 na '' maintanance '' itaanza mapema sana, hasara itafuata

Biashara inaongozwa na soko na si siasa. Hii imeshafeli

JokaKuu
 
Hongera kwa serikali kwani nauli zipo vizuri na zimepokelewa vema. Mwongozo wa kudhibiti huduma na Serikali kupata mapato ni mzuri.

Ishukubwa ni kusimamia huduma kwenye hili eneo pasiwepo na kuchekeana wala kujuana. Serekali imewekeza fedha nyingi lazima watendaji waelimishwe vya kutosha.

Pia kuwe na vipindi vya TV na redio kuwaelimisha abiria. Sio abiria kupanda na mbuzi na bata kwenye treni.

Pia mifumo ifanye kazi ya kuzuia hujuma yoyote inayoweza kujitokeza. Taratibu zinazotumika airport zitumike kwenye hizi treni.


Hongera TRC Hongera Serikali. Nasubiri safari ya kwanza.
 
Treni moja Ila mabehewa ndiyo Yana daraja mjumbe
Nazungumzia treni express na ya kawaida. Express haiwezi kusimama Pugu labda Morogoro tu then Dodoma. So far mabehewa waliyoleta yote yako sawa.
 
Waweke na nauli kwa daraja lisilo la kawaida tuone.
 
Tikiti siyo za dirishani unakata mwenyewe kupitia simu yako, jitahidi uwe unasafiri kwa mabasi hata kama hauna kwenu mikoani ujue jinsi ya kukata tikiti kupitia simu yako.
nitashangaa sana kama Trc watauza hizo ticket manual, maana hadi mabasi siku hizi ticket tunakata online.
Maana yake abiria watakuwa wengi kuliko nafasi. Nauli rafiki sana ingawa bus iko chini kidogo.
 
Zimekaa poa kwetu na kwa mujibu wa latra, ila Sidhani kama ni rafiki kwa Trc., proposal yao ya nauli ilikuwa juu mno na nina wasiwasi wakitumia hizi nauli za latra moja ya tatizo litakaliwakumba litakuwa ni huduma mbovu.
Mwendokasi walipendekeza nauli yao iwe 1,200/- wakapangiwa 650/- kilichotokea zimekuwa hovyo kuliko daladala. Hawa pia wamepangiwa nauli za chini itakuwa kama mwendokasi. Wataanza vizuri sana ila baadae itakuwa kama treni la Kigoma.
 
Kwa nauli hizo lazima shirika life.
 
Wote wa madaraja tofauti si mnavutwa na kichwa kimoja, kikisimama mnasimama wote?
Kuna express na ya kawaida inayosimama kila kituo. Ukiwa na tiketi ya kawaida huwezi kupanda express.
Kuhusu madaraja hili la kawaida huwa inakuwa daraja moja. Ila express kuna madaraja tofauti na nauli tofauti. Nauli ya chini kabisa inazidi ile ya treni ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…