Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000

Hiyo treni ina sehemu ya kubebea kuku na viazi?
Huko kwenye hizo bei lazima ukutane na huo ujinga.

Kwanza treni nzuri inayokupa fursa ya ku enjoy safari ni Tazara huko kwingine ni kama unataka kufika haraka tuu nothing else but itawasaidia watu maskini ingawa sijui kama watapata faida
 
Zimekaa poa kwetu na kwa mujibu wa latra, ila Sidhani kama ni rafiki kwa Trc., proposal yao ya nauli ilikuwa juu mno na nina wasiwasi wakitumia hizi nauli za latra moja ya tatizo litakaliwakumba litakuwa ni huduma mbovu.
Ndio maana nimesema kupelekea uchaguzi Serikali itabeba hasara ila baada ya uchaguzi Mkuu zikiendekea hizo nauli ,shirika litakufa fasta
 
Mwendokasi walipendekeza nauli yao iwe 1,200/- wakapangiwa 650/- kilichotokea zimekuwa hovyo kuliko daladala. Hawa pia wamepangiwa nauli za chini itakuwa kama mwendokasi. Wataanza vizuri sana ila baadae itakuwa kama treni la Kigoma.
When politics interfere technical matters, hicho unachokiongea ndio exactly kimetokea mwendokasi na kitatokea huku Trc, ni swala la muda tu.
Miradi mingi ya serikali kama ingeangaliwa kwa jicho la kiufundi ilikuwa hakuna haja ya kuianzisha, yote itakufa kibudu. Huku ikiwa imetutia hasara walipakodi.
 
Pole, Dar to Dom itatumia saa 14
 
Serikali kwenye sekta ya biashara hawajawahi kufanya vizuri.

Anyway, naskia safari zinaanza mwakani 😎
 
Ksbls ys yote semina elekezi itolewe watu wataanza kuchafua kukojoa na haja kubwa hovyohovyo mabehewa yakaanza kunuka
Ustarabu huwa haufundishwi bali na makuzi anayokuwa nayo mtu toka utotoni!! Ndio maana usafiri kama wa ndege ningumu kukuta vitu vya ajabu ajabu kwani wanaoutumia wengi ni wastarabu. Nenda kwenye treni /mabasi ya kigoma ni aibu tupu.
 
Kongole..Bei ni Rafiki sana...Tunaomba hii kitu ipite nchi nzima kwa sasa tunabaguliwa watu wa mikoani !!
 
mwanzoni biashara ya serikali inakuwa nzuri ila ikitokea taa ya ndani ya behewa imeharibika au hata siti kuharibika itabaki hivyo hivyo na hapo ndio utajua kwanini serikali ni zero kwenye biashara. Check mabasi ya udart magari machafu utadhani hakuna maji Dar. Viti vimeharibika na camera zile zinaning'inia hadi unajiuliza hela za mradi ule zinaenda wapi ikiwa hawawezi hata kukarabati gari.

Serikali pamoja na wasomi wake wote wakipewa kampuni ya mabasi kama ya Shabiby hawataweza kuiendesha kwa faida na mabasi yakawa katika hali bora kama yanavyoonekana barabarani.
 
Angalau bei ni ridhishi.
Ila ni kama zinalingana na za basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…