Hizi hapa takwimu za hasara aliyopata Putin na Urusi, vifaru 684 vilifyekwa kwenye msafara

Hizi hapa takwimu za hasara aliyopata Putin na Urusi, vifaru 684 vilifyekwa kwenye msafara

Leta source ya $570b wacha kukwepa na maneno mengi.
Mm siwezi kupoteza muda kukuletea chanzo wakati habari ilitangazwa na kila chombo cha habari kama hukuiona ni uzembe wako.
 
Hiyo sio sawa kabisa.. na ni dalili mbaya mno kwasababu ni Kama wanaitafuta attention kwanguvu ya watu ili wapate nguvu na support ya kuishusha Russia.. ni sawa na kumchokoza Mmbwa alafu akianza kukukimbiza unasema huyu "Mmbwa Ana kichaa naomba auliwe"..[emoji28][emoji28][emoji28]

Mchezo anao ucheza US na NATO unajulikana.. watu wengi wanaifatilia hii Vita kwa karibu mno pamoja na kwamba upande mmoja unapendelewa zaidi
Kosa la NATO lingine ni kulazimisha nchi zingine zijenge uadui na Urusi katika vita ambayo haiwahusu

Ila kinachokuja kunishangaza kwenye hii vita ni pale ambapo wananchi wa Urusi wakiandamana kupinga uvamizi unaofanywa na raisi wao

Kinachokuja kuchanganya zaidi ni pale ambapo wabongo wanakuwa wazalendo sana na urusi kuliko warusi wenyewe ambao mpaka wamediriki kuandamana kuzuia vita isiendelee
 
Mkuu kwani haiwezekani au?
Global power mwaka juzi kama sikosei walitoa takwimu kuwa urusi ina miliki tanks mara mbili ya marekani.

Kipindi hicho marekani alikuwa anamiliki tanks 6000 ambapo ukizidisha mara mbili ni 12,000 na ndio record kubwa kidunia

Sasa labda kama katika kipindi cha miaka miwili utuambie Urusi alifanikiwa kutengeneza tanks 8,000 yani kwa miaka miwili kaweza kutengeneza idadi ambayo ni mara 2 kasoro ya idadi ya vifaru vya marekani ambayo ana miliki katika carrier yake yote ya utengenezaji wa tanks za kivita
 
Sasa Russia ana nini cha maana zaidi ya 'kuwekeza kijeshi' only to realize hata jeshi lenyewe kumbe mdebwedo
Jeshi mdebwedo naniwakati sahihi huu wa NATO kwenda kuliondoa jeshi mdebwedo linaloiadhibu UKRAINE kama lilivyofanya IRAQ VIETNAM YUGOSLAVIA AFGHANISTAN nk
 
Sio kweli hakuna unachofahamu hapo na wala hiyo sio pesa kwa nchi za magharibi. Bonds za Russia zinazoshikiliwa na nchi za magharibi tu zinaizidi hiyo pesa na tayari wameshaanza kuzitumia kuikarabati Ukraine hata bila kuiambia Russia.

Usicheze na G-7 wewe, hao ndio wanahodhi uchumi wa dunia na kila mtu anatamani awe mshirika wao wa kibiashara ndio maana leo Iran anabembeleza ule mkutano wa 6+1 ufanyike ili Marekani amuondolee vikwazo vya kiuchumi.

Na ni kwa mantiki hiyo hiyo China anamkwepa rafiki yake Russia asije akamponza.
UCHINA hamkwepi RUSSIA nabado anafanya biashara nae mnapata faida gani kudanganya!!!
Kuhusiana na IRAN pia IRAN hajawahi kumbembeleza mtu kuongea nae kuhusiana na mkataba wa NYUKLIA ila waliovunja ndio wanalialia kila leo kwamba IRAN anakiuka makubaliano yakwenye mkataba husika
MUACHE KUTUDANGANYA
 
Kwenye swala la kuzuia vyombo vya habari za urusi hapo ndo western wamebugi

Sijajua wamefanya hivyo kama vikwazo au kupunguza temper za raia wasisikie madhara wanayopata watu wa Ukraine au namna gani
Wamezuia ili kuwalisha propaganda kama vile kipigo wanachokula huko hao wa UKRAINE wanawaaminisha kwamba jamaa wanaongoza kumbe hali tete
Wanawaaminisha kwamba RUSSIA wamekimbia KIEV kumbe wamekubaliana ndio wakasepa
Sehemu pekeee ambayo UKRAINE anashinda hii vita nikupitia ama kwenye MEDIA ila sio huko field
 
Kosa la NATO lingine ni kulazimisha nchi zingine zijenge uadui na Urusi katika vita ambayo haiwahusu

Ila kinachokuja kunishangaza kwenye hii vita ni pale ambapo wananchi wa Urusi wakiandamana kupinga uvamizi unaofanywa na raisi wao

Kinachokuja kuchanganya zaidi ni pale ambapo wabongo wanakuwa wazalendo sana na urusi kuliko warusi wenyewe ambao mpaka wamediriki kuandamana kuzuia vita isiendelee
MKUU hakuna jambo lolote utakalolifanya eti ukaungwa mkono kwa 100 hilo hakuna nahalitawahi kutokea
Watu walioandamana RUSSIA niwachache mnooooo mnooo bora wale waalioandamana kushinikiza NAVALNI mpinzani wa PUTIN aachiwe huru walikua mamia kama sio maelfu
waandamanaji wale hawakuzidi hata miambili
Asilimia kubwa wananchi wa RUSSIA wapo bega kwa bega na PUT IN ma serikali yake kwenye hii OP
Kama wengi wangekua wanaandamana ama kupinga kama unavyosema hio ndio ingekua habari kubwa kwenye western media lakini wapiii
 
Warussi wa kwa mtogole mmepigwa kitu kizito mpaka mmepoteza network kwenye bongo zenu
 
Wamezuia ili kuwalisha propaganda kama vile kipigo wanachokula huko hao wa UKRAINE wanawaaminisha kwamba jamaa wanaongoza kumbe hali tete
Wanawaaminisha kwamba RUSSIA wamekimbia KIEV kumbe wamekubaliana ndio wakasepa
Sehemu pekeee ambayo UKRAINE anashinda hii vita nikupitia ama kwenye MEDIA ila sio huko field
Tatizo la wengi hawajadili uhalisia wanajadili hisia

Mimi nilikuwa sielewi kuwa kwenye hii vita kuna dhana ya udini iliyowagawa watu kimakundi, mpaka nilipokuja kuona analysis kutoka kwa Great thinkers wa JF

Kwamba kuna mtu anai support Ukraine au Urusi lakini sio kwasababu ya facts kwamba Ukraine au Urusi anastahili kusapotiwa kwasababu ni haki yake na anapaswa kuitetea. Ila ana sapoti Ukraine au Urusi kwasababu ya implications za kidini kuwa nyuma ya pazia kunalo taifa ambalo linai support Ukraine au Urusi hilo taifa ni la dini fulani ambayo mtu huyo ndio anaiamini
 
MKUU hakuna jambo lolote utakalolifanya eti ukaungwa mkono kwa 100 hilo hakuna nahalitawahi kutokea
Watu walioandamana RUSSIA niwachache mnooooo mnooo bora wale waalioandamana kushinikiza NAVALNI mpinzani wa PUTIN aachiwe huru walikua mamia kama sio maelfu
waandamanaji wale hawakuzidi hata miambili
Asilimia kubwa wananchi wa RUSSIA wapo bega kwa bega na PUT IN ma serikali yake kwenye hii OP
Kama wengi wangekua wanaandamana ama kupinga kama unavyosema hio ndio ingekua habari kubwa kwenye western media lakini wapiii
Naskia jamaa ni raisi ambaye anaogopeka kwa sheria kali, hivyo hao waliothubutu kuandamana halafu wakakamatwa kuna dalili nyingi za kupewa adhabu kali

Halafu hiyo takwimu ya watu 200 sina hakika nayo kama iko sahihi na siwezi kujua exactly kipi ni chanzo sahihi ikiwa kila taarifa inadaiwa ni propaganda
 
Waendelee tu kutwangana mpaka wese lifike buku tano za kibongo huku wamatumbi tukiendeleza ushabiki wa mzungu gani mbabe..
 
Dunia aindeshwi kienyeji kama unavyo fikiri hela zina tafutwa haziokotwi usi dhani pesa inatolewa kienyeji kienyeji na bure bure.

Na wala usidhani hizo nchi za magharibi zina wapenda sana raia wa Ukraine bali wapo hapo kwa maslahi yao hakuna pesa za burebure atakazo zipata Ukraine.

Hata hizi silaha unazoona wana pereka Ukraine ni mikopo na si misaada kama wanavyo tangaza watatakiwa kulipa siku za mbeleni baada ya vita.

Hiyo hela ni ndogo kuitamka lakini ni pesa ndefu mno.

Mpaka sasa ulaya na Marekani bado kuna mamilioni ya watu hawana makazi wanaishi kwenye mabaraza ya nyumba na maduka wakiumizwa na baridi sasa kama wana pesa za kumwaga kwanini wasiwajengee kwanza nyumba raia wao wanao teseka na baridi.
Ngoja nikwambie basi naona unataka kuleta joto., Katika mazungu kule Turkey, Urusi walikubali kulipa izo gharama zote wajenge wao ukraine lakini Donbas iwe majibo huru na cremea iwe sehemu ya russia lakini Ukraine walikataa wakasema hela za kujenga ukraine tunazo na tutajenga wenyewe, walikataa kataka kata na wakasema hawako tayari kusamehe hata cm 1 ya majimbo ya Donbas na cremea kuchukuliwa kama sehemu ya russia, sasaiv ninavyoandika vita inaendelea Donbas ukraine kugomboa hayo majimbo.

Iwe ni kwa mkopo ama ni kwa vipi hizo hela tayari ziko mikononi mwa Zelensky., mimi na wewe tu ndio hatuna hela tunashinda hapa jf
 
Hivi kujenga hayo magorofa ya ukraine yanayobomolewa kila siku ni dollar ngapi na uchumi uliopolomoka ukraine mwezi hamna kazi zinafanyika kweli sisi ukraine hatupotezi russia ndo anapoteza
We naye kaanzishe uzi wa alivyopoteza Ukraine
 
Drones za Uturuki ni hatari sana, na ndio dunia inakoelekea, ujeda wa kukaa ofisini ukibonyeza bonyeza, sio ubabe wa kupasua matofali kwa kichwa.
_____________

Ukraine’s Armed Forces reported that Russia also lost 684 tanks, 1,861 armored personnel carriers, 1,324 vehicles, 332 artillery systems, 107 multiple launch rocket systems, 55 anti-aircraft defense systems, 135 helicopters, 150 aircraft, 76 fuel tanks, 96 UAVs and 7 boats.

View attachment 2182172

April-5-2-1024x1024.png

CNN, BBC,VOA,DW...... wamekuharibu akili.
 
Mm siwezi kupoteza muda kukuletea chanzo wakati habari ilitangazwa na kila chombo cha habari kama hukuiona ni uzembe wako.

Siku nyingine uwe makini usitaje taje herufi bila kujua unachoongea kuhusu au chanzo, kisa ulisikia huko kijiweni, fahamu kunao tunafuatilia sana huu ugomvi na tupo makini sana.
 
UCHINA hamkwepi RUSSIA nabado anafanya biashara nae mnapata faida gani kudanganya!!!
Kuhusiana na IRAN pia IRAN hajawahi kumbembeleza mtu kuongea nae kuhusiana na mkataba wa NYUKLIA ila waliovunja ndio wanalialia kila leo kwamba IRAN anakiuka makubaliano yakwenye mkataba husika
MUACHE KUTUDANGANYA
Hakuna unachojua hapo, Iran ameshaiuliza Marekani mara ngapi kuhusu mkutano Marekani akamwambia Russia ndio inachelewesha.

Kumbe Russia anaona mazungumzo yakienda vizuri itafanya Iran aruhusiwe kuuza tena gesi na mafuta na kuweza kuwanyang'anya soko wao Russia.

China hawezi kuongeza volume ya biashara yake na Urusi kwani ameambiwa akicheza Taiwan inaweza ikajitangazia uhuru.
 
Kumbe tunabishana na watu wasio na uelewa wowote.
Dunia haiendeshwi kienyeji namna hiyo.
Pesa zimezuiliwa tu na wala hazujachukuliwa
Huwezi kutumia pesa za nchi nyingine kienyeji namna hiyo.
Eti nchi za magharibi hela sio tatizo ?

Nchini Marekani na Ulaya kuna mamilioni ya watu hawana makazi wana kufa kwa balidi kwa nn wasitumie hizo hela ambazo wanazo nyingi kuwa jengea makazi raia wao?
Kuna billions za dola za Iran zilizuiliwa Marekani toka mwaka 1979 sasa unataka kuniambia kwamba Marekani wamewatunzia tu Wairan hizo pesa zaidi ya miaka 40, hujui kwamba zingine ndio walitumia kuwanunulia neti.
 
Back
Top Bottom