Hizi Harrier 3rd gen zilivyojazana hapa mjini utasema haziuzwi Mil 70+

Hizi Harrier 3rd gen zilivyojazana hapa mjini utasema haziuzwi Mil 70+

Mkuu hamna gar ya mil 3 niamini Mimi, ukinunua hiyo gar utakua na namba za mafundi zaid ya watano. Maana week haiishi upo na fundi.
Sio kweli mkuu, mie nilikuwa na Spacio Old model haikuwa na shida yeyote, nilimtumia Kwa takriban miaka 9 nikaiuza Kwa bei hiyo. Alienunua hakubadili chochote na aliisafirisha zaidi ya km 500. Mpaka Leo haijawahi msumbua kitu chochote Cha ajabu tofauti na service za kawaida tu.
 
Tusioyakubali magari ya Japan tunapita hapa huku tunacheka kama tumemeza fundo la maji, like pfuu. Mil 70 shaah! Mjep ni Cruiser tu kwingine hakuna kitu.

Binafsi nisiwe mnafiki hakuna gari ya Japan huwa inanistua labda LC 200 na 300 series kidogo...ndio nije nilipe M70 kwa hivyo vidude kanaondoka injini inatokota niache kununua mnyama BMW,Audi au Cayenne aa bado
 
Mimi ndoto zakuwa tajiri naona zimepotea maana umri unakimbia sana hata baskeli Sina, licha ya kipato changu kufikia 5Mil kwa mwezi lkn ndoto at least za kupata mil 30 kwa mwezi zinaniishia.

Wenzetu wanawezaje kununua gari za mil 100 au 80 cash. Mambo ya mikopo ya sitaki kuyasikia.

Tupen code wakuu.
Mkuu wewe kibongobongo ni milionea, ktk watu million 60 nchini nadhani wenye kipato kama chako hamzidi million 10, tunaijua hali halisi ya maisha ya watanzania, hivyo hata wewe ni tajiri haswa, kwa hali yetu

Huwa nashangaa sana watu wenye uwezo wa kumake not less than 5 million per month bado wanajitoa ktk kundi la matajiri, wakati huo ninyi mko ktk Ile 10% ya Tanzanians elites😂, utani tu, kazana unaweza kufikia malengo yako
 
Una kipato cha milioni 5 kwa mwezi huna hata baiskeli, 🤣🤣 sasa hapo hata mungu si anakushangaa,

Chunguza akili yako vizuri nahisi shida inaanzia hapo🤣
Kwa hela yake Mimi ningemletea Toyota paso ya million 4, alafu baiskel 2 za mazoezi na chenji ikibaki tunampa mke hapo maisha keshayapatia, Kawa tajiri Sasa anaweza kuwakolomea majirani zake😂
 
Kwa hela yake Mimi ningemletea Toyota paso ya million 4, alafu baiskel 2 za mazoezi na chenji ikibaki tunampa mke hapo maisha keshayapatia, Kawa tajiri Sasa anaweza kuwakolomea majirani zake😂
😁😁😁
 
Back
Top Bottom